Bila kumkamata huyu, siri za kutekwa Kibanda hazitajulikana

Hii mashine ya kazi. Inawezekana yeye hakushiriki moja kwa moja kwenye hili jambo, lakini akihojiwa anaweza kutoa mwelekeo wa picha kamili.

Kama wana usalama wanaingia humu JF, waamini maneno yangu.

JF ni jukwaa huru,ingawaje tunaelewa hofu yako kwa hali iliyopo sasa Tanzania,ila unaweza kusema zaidi ili tumfahamu huyu bwana wapi kazi zake na ni nani,je nae ni mfanyakazi polisi? maana hapo juu unasema alipata taarifa akiwa polisi usiku wa manane.
 
kuna uhusiano gani hapa jacton au umeamua kumuuzia kesi jamaa coz alikuwa na mjengwa mi naona matukio yalifuatana tu.ukiwa polisi kwa muda waweza jua mambo mengi yalizotokea
 
Plus other points zilizopo hapo chini toka mwanzoni nilishasema nani mjinga kiasi hicho kupanga mikakati ya kuua mtu kwenye mazingira kama hayo???

Policcm wakifanya kosa hakika watakuwa watu wa kwanza kuingiza nchi kwenye taharuki isiyo na sababu. Hii kitu ifuatiliwe kwa makini kweli lakini ukweli upo clear. The Video is FAKE HATUNA HAJA YA KUPELEKA KWA WATAALAMU WA LIP READING HATA MTOTO WA DARASA LA KWANZA ANAWEZA KUTAMBUA KUWA HII CLIP IMEPIKWA. AS FOR LUDOVIC HAHAHA HE DEFINITIVELY ANAFAHAMU MENGI KUHUSU HII CLIP NA KUTESWA KWA KIBANDA


Hii ameandika mwana JF mwenzetu de'levis

======================================

Nilikuwa sina nia ya kuandika sana humu lakini baada ya kusoma comment yako nimelazimika kusema kitu...jambo lolote unaloambiwa , kuliona au kulisikia ni lazima ushughulishe akili kufikili ili ujiridhishe kama ni la kweli au la vinginevyo utakuwa unakubaliana na jambo ambalo si la kweli...jaribuni kuipa nafasi akili yenu kufikiri.... bahati mbaya sana katika siku za hivi karibuni imeonekana watanzania wengi sana wana tatizo la kutoipa akili nafasi ya kufanya maamuzi na kung'amua na mmoja wao ni Pasco....wachache wanaipa akili nafasi ya kufikiri.

Kuna matukio mengi sana na mengine wengi hamuyafahamu ambayo yanalenga kuichafua image ya taifa na kwa kuwa matumizi ya technolojia nchini yamekuwa yakikuwa kwa kasi hasa matumizi ya simu na intanet na kwa kuwa techolojia inakuwa kwa kasi na hivyo wengi wanashindwa kwenda sambamba na ukuaji wake na hivyo wanajikuta wanakubaliana na kila kitu wanachokiona ama kusikia..

katika mkanda huo ambao wewe pasco unauita ni ''bonafide and genuine'' nimefanikiwa kuuona jana mchana na mimi na wenzangu tumekaa na kuupitia kwa makini kabisa na kwa njia za kisasa zilizotusaidia kujua uhalisia wake... mkanda huo ni fake na tayari taarifa imeshatolewa....hata wewe pasco ukijipa mda wa kukaa na kuipa akili yako nafasi utagundua kuwa mkanda ule ni fake vinginevyo utakuwa unasumbuliwa na '' invincible ignorance''

Chini hapa nitakusaidia kidogo ili walau upate picha ya kuwa mkanda ule ni fake...

00:01 ------Sauti inaanza kwa kutamka ‘’MIKE’’ na kisha kuuliza ‘’ HAPO?’’ maana yake watu hawa wanajiandaa kuanza kujirekodi na wakati wa nafanya editing waliyaacha maneno hayo

00:15 ..........sauti ya mtu wa pili inasikika ikisema ‘’ TUTANOTE TENA HAPO’’ ...inaelekea watu hawa kuna mahali walikosea na kusema watarudia mahali hapo...

00:28 .......Binti anaonekana akija dirishani na kisha anaondoka baada ya maongezi mafupi na mwenzake aliyoko upande wa pili wa dirisha.

