Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,347
- 11,447
Kwa furaha kubwa naandika nikitoa shukrani kwa Serikali ya Jam ya Muungano na pia Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kuamua rasmi siku ya kumaliza Corona.
Hatua hii ni kubwa na najua Mabeberu itawaumiza sana kuona nchi maskini imeweka siku maalumi ya kumaliza Corona na maisha kurudi upya.wao bado wanahangaika nayo.
Leo nlipokuwa napita barabarani nawaona wauza barakoa najiuliza nikitabasamu baada ya Jumapili watauza nini sasa? Wengine nimewashauri hizi barakoa walizobaki nazo wauze hata tsh 100 ili wamalize mapema.
Naona kabisa sanitizer hazitakuwa deal tena, maana za nini na Corona tunaenda kui lockdown Jumapili? Nashauri lifanyike tamasha kubwa la Kumaliza Corona Dar es Salaam.
Dunia ijue sisi tumeweza. Kiukweli tumeishi miezi miwili na nusu ya mateso shida na adha kubwa, kumbe viongozi wetu walikuwa wakifanya mchakato na sasa mchakato umefanikiwa. Jumapili hakutakuwa na Corona tena DSM, itabaki historia.
Naipongeza serikali na nampongeza mkuu wa mkoa kwa kufanikisha hilo.hili, jambo si rahisi hata kidogo, ni juhudi kubwa na maarifa yametumika.
Narudia haikuwa kitu RAIS.