Bila kumkamata huyu, siri za kutekwa Kibanda hazitajulikana

Angalia vizuri video ya Lwakatare yule aliyekuwa anapewa maagizo ndio mashine yenyewe ya Mbowe, au muulize Shonza.

Ya Lwakatare cha mtoto, ANGALIA video ya shehe ILUNGA anavyoagiza waislamu waue mapadre!.. Na kweli ndani ya miezi 6 padri mmoja kajeruhiwa vibaya kwa risasi na mwingine kauawa!. Cha ajabu ILUNGA yuko mtaani anakula BATA!...
 
Hebu mkuu funguka zaidi. Huyu Joseph Ludovick ndo nani hasa. Tukiweza kujua kazi au nafasi yake katika taifa hili tunaweza kupata mwanga wa jinsi gani anaweza kuwa mtu muhimu katika kesi hii.

Amesema alipata taarifa usiku wa manane kupitia simu ya Upepo sina shaka atakuwa polisi au mtu wa usalama na hivyo inawezekana ndo waliohusika kufanya hicho kilichotokea.
 
Lakini mkuu Manyerere usijekuwa kama Mzee Mwanakijiji,anaanzishaga vitu vingine halafu anatuacha hewani
hivyohivyo'Funguka ueleweke'
Mkuu ukiona hivyo basi ujue hana uhakika na anachokisema!
 
Hii mashine ya kazi. Inawezekana yeye hakushiriki moja kwa moja kwenye hili jambo, lakini akihojiwa anaweza kutoa mwelekeo wa picha kamili.

Kama wana usalama wanaingia humu JF, waamini maneno yangu.

Ndugu yangu Manyerere Jackton kwanza kabisa mimi niseme ninakuheshimu sana kwa kazi yako ya uandishi wa habari ulio makini na ukweli tangu nimekufahamu ukiwa mwananchi communication hadi leo hii Jamhuri Media.

Kama unataka kulitendea haki jukwaa hili la JF, kumtendea haki swahiba wako Kibanda na kulitendea haki taifa lako la Tanzania basi unatakiwa utueleze kinagaubaga huyu Joseph Ludovic ni nani na kadri unavyofahamu alishiriki vipi katika mpango mzima wa kumteka na kumtesa Kibanda.

Vinginevyo nataka kuamini kwamba nawe umeamua kuanza kupiga propaganda kwa lengo unalolifahamu wewe mwenyewe. Kwani kwa namna ulivyoanzisha hii thread na kuiacha bila kuijaziliza nyama basi hujawatendea haki wanaJF ili waweze kutafakari kwa ukamilifu juu ya mtu huyu na involvement yake katika uharamia uliofanywa dhidi ya Kibanda.
 
Last edited by a moderator:
Hii mashine ya kazi. Inawezekana yeye hakushiriki moja kwa moja kwenye hili jambo, lakini akihojiwa anaweza kutoa mwelekeo wa picha kamili.

Kama wana usalama wanaingia humu JF, waamini maneno yangu.

hii ndo kijiwe cha wana-uhasawa wa taifa. Watapita tu na kuona. Shida ni utashi wa kufuatilia
 
kama nimewahi kusoma vizuri umbeya, basi niliona kwamba huyo jamaa ana uhusiano na blogger mmoja maarufu
 
Ndugu yangu Manyerere Jackton kwanza kabisa mimi niseme ninakuheshimu sana kwa kazi yako ya uandishi wa habari ulio makini na ukweli tangu nimekufahamu ukiwa mwananchi communication hadi leo hii Jamhuri Media.

Kama unataka kulitendea haki jukwaa hili la JF, kumtendea haki swahiba wako Kibanda na kulitendea haki taifa lako la Tanzania basi unatakiwa utueleze kinagaubaga huyu Joseph Ludovic ni nani na kadri unavyofahamu alishiriki vipi katika mpango mzima wa kumteka na kumtesa Kibanda.

Vinginevyo nataka kuamini kwamba nawe umeamua kuanza kupiga propaganda kwa lengo unalolifahamu wewe mwenyewe. Kwani kwa namna ulivyoanzisha hii thread na kuiacha bila kuijaziliza nyama basi hujawatendea haki wanaJF ili waweze kutafakari kwa ukamilifu juu ya mtu huyu na involvement yake katika uharamia uliofanywa dhidi ya Kibanda.