01:45......Sauti ya mtu mwingine ambaye baadae alikuja kutambulika kama ‘’RICH’’ anasikika akiwasalimia lakini aliyesalimiwa(lwakatare) kulingana na picha na mdomo wake inaonekana si yeye aliyeitikia ’’ marahaba’’..kuthibitisha hilo mara baada ya salamu msalimiwa hakugeuka kumwangalia anayesalimia ila aliendelea na shughuli zake na papo hapo kijana anayeonekana na kupewa maelezo mara moja anaanza mazungumzo na kijana (rich) aliyekuwa anasalimia na ndipo anamwita jina hilo ‘’rich’’ na wanapeana pole za matatizo na habari za sikukuu nk. katika mazungumzo mtu anayeonkena kwenye clip(lwakatare) bado haeguki kumwangalia huyo rich badala yake anaendela kutoa maelezo namna ya kudhuru watu.... hapa kuna abrakadara katika clip hii......

03: 15......wakati mazunguzo na melekezo toka kwenye clip ya lwakatare yakiendelea kwa mbali anasikika binti anayemkaribisha mtu mwingine na pia anasikika akisema ‘’ napanda maua’’ na anamalizia na neno ‘’karibu ingia ndani’’..( ili kumsikia binti umakini unahitajika kidogo)

03:20.....inasikika sauti mtu akikoroga chai kwenye meza yalipokuwa yanafanyika mazungumzo na anarudisha kijiko kwa kugonga meza lakini picha inayoonekana haimuoneshi mtu huyo na wala hakuna dalili za kuwa kwenye meza ya lwakatare kulikuwa na kikombe cha chai na kuwa chai ile ilikorogewa pale.. ...na pia kwa kufatilia kwa makini mtu anayekoroga chai si yule aliyekuwa anapewa maelekezo.... kitu kingine ni kwamba clip nzima quality ya sauti ya lwakatare haisikiki sawa sawa kama sauti ya mtu wa pili (kijana anayepewa maelekezo) ...

05:35 .....sauti inasikika ikitamka ‘’ UNAELEWA LAKINI?’’ lakini ukiangalia kwa makini mdomo wa lwakatare hakutamka neno hilo badala yake mdomo unaonyesha ametamka ‘’ UMELIONA HILI?’’ ni sawa na pale alipokuwa akisalimiwa na ‘RICH’’ hakutamka neno ‘’marahaba ‘’ na badala yake neno alilotamka kulingana na mdomo ulivyoonekana alitamka ‘’ YOTE MUHIMU’’ na ndio maan hakugeuka kumwangalia yule aliyekuwa anasalimia kama ilivyoelezwa hapo juu..

05:57... Sauti inasikika ikitamka kuwa ‘’kama tulivyofanya hii ya morogoro kisha kwenda igunga’’ swali la kujiuliza hapa ni mauaji yapi yalitangulia? Ya morogoro au igunga?..... bado ushahidi unaonyesha video hii ni ya kupika..

07:36.....Sauti inasikika ikisema ‘’ dawa aina mbali mbali vidonge, unga ama liquid form fanya utafiti ujue zinapatikana wapi na ni bei gani; ni rahisi mno kama tulivyofanya utafiti wa mgongolwa tukapata ile kitu’’ hapa pia kunachanganya inawezekanaje kijana anapewa jukumu la kutafuta bei na upatikanaji wa madawa wakati huo huo akikumbushwa namna walivyopata ‘’ ile kitu’’ kwa mgongolwa ambapo kijana alishiriki ...maana yake kijana anajua bei na wapi yanapatikana...( who is mgongolwa by the way?)

15:59 ...sauti inasika ikisema ‘’ unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ‘’LUDOVICK’’ ndiye unamfatilia’’...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

17:10 kijana anayepewa maelekezo (‘’Ludovick) anauliza ‘’ kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?’’ lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema ‘’ Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza’’ ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

19:20...Lwakatare anaonekana akiongea kwa mdomo na vitendo(kuchezesha mikono) huku kichwa chake na macho vikielekea kwa kijana(ludovick) aliyesimama/ kukaa mbele yake ..mara gafla kitu kinadondoka chini na kijana anainama kukiokota lakini bado lwakatare akiongea kichwa na macho vikiangalia juu alipo kijana na kijana anaitikia mmmh, mmmh mara gafla clip inakatwa na kuishia hapo... hapa pia kunamkanganyiko mkubwa... na hakuna uhusiano wowote wa maneno yale na picha inayoonekana na tukio la kudondoka kitu chini..... binafsi naamini clip ingeendelea kuanzia hapo sura ya mtu wa pili ingeonekana hasa mara baada ya kuokota kitu kilichodondoka na ndio maana clip imeishia hapo.......


