Tetesi: Bila kitambulisho cha taifa hauruhisiwi kuchukua cheti UDOM

Bunchari

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
489
531
Naandika ujumbe huu nikiwa mwenye masikitiko kutokana na uamuzi wa chuo kikuu dodoma kuhitaji kitambulisho cha taifa,leseni ya udereva au kadi ya mpiga kura ili uchukue cheti.

Binafsi sina hivyo vitu vyote nimefatilia kitambulisho cha taifa wameniambia kupatikana sio leo wala kesho kuna watu wanazaidi ya mwaka awajawai kupata.Sio kila mtu ana reseni ya udereva kwangu mimi sijui hata gari inaendeshwaje.Sijawai kupiga kura sina hizo kadi zao.

Nitoe wito kwa Udom kutumia mbinu nyingine au kuwasiliana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa ili tupate msaada.

Ajira zimekua adimu na ninyi mnaleta kauzibe.
 
Wakati unajiunga nao na wakati upo nao walikutambuaje?
 
Sina Identity card,sina hata moja sio ya kupiga kula,leseni ya udereva wala utaifa nipo mtupu.
 
Kuhusu kitambulisho hilo sahau maana NIDA ni jipu ambalo limekwiva limekosa mtumbuaji tu.

Kuhusu kuchukua cheti, siyo UDOM tu hata UDSM utaratibu uko hivyo ila kama ukiwa huna kitambulisho kimojawapo kati ya hivyo ulivyotaja unaenda kwa mwenyekiti wako wa kijiji/mtaa au mtendaji wa kata unayoishi atakwandikia barua ambayo utaitumia kama mbadala wa kitambulisho cha utaifa.

Sent using my infinix hot 6 pro
 
Duh pole. Ila na wewe kwa miaka ya sasa unakosaje viambatanisho hivyo? Tatizo mnadharau mambo ambayo hamjui impact zake huko mbeleni. Kwa mfano wewe naamini uchaguzi wa 2015 ulikuwa above 18yrs kwa nn hukuwa na kadi ya kura? Bado vitambulisho wa uraia navyo vimetolewa tena bure eti huna. Ngoja mjifunze wakati mwingine iwe tuwe on right truck.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye orodha yao hakuna pasi ya kusafiria?

Kama hana vyote hivo pasi ya kusafiria atakuwa nayo kweli? pole sana na pia tambua ni muhimu kuwa na documents muhimu tayari mda wote, haujui siku wala saa. inasikitisha kwa msomi kama huyo inaleta picha hajielewi
 
Nadhani kupitia wewe wengine na wadogo zake watajifunza.

Ushauri fanya yafuatayo.

Nenda kwa dean mweleze akupe barua na usikute hata copy au kitambulisho cha chuo huna.

Ukishindwa kabisa nenda Nida na bahasha kaonane na mtendaji mkuu utakipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My vote does not count,siwezi kupoteza valuable time kutafuta kadi ya mpiga kura wakat mshindi tayari ameshapangwa.Kila kitu na wakat wake ndugu sidhani kama ilikua sahihi kwangu kuacha masomo yangu kwenda kutafuta vitambulisho.
 
Wewe umesoma chuo kweli? Mbona una mambo ya ajabu.
Watu wanakushauri kuwa na kitambulisho cha kupiga kura ni muhimu na wewe unaandika hivyo. Kachukue cheti sasa.
Si uliona kazi ya hicho kitambulisho ni kupigia kura tuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nida ilinichukua mwez mmoja nilikuwa nimejiandaa nkaenda na hela ya kuhonga kabisa ile nafika nashangaa naitwa jina sikutoa hata hela tu nenda nida wakupe kitambulisho fasta
 
Duh pole. Ila na wewe kwa miaka ya sasa unakosaje viambatanisho hivyo? Tatizo mnadharau mambo ambayo hamjui impact zake huko mbeleni. Kwa mfano wewe naamini uchaguzi wa 2015 ulikuwa above 18yrs kwa nn hukuwa na kadi ya kura? Bado vitambulisho wa uraia navyo vimetolewa tena bure eti huna. Ngoja mjifunze wakati mwingine iwe tuwe on right truck.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vijana wa sasa hivi wanatembea wallet hazina hela,hata vitambulisho pia hawana hata kimoja,zaidi ya condom tu ndo walizonazo
 
Back
Top Bottom