Hii sio wiki nzuri kwa nchi zetu za Afrika Mashariki hasa Tanzania na Kenya. Wakati Kenya wanaandamana kihuni kupinga kupitishwa kwa sheria mpya ya fedha huku Tanzania kuna mgomo wa wafanyabiashara. Hawa wafanyabiashara wana hoja kadhaa za msingi ingawa pia wanazo hoja zingine za kipumbavu. Baada ya kutazama kwa kina huu mgomo nimeona tatizo kuu ni BUNGE LA TANZANIA kupitisha sheria za hovyo mno. Kinachoendelea kwa sasa ni kulipishana kodi juu ya kodi. Sina haja ya kuelezea watu wanalipa kodi kiasi gani kwasababu kuna nyuzi nyingi humu zimeelezea. Kimsingi HAZILIPIKI.
Hatutaweza kuwabadili wabunge ghafla bila kubadili kifungu cha katiba kinachoruhusu hata mwendawazimu kuingia bungeni kisa anajua kusoma na kuandika. Ukitazama bunge utaona ni wabunge wachache sana wanaoweza kuchambua muswada uliopelekwa bungeni. Wengi wao wakisimama ni kuomba serikali iwajengee daraja au zahanati jimboni. Hivi kwenye ulimwengu wa kidigitali hata barabara iliyopo maporini si inaonekana tu? Utakuta ni muda wa kujadili muswada wa sheria ya elimu mbunge anasimama kuomba serikali ijenge barabara ya kijijini kwake.
Ninashauri sana serikali pia ishtuke kuwa hata hawa polisi tulio nao ni polisi wa kizazi kipya ambao hawajui mambo ya "Zidumu fikra za mwenyekiti".. hawa wa sasa nao wanataka maisha mazuri na sio kuishi kwa dhiki makambini. Ipo siku nao watasapoti wananchi. Mwaka 2008 kuna jamaa alipost yuko na watoto wake wenye umri kama miaka 4 hadi 8 wakiwa wamevaa gwanda za CHADEMA. Wale watoto kwa sasa ni watu wazima kwahiyo kama walikuzwa na baba mpinzani tayari hapo ni shida.