Pasco unaweza kuishabikia clip hii kama bonafide genuine kama na wewe ni mmoja wa washiriki wake au basi ni ushabiki wa kipuuzi ...anyway hata hivyo taarifa juu ya uhalilisia wa clip hii imetolewa....
 
Bill Mkuu,mimi nimekubaliana nawe kwa hiyo analysis na nyongeza pia ni kuwa hapa mjini Dar Es Salaam hakuna mtu mjinga wa kukuta watu wamepanda kwenye bajaj na muda ule wa usiku halafu wakakwambia tuchangie twende wote na mbaya zaiidi eti ukakaa katikati yao!
 
Mbona unaanza kulia! Tulia
alaf case yako imekwisha?

kuna uhusiano gani hapa jacton au umeamua kumuuzia kesi jamaa coz alikuwa na mjengwa mi naona matukio yalifuatana tu.ukiwa polisi kwa muda waweza jua mambo mengi yalizotokea
 
Ndugu Ludovick, sijakuelewa vizuri.

  1. Usiku saa 5.30 unatembea na vitu vyote hivyo, sheikhKilango/Manzese. Hauwezi kuwa serious.
  2. Ukapanda bajaji usiku wote huo,ukakaa katikati yao. Mhhhhh! Jambo la kufikirika.
  3. Mabibo relini wakakunyang'anya begi lenye vitu vya thamani, hawakulifungua. Hivi unadhani watu wote ni mabwege, kwani shida yao kubwa ilikuwa nini?
  4. Kigogo mwisho walikushusha ukaanza kuwadai begi lako. Wewe mwendawazimu, yaani mamba kakutema kisha mwenyewe unarudi tena mdomoni kwake!!!!!!!!!
  5. Ukarudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo ukakuta kituo kidogo cha polisi Kigogo. Yaani hawa vibaka wamekutoa sehemu ambayo hakuna kituo cha polisi, wakaenda kukushusha kituo cha polisi, du basi nchi hii hatuwezi kusalimika. Acha upuuzi, yaani hatua kumi, ushindwe kumwita polisi ama kukimbilia kituoni hadi unavuliwa nguo???
  6. Polisi walikupa gari ukaelekea Hotelini kwa Mjengwa. Ina maana vituo vidogo siku hizi vina magari? Kwa nini haukuenda nyumbani kwako? Dogo unajifunza usanii sio!!!

Hawa wapuuz wanadhani kila kitu ni ni kwa manufaa ya siasa?? Hii movie wameikosea sana kupanga script zao. Kama polisi walipeana taarifa hizo usiku wote huo kwa nini tukio lenyewe liliripotiwa asubuhi?? Hata kituo cha polisi aliporipoti Ludovick wanahusika kwa namna moja au nyingine nao wanatakiwa kuhojiwa akiwamo aliyetoa hiyo RB,
 
Mojawapo ya sifa ya uongozi bora ni kutatua matatizo yanayoonekana kana kwamba hayana mlango wa kutokea.

Hata wao ccm wanajifunza mengi juu ya matukio wanayotuletea CHADEMA na namna tunavyoyatatua.
Kwa tatizo hili la Lwakatare na jinsi litakavyotatuliwa, itakuwa ni uthibitisho mwingine mbele ya jamii kwamba CHADEMA inao uwezo wa kushika uskani wa Taifa hili na kukabili matukio na kuyatatua.........

Hiki ni kipimo bora cha kuwaonyesha wananchi uwezo CHADEMA ilio nao wa kung'amua mambo ya sirini na kuyadhibiti na nchi ikawa salama.
 
Kama ni mwana CDM hakika jogoo hatawika mara tatu kabla ludovic hajafkishwa oysterbay. Ila kama ni "Iyena iyena"hilo halitakaa litokee,
 
Ndugu Ludovick, sijakuelewa vizuri.

