Mabibi na mabwana haihitaji elimu ya kiwango cha PhD kutambua sakata la Wabunge wa Viti Maalum limegubikwa na jinai ya wazi.
Haihitaji elimu kama hiyo kutambua kuwa ni nani aliye nyuma ya jinai hii.
Kwamba tume haina mifumo yoyote ya kujiridhisha na uhalali wa mawasiliano yake rasmi na vyama vya siasa? Kwamba kwake kila anayelia bwana bwana atauona ufalme wa mbinguni?
Aaaah Wapi!
Tunataka kudanganyana kwa nguvu sasa.
Kama tume haijaagizwa kufanya haya tunayoyaona na uchaguzi huu, ni vipi tume ya namna hii inaweza hata kufikiriwa kupewa majukumu nyeti ya kuandaa na kusimamia mambo nyeti kama haya yenye kubeba hatima ya taifa letu?
Kwamba mamlaka zinashabikia na hata kuahidi kusimama na matokeo ya jinai? Kwa maneno yake Bi. Halima: "Hii itakuwa ni akili au matope?"
Heko CHADEMA na heko Mbowe kwa maamuzi thabiti yenye kujaa hekima. Uthibitisho ni kuwa hata huku kwenye mitandao washabikia jinai hatimaye wamekituliza!
Kwa hakika Bi Halima na wenzake msingeweza kutendewa haki zaidi ya hii.
Mnayo nafasi ya kuomba kusamehewa au kukata rufaa. Kwamba mnaamua kusuka au kunyoa ndani ya CHADEMA hilo liko mikononi mwenu.
Hali ya upepo tu katika CHADEMA imeonyesha wazi kuwa haki iko wapi. Dunia ya kistaarabu haijawahi kubeza masuala ya "public opinions." Mengine ya kujidanganya unapendwa ni kujilisha upepo tu.
Haiwafikirishi kweli wamama nyie kuwa hamna uungwaji mkono wowote ndani ya CHADEMA isipokuwa akina jiwe, supika, jingaletu na ndugu zao huko mboga mboga? Mtakuwa mmevutishwa sigara gani nyie?
Kumbukeni, kauli ya wengi ni kauli ya Mungu!
Bila kusimama sote kuifahamisha mamlaka na haswa kuanzia kwa juu yake kuwa sisi kama taifa hatufurahishwi na ghiliba ghiliba hizi, basi tutakuwa bado tungali tuna safari ndefu sana.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu:
"Mamlaka zenye kuhalilisha na kusimama na ghushi ghushi kama hizi, hazitufai!"

Halima Mdee, wenzake 18 wavuliwa uanachama Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Halima Mdee na wenzake 18 wamevuliwa uanachama wa chama hicho kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa...
www.mwananchi.co.tz