Ndugu yangu, kwanza nikushukuru sana kwa heshima yako kwangu. dunia ya leo ukiambiwa na mtu yeyote kuwa anakuheshimu, shukuru Mungu!

Mimi nimeshatekelezaa wajibu wangu kwa jamii. ni wajibu wa wahusika kutafakari na kufuatilia hili nililowambia. Habari za uchunguzi nimezifanya kwa miaka mingi. Sina shaka na ninalolisema, hasa ukizingatia kuwa ni jambo zito na la kutishia uhai wangu. Lazima zote tuhakikishe Tanzania panakuwa mahali salama pa mtu yeyote kuishi-awe ni mwanahabari, injinia, mwanasiasa, mkulima, mmachinga, dereva, konda, mhudumu wa mochwari na yeyote awaye. Tanzania for Tanzanians!!
 
Wadau, mimi nilishajua kuna siku nitakufa. Lakini kabla sijafa nasema bila Polisi na Usalama wa Taifa kumkamata mtu anaitwa Joseph Ludovick, hawatakaa kamwe wajue kilichojificha kwenye sakata la kumteka na kumuumiza Kibanda. Huyu mtu ni muhimu sana kumnasa na kumhoji. Liwalo na liwe. Amini, naawaambia. Mkitaka kujua, unganisheni alichodai kimemtokea usiku ule alioumizwa Kibanda. Akadai alipata taarifa za kuumizwa Kibanda kupitia redio ya upepo akiwa polisi usiku wa manane.
google say's https://www.google.co.tz/search?q=J...rg.mozilla:en-US:official&client=firefox-beta
 
Angalia vizuri video ya Lwakatare yule aliyekuwa anapewa maagizo ndio mashine yenyewe ya Mbowe, au muulize Shonza.

ha ha ha a a a! Mama kumbe upo? Msalimie mmeo mwigulu chemba, akirudi atakuletea zawadi ya kumuwakilisha vyema.
 
Taratibu tutasikia mengi sana kuna mwingine tena nasikia anaandaa press coference jumapili kusema ya kwake tusubili harafu mkionganisha kitapatikana kitu sasa ukweli unakalibia hata kabla vyombo vya usalama havijatoa taarifa.
 
Ndugu yangu, kwanza nikushukuru sana kwa heshima yako kwangu. dunia ya leo ukiambiwa na mtu yeyote kuwa anakuheshimu, shukuru Mungu!

Mimi nimeshatekelezaa wajibu wangu kwa jamii. ni wajibu wa wahusika kutafakari na kufuatilia hili nililowambia. Habari za uchunguzi nimezifanya kwa miaka mingi. Sina shaka na ninalolisema, hasa ukizingatia kuwa ni jambo zito na la kutishia uhai wangu. Lazima zote tuhakikishe Tanzania panakuwa mahali salama pa mtu yeyote kuishi-awe ni mwanahabari, injinia, mwanasiasa, mkulima, mmachinga, dereva, konda, mhudumu wa mochwari na yeyote awaye. Tanzania for Tanzanians!!

nakumbuka kuna mtu alisema kwamba na yeye alitekwa, the same day AK alipotekwa
 
Mkuu, angalao ungetufahamisha tu huyu Ludovick ni nani hasa. Mengine tutawaachia wafuatiliaji wa mambo.
 
Wadau, mimi nilishajua kuna siku nitakufa.

Lakini kabla sijafa nasema bila Polisi na Usalama wa Taifa kumkamata mtu anaitwa Joseph Ludovick, hawatakaa kamwe wajue kilichojificha kwenye sakata la kumteka na kumuumiza Kibanda.

Huyu mtu ni muhimu sana kumnasa na kumhoji. Liwalo na liwe.

Amini, naawaambia. Mkitaka kujua, unganisheni alichodai kimemtokea usiku ule alioumizwa Kibanda. Akadai alipata taarifa za kuumizwa Kibanda kupitia redio ya upepo akiwa polisi usiku wa manane.
Kinachonishangaza siku hizi ni polisi kutumia mitandao ya kijamii kufanya upelelezi,mtu kaja na mkada wa lwakatare,polisi hao mbio,sasa na ww umekuja tena,!haya tusubiri nani mwingine atakuja.Sijawahi kuona Jeshi la Polisi kama hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom