Bila katiba mpya,tunajikaanga wenyewe kwenye mafuta

MAGACHA

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,076
2,000
*DED anagombea ubunge
*DED awe msimamizi wa uchaguzi
*DED ateuliwe na Rais mwenyekiti wa ccm
*DED anaambiwa hakuna kuwa neutral na Uteuzi
*DED ana kadi ya ccm
*DED ni mtumishi wa umma
*DED atangaze mbunge wa upinzani ameshinda- ili afukuzwe kazi na uteuzi
Halafu mnasema tumeshinda kwa kishindo

Vyama vya siasa mjitafakari upya kama huu ndo mfumo wa vyama vingi mnaoutaka

Mwenyekiti wa vyama vya siasa Shibuda atafakari huu mfumo tunaotumia Tanzania kama ni halali au tunajiandalia mlipuko wa moto wa petrol kati ya Tume ya uchaguzi na wananchi,na kama yupo hapo kwa maslahi binafsi aseme na kama hakuna mabadiliko ya katiba acheni kuharibu hela za wananchi kwa uchaguzi hewa

DED korogwe na katibu tawala wamechukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Korogwe vijijini!!!!!!!!!!!!
IMG_20180809_092046.jpg
 
Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,281
2,000
Wale wote tuliowaamini kwenye utafutaji wa Katiba mpya ndio wameshapewa vyeo.

Ile rasimu wameshaitupa.
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,028
2,000
Kamwe usimwamini mtu jiamini mwenyewe na Mungu wako. Sina imani na wanasiasa hata siku moja.

Jambo la kufanya ni moja tu - tuhamasishane kuwa tunafuatilia mambo mbali mbali kwa kusoma yanayoandikwa vinginevyo tunaweza kuuzwa ndani ya nchi yetu. Unaelewaje tabia ya wanasiasa kuficha pesa nje ya nchi? Mwalimu Nyerere ambaye ni muasisi wa taifa hili hakuwahi hata siku moja kuficha fedha nje .. iweje hawa wa siku hizi wanaficha, wanajuana lakini hakuna ufuatiliaji?
 
Katiba mpya ndo dawa ya kila kitu,tusitegemee mtu ndo aje abadilishe vitu ,kuna siku mwehu zaid atakuja kushika hii nchi siku hiyo tutaisha,tunataka katiba ambao itaonyesha strong institutions zinazojitegemea, otherwise tutapata taabu sana
 
Addis Ababas

JF-Expert Member
Aug 5, 2018
353
500
Kinachotakiwa n integrity, siyo Katba... Marekan wana Katiba ya hovyo, ndogo sana kama ka pamphlet, lakn wanakwenda kwa sabab ya integrity ... Ukipewa amri/kazi inayokiuka maadl, miko basi, unajiuzulu kulinda integrity yako. Hata iandikwe katba nzr kiasi gani, bila integrity n 0!
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,044
2,000
*DED anagombea ubunge
*DED awe msimamizi wa uchaguzi
*DED ateuliwe na Rais mwenyekiti wa ccm
*DED anaambiwa hakuna kuwa neutral na Uteuzi
*DED ana kadi ya ccm
*DED ni mtumishi wa umma
*DED atangaze mbunge wa upinzani ameshinda- ili afukuzwe kazi na uteuzi
Halafu mnasema tumeshinda kwa kishindo

Vyama vya siasa mjitafakari upya kama huu ndo mfumo wa vyama vingi mnaoutaka

Mwenyekiti wa vyama vya siasa Shibuda atafakari huu mfumo tunaotumia Tanzania kama ni halali au tunajiandalia mlipuko wa moto wa petrol kati ya Tume ya uchaguzi na wananchi,na kama yupo hapo kwa maslahi binafsi aseme na kama hakuna mabadiliko ya katiba acheni kuharibu hela za wananchi kwa uchaguzi hewa

DED korogwe na katibu tawala wamechukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Korogwe vijijini!!!!!!!!!!!! View attachment 830868
mbona mbowe alimshinda DED huko Hai?
 
ulaya12

JF-Expert Member
Nov 16, 2017
798
1,000
Mwanasiasa siyo mtu wa kumuamini hata akiwa baba yako.halafu kuna yule mzee kwenye kipindi fulani Star tv yeye ana kauli mbiu yake inayosema "siku ya kiyama mtu wa Kwanza kwenda motoni baada ya shetani anayefuata ni mwanasiasa"
 
MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,065
2,000
Hivi vyama vya upinzani ni mamluki tu. hivi wanashiriki vipi uchaguzi ambao dhahiri shahiri wanajua sio wa haki? wangekubaliana kuugomea dunia ijue Tanzania hakuna uchaguzi wangepata support huko duniani. lakini wanashiriki then wanakuja kulalamika.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
30,377
2,000
Nimeamini kuwa Tanzania bila maandamano yasioisha inawezekana katiba ya nini sasa wakati yote tuliokuwa tunayaota yamekuwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom