Bila kulipa kodi tutarudi nyuma, Watanzania waelimishwe

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,037
1,154
Baada ya kusomwa kwa bajet ya serikali kwa mwaka 2021/22, kumekuwa na mijadala lukuki kuhusu vyanzo vya fedha kupitia ulipaji wa kodi. Serikali imekuwa ikiwaogopa wananchi kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa kulipa kodi, badala yake inabuni mbinu za kufidia kodi matokeo yake makosa.

Uoga wa serikali kuwatoza kodi watanzania directly ni kujikomba na kuweka mtaji wa kisiasa kwa kuogopa kuchukiwa na Wananchi.Hii tabia ya watanzania kutokujua umuhimu wa kulipa kodi na kutolipa kodi moja kwa moja tunachelewa kimaendeleo.

Serikali ina uhakika wa kodi kwa watumishi wa umma tu ambao hawana ujanja, ila haipati kodi kutoka kwa Wananchi na wafanya biashara. Mfano ukienda Kariakoo wafanyabiashara wenye maduka makubwa hawalipi kodi badala yake wanatoa bidhaa nje huku wakitumia vijana kuwauzia.

Watanzania kutokulipa kodi ni tatizo linalotengenezwa na serikali yenyewe, hizo njia nyingine ni usumbufu tu, mwishowe Watanzania wanashindwa kujua umuhimu wa kulipa kodi.
 
Wameanza kodi ya nyumba na kodi ya bando. Tuendelee ili wote tuwe tunalipa kodi. Kodi wanayolipa asilimia tatu ya watu mil 60 haiwezi kutosheleza.

Ndio maana biashara nyingi zinafungwa maana zinabeba kodi zisizo bebeka. Tukianza kuchangia kodi sisi sote, tutaanza kuwa wakali kuona kodi zetu zinatumika ipasavyo
 
Back
Top Bottom