Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Katika awamu hii ya uongozi Polisi imetokea wanahangaika sana na kauli ndogondogo zinazotolewa dhidi ya Magufuli au serikali. Hizi kauli nyingine za wanasiasa ni kuacha tu zipite. Wanasiasa lazima wapayuke, la sivyo wanakuwa sio wanasiasa. Sasa kujaribu kuwafumba midomo wanasiasa ni sawa na kumwambia mwalimu asifundishe.
Hamna haja ya Polisi kutumia nguvu nyingi, wakati na kodi za wananchi kukimbizana na kauli za wanasiasa au kisiasa. Inaweza kuonwa pia ni Polisi kujipendekeza kwa Magufuli. Ukweli ni kwamba mara nyingi kitendo cha Polisi kufuatilia ndicho kina ubaya zaidi kuliko kama wangekaa kimya, maana wengine tunapata ujumbe juu ya kauli hizi kwa kuwa Polisi wamefuatilia kuliko kama wangeziacha.
Baba yako akitukanwa au kusemwa mbele ya watu watatu ni afadhali ukae kimya ili athari yake isienee. Ukienda kutoa malalamiko magazetini juu ya tusi alilotukanwa baba yako, wewe ndio unamtukana baba yako mbele ya mamilioni ya watu. Kimsingi Polisi wanatumika kama "promotion tool" pale ambapo wanafuatilia kauli ambazo wangeziacha zingepita tu na upepo.