  1. Usiku saa 5.30 unatembea na vitu vyote hivyo, sheikhKilango/Manzese. Hauwezi kuwa serious.
  2. Ukapanda bajaji usiku wote huo,ukakaa katikati yao. Mhhhhh! Jambo la kufikirika.
  3. Mabibo relini wakakunyang'anya begi lenye vitu vya thamani, hawakulifungua. Hivi unadhani watu wote ni mabwege, kwani shida yao kubwa ilikuwa nini?
  4. Kigogo mwisho walikushusha ukaanza kuwadai begi lako. Wewe mwendawazimu, yaani mamba kakutema kisha mwenyewe unarudi tena mdomoni kwake!!!!!!!!!
  5. Ukarudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo ukakuta kituo kidogo cha polisi Kigogo. Yaani hawa vibaka wamekutoa sehemu ambayo hakuna kituo cha polisi, wakaenda kukushusha kituo cha polisi, du basi nchi hii hatuwezi kusalimika. Acha upuuzi, yaani hatua kumi, ushindwe kumwita polisi ama kukimbilia kituoni hadi unavuliwa nguo???
  6. Polisi walikupa gari ukaelekea Hotelini kwa Mjengwa. Ina maana vituo vidogo siku hizi vina magari? Kwa nini haukuenda nyumbani kwako? Dogo unajifunza usanii sio!!!

Nimefurahi uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja. Hii ndo aina ya watu wanaotakiwa JF.
 
Swali zuri. Una habari kwamba tukio la Kibanda kutekwa na kuteswa halikuripotiwa hadi asubuhi? Hii redio call aliyosikiliza yeye ilikuwa ya polisi gani? Siwezi kudadavua zaidi, subiri usome JAMHURI ijayo.

da mkuu hebu niondoe ki-dot kwa kunihakikishia hili
 
Leo usiku yapata saa tano na nusu niliachana na Maggid Mjengwa maeneo ya Shekilango tukitokea Rose Garden.yeye alielekea hotelini alikofikia,sehemu fulani kariakoo,nami nikasubiri kigari kuelekea nyumbani kwangu.hapo shekilango,magari yalichelewa kidogo,pembeni ilipaki bajaji ikiwa na watu 2 na dereva.ndipo wakaniambia twende tuchangie mia tano tu kwenda ubungo mataa.
huyo Ludovick anaishi wapi hapa dsm?
 
Manyerere pamoja na post yake ni nini hasa uhusiano wake na tukio lenyewe?mkuu funguka kwa undani tupate picha,maana huenda ni kweli aliibiwa ama si kweli,kwa vyovyote wewe utakuwa unajua kitu kuhusu Ludovick.funguka mkuu tupate mwanga
 
Asante sana kwa link hii.

