Bila kumkamata huyu, siri za kutekwa Kibanda hazitajulikana

Sasa mbona sipati link ya moja kwa moja ya jinsi huyu jamaa alivyo husika kwenye tukio au kuwa primary source kwenye incidence yenyewe. Kwa mujibu wa maelezo ya huyu jamaa ni kwamba wakati akiwa polisi kuripoti tukio lake aliwasikia polisi wakitarifiana kupitia radiocalls kuhusu tukio la kibanda. Na hii ni kawaida kwa polisi kuripoti matukio ya sehemu mbalimbali kupitia radiocalls katika vatuo vyao au makao makuu. Na kwa jinsi navyo fahamu radiocalls za polisi huwa hazina siri kwani taarifa zake husikika katika kwa polisi mwingine yeyote mwenye radiocall. Sasa je huyu Joseph Ludovick anawezaje kuwa chanzo cha taarifa cha moja kwa moja cha tukio eti kwa kuwasikia tu polisi wakiwasiliana kutokea kwa tukio la kibanda kupiti radiocalls?

Ndugu, ni hivi: Kwenye ule video ya Rwakatare, kuna sehemu Rwakatare anamwambia maneno haya huyo anayezungumza nae: ''Hajui ni nani adui, ni nani.... unanielewa.... yaani unamwacha kwenye nanihii.... anakuja hapa anakutana na Ludovick'' Sasa hii inaonyesha kuwa Rwakatare alikuwa anazungumza na mtu anayeitwa Ludovick.
Wakati huohuo, Kibanda alipoumizwa, kuna bwana anaitwa Ludovick alipost story kwenye blog moja eti ameporwa na akaenda kuripoti polisi. Alipokuwa polisi akasikia ma-polisi wanawasiana kwenye radio call kuwa Kibanda ameshambuliwa. Hii ilikuwa ni usiku na habari za Kibanda zilikuwa hazijasambaa.... HALAFU hata maelezo yake ya kuporwa yanaacha mashaka makubwa. Jaribu kuyasoma wewe utaniambia kama majambazi hutumia style ya namna hiyo kupora mtu.....
 
Kamanda una akili sana. Hapo ndo kwenye point. Safi kabisa! Umenisaidia kuiainisha hoja yangu. ubarikiwe
Hata hayo maelezo ya huyo jamaa anayeitwa Ludovick ya kuporwa hayajaniingia akilini! Ukisoma mtiririko wake ni kuwa majambazi hawawezi kukunyanganya vitu halafu wanakuachia vingine, halafu ukiwauliza ndio wanamalizia kukunyanganganya vile vilivyobaki.
 
Huku kwetu Jamhuri hatuipati mkuu, sijui unatusaidiaje, tuna kiu pia ya kujua kilichojiri


Wapi huko huko ndugu yangu, kwa sababu JAMHURI linasomwa karibu kila kona ya nchi hii. Tafadhali nieleze ili nami niwaombe wasambazaji wafikishe JAMHURI huko kwako.
 
Au ndo njia ya kuiuza JAMHURI?Kama ulijua kila kitu utakiweka ktk JAMUHURI,Why coming here?
 
Mengi tutaendelea kusikia mpaka kufikia 2015. JOSEPH LUDOVICK ni nani Jamani?

Huyu bwana ni moderator wa mjengwa blog. Anafanya kazi na Majid Mjengwa, vifaa alivyo taja kwenye post yake chini (laptop, modem, na card reader) bila shaka unaweza kuunganisha nukta kuwa ndio vitendea kazi vyake.

Ukienda hatua tatu mbele kwenye maelezo yake alisema "Nilimsindikiza Majid kwenda kulala hoteli..." Kwa maana hiyo ni mtu wa karibu na Majid (kijana wa majid).
 
Kamanda una akili sana. Hapo ndo kwenye point. Safi kabisa! Umenisaidia kuiainisha hoja yangu. ubarikiwe
Nimeamini tuna watu mnaojua kuunganisha dots! hata mimi imeniingia akilini kwa jinsi ulivoeleza na jinsi alivyokimbia kupost habari ya yeye kutekwa na kuripoti polisi! Thanks sana mkuu kwa ku-play your part! kilichobaki ni kwa vyombo vya dola kufanya kazi yake kama wana utashi huo!
 
Kweli kuna kitu kwa huyu Ludovic! anahusika na kumtesa kibanda!au kutengeneza ile video akajirekodi bahati mbaya!
 
Au ndo njia ya kuiuza JAMHURI?Kama ulijua kila kitu utakiweka ktk JAMUHURI,Why coming here?

Huu ni uwanja wa kupashana habari. Sidhani kama kuna dhambi kuileta habari hii. ukitaka uchambuzi zaidi, soma JAMHURI (siyo JAMUHURI). Jamhuri lina wasomaji ambao hawahitaji mbwembwe na vikorombwezo; bali wanahitaji detail facts
 
Swali zuri. Una habari kwamba tukio la Kibanda kutekwa na kuteswa halikuripotiwa hadi asubuhi? Hii redio call aliyosikiliza yeye ilikuwa ya polisi gani? Siwezi kudadavua zaidi, subiri usome JAMHURI ijayo.

njaa zitawaua nyie waandishi makajanja, kumbe hapa unatangaza biashara ya gazeti len la kipropaganda! Kwann we mwenyewe usiende polisi kutoa maelezo kama unajiamin? Je una tofauti gani na yule mpuuzi aliweka video yotube badala ya kupeleka ushahid polisi kama kweli ana uchungu pia anajiamin? Pia unatofauti ganna mwigulu aliyekuwa abwabwaja kuhusu CD ya mauji badala ya kuipeleka polisi?
Huu ni upumbavu mkubwa wa kusingiziana pasipo ushahidi ila kwa kuongozwa na chuki binafsi na ninashangaa hao mods thread kama hii inaendelea hadi muda huu.
 
Kweli kuna kitu kwa huyu Ludovic! anahusika na kumtesa kibanda!au kutengeneza ile video akajirekodi bahati mbaya!

Usiwe mwepesi kufanya conclusion namna hii mkuu. Kuna watu wanakaa wanapanga mpango na unapangika. Tuwe watulivu kwani hii ''movie'' inaonekana imepangwa na watu wenye ujuzi na kwa kutumia mbinu ya hali ya juu. Usije kuna hata hii thread ni moja ya hiyo mikakati....!
 
Usiwe mwepesi kufanya conclusion namna hii mkuu. Kuna watu wanakaa wanapanga mpango na unapangika. Tuwe watulivu kwani hii ''movie'' inaonekana imepangwa na watu wenye ujuzi na kwa kutumia mbinu ya hali ya juu. Usije kuna hata hii thread ni moja ya hiyo mikakati....!

Mkuu nakupata, ishu ya Kibanda tutaona mengi, lkn mwishowe majahili watajulina tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom