Bila Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi wapinzani hawatashinda hata jimbo moja 2020

Watu wanataka maendeleo sio katiba mpya.
Magufuli hakuahidi katiba mpya.

Unaweza kukumbuka ni bilioni ngapi zilitumika kuandaa mapendekezo ya katiba mpya ?Vipi kama fedha hizo zingesambaza maji vijijini?
Stop ur nonsense atleast jaribu siku mojamoja kuficha ujinga wako.
 
na wapinzani 2020 watapoteza sana majimbo kwakutoonewa na tume ya uchaguzi, kwanza wameshapoteza mvuto na wameonekana ni wababaishaji tu na matapeli tu.
Waliopoteza mvuto tena wanapigwa risasi 38...!!!!
 
Well said. Bila tume huru ya uchaguzi, uchaguzi hautakuwa na maana make ccm wataenda kwenye uchaguzi na matokeo mfukoni.

Hii tume iende ikasimamie tu chaguzi za ccm make nao wana chaguzi zao, haina kabisa sifa ya kusimamia uchaguzi mkuu wa taifa, wamejazamo watu wa usalama wa taifa tupu ambao kazi wanaojua ni kuiba kura. Nothing more. Waende nyumbani. Period.
 
Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Kutoshiriki uchaguzi ni dhambi isiyosameheka daima. Ni bora vyama visivyotaka kushiriki vijifute vyenyewe kutoendelea kuwepo katika duru za siasa Tanzania.

Ninakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja; uchaguzi wa 2020 chini ya utaratibu uliopo sasa maana yake ni kwamba Magufuli anapata kura asili mia tisini na tisa; na Bungeni hapatakuwemo na mbunge tokea chama chochote cha upinzani.

Wakati huu husikii sauti zozote toka upinzani kuhusu jambo hili. Nasi tuliopo nje inabidi tunyamaze kwa kutojua yanayoendelea huko ndani ya vyama.
Tutaimba sana mapambio ya CCM na Mwenyekiti wake baada ya 2020. "CCM itatawala milele"!
 
Nadhani nia yako ni kuwaongezea muda tena hawa walioko. Katiba mpya sio kitu cha siku 1. Upinzani wasiposhiriki ni kuwapa ushindi mezani hao ccm. Acha waharibiwe uchaguzi wao kwa kuibiwa kura au kutangazwa ndivyo sivyo ila hata huyo atakayeingizwa kinyume na matakwa ya wananchi atajua HAPENDWI.
Tuatshiriki chaguzi kwa kila nafasi inayopatikana huku tukipigania tume na katiba mpya.kwa sababu hujui vitapatikana lini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna ujualo, hii katiba tuliyonayo 80% ni ya 77, ukiacha marekebisho machache yaliyofanyika. Katiba mpya itafanya taasisi za kimamlaka zitekeleze wajibu wake kwa wananchi na mujibu wa sheria na sio kwa rais.
Taasisi ipi inayotekeleza majukumu yake nje ya mujibu wa Sheria ?Inapotokea hivyo sheria inataka utengeneze katiba mpya?kwa fikra zako kila taasisi ikikiuka sheria tutaunda katiba mpya!!Huko ufipa mnasomea zero ya mwenyekiti?
 
Wewe nawe uwe unatumia akili , million hamsini alizoahidi kila kijiji vipi zenyewe amepeleka .Hapa watu wanazungumzia mustakabali wa nchi sio level yako .
Mustakabali wa nchi ni maendeleo ya watu haswa wanyonge.Hatujakosa maendeleo kwa sababu ya katiba mbovu bali kwa kushindwa kufanya kazi na kuendekeza ubadhirifu huku tukijilaza kwenye makucha ya wanyonyaji.
 
Mpaka mtakapoacha unafiki na ukasuku.
Anzeni kubadili katiba ya chama chenu iliyoruhusu mwenyekiti wa kudumu
Hahahaha sasa aliyekuambia mimi chadema nani ili tuweze kuendelea nchi hii uchama ungekaa pembeni maana unatupofusha sana.
 
Taasisi ipi inayotekeleza majukumu yake nje ya mujibu wa Sheria ?Inapotokea hivyo sheria inataka utengeneze katiba mpya?kwa fikra zako kila taasisi ikikiuka sheria tutaunda katiba mpya!!Huko ufipa mnasomea zero ya mwenyekiti?

Makosa mengi ya hizo taasisi yanachangiwa na katiba yenye mapungufu mengi.
 
Mustakabali wa nchi ni maendeleo ya watu haswa wanyonge.Hatujakosa maendeleo kwa sababu ya katiba mbovu bali kwa kushindwa kufanya kazi na kuendekeza ubadhirifu huku tukijilaza kwenye makucha ya wanyonyaji.

Kwahiyo jiwe ndio ameenda kujilaza kwenye makucha ya mzalendo rosti tamu?
 
Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijaelewa unataka waidai CCM iwape Katiba Mpya ambayo itasaidia kuiondoa CCM madarakani? Huu siyo upinzani basi...
 
Mustakabali wa nchi ni maendeleo ya watu haswa wanyonge.Hatujakosa maendeleo kwa sababu ya katiba mbovu bali kwa kushindwa kufanya kazi na kuendekeza ubadhirifu huku tukijilaza kwenye makucha ya wanyonyaji.

Tofauti sana na 'zealots' wengi, unapoamua unatoa mambo mazito. Leo naona umeamua!

Ni vigumu sana kubishia mawazo uliyoyaandika katika mstari huo hapo juu.

Lakini unashindwa au unakataa kwa maksudi kuona umuhimu na nafasi ya katiba katika kulinda haki, ikiwemo haki ya wananchi kuwachagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru, na bila ya bugdha toka kwa mtu au taasisi yoyote ile, ikiwemo polisi, tume ya uchaguzi, rais, n.k.

Nimeona niweke haya kwenye mchango wako leo baada ya kuona mchango wako makin leoi.
 
Pamoja na kuwa sio mfuasi wa chama chochote lakini nimekuwa sifurahishwi na namna Uchaguzi unavyoendeshwa katika nchi hii Chini ya Katiba iliyopo na Tume ya Uchaguzi iliyopo.

Kama Vyama vya Upinzani vitashindwa Kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni bora visishiriki Uchaguzi huo kwani kitakachofanyika ili ionekane CCM inakubalika hamtaamini Macho na Masikio yenu na Wanachama wafuasi na wapenda mabadiliko mtawakatisha tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mpima Mstaafu, kwanza asante kwa hoja hii, japo haya usemayo kuna mengine ni kweli na mengine sii kweli.

Tuanze na la kweli ni Uchaguzi wa 2020, CCM itashinda kwa kishindo na wapinzani watapigwa chini jumla, hivyo Tanzania kurudi kuwa nchi ya chama kimoja kwa Bunge la chama kimoja.

Tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi nchini, tumeshudia wapinzani wakiingia Bungeni na madiwani kwa Katiba hii hii na Tume hii hii ya Uchaguzi, hivyo hizi hoja zako za NEC na Katiba weka pembeni.

Sababu za CCM kushinda kwa kishindo ni kazi nzuri ya rais Dr. John Pombe Magufuli ambaye ameufanya CCM ikubalike sana kama nilivyoeleza humu.

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums

Kufuatia kazi hii nzuri sana ya rais Magufuli kutuletea maendekeo makubwa Kama Flyover, Ndege, SGR, na sasa anajenga Tanzania ya viwanda na tunakwenda kuwa nchi ya uchumi wa kati, hivyo nikauliza kama bado tunahitaji kufanya uchaguzi mwaka 2020 au tumuache tuu rais Magufuli aendelee na kwenye ubunge na udiwani tuiachie tuu CCM ipite bila kupingwa?.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

CCM itashinda kwa kishindo kufuatia kukubalika sana na tunashuhudia jinsi wapinzani wanavyo vikimbia vyama vyao na kujiunga na CCM
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

P
 
Ubabe kazini

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na wapinzani 2020 watapoteza sana majimbo kwakutoonewa na tume ya uchaguzi, kwanza wameshapoteza mvuto na wameonekana ni wababaishaji tu na matapeli tu.
kama uharo wako huu ni kweli sasa si mutengeneze tume huru ya uchaguzi
 
Nafikiri hakuna haja ya kupoteza pesa za walipa kodi kwa kutafuta katiba mpya ,wanachi tunataka maendeleo,ikiwemo miundombinu ya usafirishaji na uzalishwaji wa nishati rahisi zitakazoweza kukuza uchumi wetu kwa haraka na kumletea mwanachi nafuu ya maisha , na kama serikali inafanya yote haya ,katiba mpya ya nini?
sasa kwanni munafanya uchaguzi kupoteza pesa bure tu zawananchi si muvifute tu vyama vya upinzani tuwe na ccm peke yake
 
Back
Top Bottom