Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Ni ajabu kwamba tumeshindwa kuelewa udhaifu wa mfumo wetu wa afya, tumeshindwa kuelewa baiolojia ya COVID-19, tumeshindwa kuzuia mizunguko ya binadamu au usambaaji wa COVID-19, tumeshindwa kuzuia sara zisizokuwa na faida katika maisha yetu. Kilicho simamia maamuzi ni siasa. Ukweli ni kwamba tutakwisha.
Serikali iwe sikivu. Tumefikia hatua hata nchi kama Burundi sasa inatufukuza! Burundi kwa utawala wa kisela! Hata kama itakuwaje, Tanzania tujitafakari!
Ni aibu kuendelea kuruhusu mikusanyiko ya kunywa pombe na kutegemea eti watu binafsi watajitambua. Uelewa wetu haufikii kiwango hicho, na kama ungefikia kiwango hicho, basi wenyewe tungeomba kufungiwa hata kusafiri.
NGONGEZA: Rais aliwahi kusema anayeugua kipindupindu, awekwe rumande. Imekuwaje Corona tunabembelezana na kutegemea uelewa wa raia tu!