Haya ni maelezo yanayopatikana huko. Sasa nimeelewa ujumbe wa Manyerere Jackton

Leo usiku yapata saa tano na nusu niliachana na Maggid Mjengwa maeneo ya Shekilango tukitokea Rose Garden.yeye alielekea hotelini alikofikia,sehemu fulani kariakoo,nami nikasubiri kigari kuelekea nyumbani kwangu.hapo shekilango,magari yalichelewa kidogo,pembeni ilipaki bajaji ikiwa na watu 2 na dereva.ndipo wakaniambia twende tuchangie mia tano tu kwenda ubungo mataa.nikakaa katikati ya hao jamaa.
Ghafla wakakata kona na kuanza kuelekea mabibo na wakiulizana kama wako kamili,na mwingine kujibu yuko kamili.nikajua tayari niko mikononi mwa majambazi na sikujua wako kamili namna gani,kwa hiyo nikaamua kuwa mtulivu.Tulipofika relini karibu na mabibo,wakanipokonya begi lakini hawakulifungua.( ndani yake kulikuwa na laptop,toshiba kubwa,na chaja yake,kamera ndogo ya digital na USB yake,modem ya zantel na card reader.).tulipofika maeneo ya loyola sekondari nikawasihi wanishushe ili nirudi mwenyewe,wakaniambia safari ile inaishia jangwani.nikaingiwa na wasiwasi mkubwa na nia yao hasa.maana wameshanipokonya begi,kwa nini wasiniachie? lakini niliendelea kuwa mtulivu ili kutowa provoke.
Tulipovuka kigogo mwisho kwenye giza karibu na msikiti,wakasimama pembeni ya barabara na kuniamuru kushuka.nikashuka na kuanza kuwadai begi langu.ndipo mmoja akasema wamekuwa wastaarabu mimi naanza kuwadharau.Ghafla akanivuta kwa nguvu kunirudisha kwenye kibajaji,akamwambia mwenziye wanisachi kama nina vitu vingine.wakanisachi na kuchukua pesa (nilikuwa na elfu 35) na simu mbili ndogo za nokia.moja yenye line mbili.kisha mmoja akatoa order nivuliwe nguo.Nikavuliwa viatu,T shirt na suruali.nikabaki na nguo za ndani pekee.wakanishusha na kuniacha hapo.
Kurudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo kituo kidogo cha polisi Kigogo.nikaanza kutoa maelezo hapo kwa zaidi kama ya saa 2 nikiwa uchi na nguo za ndani tu.Nikiwa hapo nikasikia polisi wakiwasiliana juu ya tikio la kupigwa vibaya ABSALOM KIBANDA kwenye redio calls.ilikuwa yapata saa nane.baada ya kuchukuliwa maelezo,polisi walinipatia gari nikaelekea hotelini kwa Maggid,ambaye saa kumi aliamshwa na kunichukulia chumba hapo nikapumzika.ameniazima nguo zake ndizo nimevaa bado hadi sasa.naelekea kituo cha polisi Magomeni kwenda kupewa mpelelezi wa kesi yangu.namba ya case yangu kigogo ni KIG/RB/318/2013 (WIZI KUTOKA MAUNGONI).
Namshukuru Mungu hawajanijeruhi wala kunipiga.namshukuru Maggid kwa msaada wake hadi sasa.MUNGU NI MWEMA: LUDOVICK

Shekilango ... Shekilango! Hata Bashe alisema gari lilokuwa likiwawinda yeye na Kibanda lilikuwa huko huko Shekilango
Soma hapa; www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=46667

Haya, TISS unganisheni dots vizuri
 
Ndugu Ludovick, sijakuelewa vizuri.

  1. Usiku saa 5.30 unatembea na vitu vyote hivyo, sheikhKilango/Manzese. Hauwezi kuwa serious.
  2. Ukapanda bajaji usiku wote huo,ukakaa katikati yao. Mhhhhh! Jambo la kufikirika.
  3. Mabibo relini wakakunyang'anya begi lenye vitu vya thamani, hawakulifungua. Hivi unadhani watu wote ni mabwege, kwani shida yao kubwa ilikuwa nini?
  4. Kigogo mwisho walikushusha ukaanza kuwadai begi lako. Wewe mwendawazimu, yaani mamba kakutema kisha mwenyewe unarudi tena mdomoni kwake!!!!!!!!!
  5. Ukarudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo ukakuta kituo kidogo cha polisi Kigogo. Yaani hawa vibaka wamekutoa sehemu ambayo hakuna kituo cha polisi, wakaenda kukushusha kituo cha polisi, du basi nchi hii hatuwezi kusalimika. Acha upuuzi, yaani hatua kumi, ushindwe kumwita polisi ama kukimbilia kituoni hadi unavuliwa nguo???
  6. Polisi walikupa gari ukaelekea Hotelini kwa Mjengwa. Ina maana vituo vidogo siku hizi vina magari? Kwa nini haukuenda nyumbani kwako? Dogo unajifunza usanii sio!!!
[/QUO
vibaya ni hakuna anayejiuliza maswali haya zaidi ya wewe mkuu, polisi wako bize kui-save CCM. bila ubishi Ludovick anahucka
 
Mkuu, angalao ungetufahamisha tu huyu Ludovick ni nani hasa. Mengine tutawaachia wafuatiliaji wa mambo.

katekwa na kuachwa salama salimini mmh!kapokonywa laptop na simu mmh!kasikia taarifa ya kibanda juu juu kwa staili hiyo mmh!anamtajataja blogger mmh!ila kuna kadot kanamis hapa..aliipost lini hiyo taarifa humu na tukio la kibanda liligundulika muda gani!...hebu...akapelekwa muhimbili...askari wanataarifiana..mabibo mbezi...hebu...aaargh!
 
Bashe alitaja saa 5 usiku, Shekilango
Ludovick anataja saa 5 usiku, Shekilango

Kwa hiyo; SHEKILANGO SAA 5 USIKU NOMA!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom