Bila kadi hupandi mabasi ya mwendokasi kuanzia August 1

Mkiambiwa mnakurupuka mnatupeleka senturo kuhojiwa. Sasa mimi nimetoka zangu Tarime leo, nimefika Dar naondoka keshokutwa, ukanikatishe kadi ya 5000 huko Tarime naenda kuifanyia nini?
unatakiwa uiuze au uiharibu baada ya muda kuisha alafu kitu cha elefu mbili kinakupigizaje kelele, tumia mpaka kiishe then tupa au choma
 
Hata huko tulikogeza matumizi ya kadi kwenye usafiri kuna cash pia. Maana si kila raia anatumia usafiri wa umma daily; wapo wageni wanoingia Dar kwa siku chache na kuondoka na pengine hajui atarudi tena lini, wapo ambao wana usafiri wao binfasi lakini hupata dharura akatumia hayo mabasi may be once in a year kwa mifano hiyo ni upuuzi kulazimisha kila abiria awe na kadi.

Pia matumizi ya credit card yanahitaji mtu mwenye kipato kinachoeleweka endelevu lakini wengi wa abiria wanaotumia usafiri wa umma hapa Dar wana vipato vya kuungaunga. UDART tangu waanze wanaonyesha ni watu ambao ni wavivu kufanya utafiti kabla ya kufikia maamuzi.

Kubwa zaidi, huu usafiri bado unawatoa ushamba wengi wakazi wa Dar na wageni wa Dar sasa kuwaongezea hiyo kitu ni kuwavuruga zaidi. Hapo nahisi kuna mtu (mzabuni) wa hizo kadi analazimisha kazi

Na hapa ndipo Watanzania au niseme Waafrika tunapokosea sana, huu usafiri ni kwa ajili yetu sisi wana Dar na siyo kwa ajili ya wageni, wao wageni wakija ndiyo wajipange kuendana na maisha yetu na siyo sisi tujipange kuendana na matakwa ya mgeni hilo ni kosa kubwa sana!
Hivyo uDART wanapaswa waangalie jinsi ya kuboresha huduma kwetu sisi wana Dar na siyo kufikiria mgeni atafanyaje, fikra kama hizi ndiyo zilizotufikisha hapa!
 
Mkiambiwa mnakurupuka mnatupeleka senturo kuhojiwa. Sasa mimi nimetoka zangu Tarime leo, nimefika Dar naondoka keshokutwa, ukanikatishe kadi ya 5000 huko Tarime naenda kuifanyia nini?

Lakini huu Mradi ni kwa ajili ya wana Dar na siyo wana Tarime hivyo wana Dar hawawezi kubadilisha maisha yao ili yaendane na wewe mwana Tarime, hata huko Tarime pia kuna taratibu za watu wa huko ambazo wamejiwekea!"

Hapa lengo ni kupunguza adha anayoipata mtumiaji wa DART wa kila siku ambaye ndiye huu mraidi umejengwa kwa ajili yake na siyo mtu wa Tarime au sijui Tunduru, wewe wa Tarime sasa itabidi ujipange lkn hatuwezi kufanya maisha yetu yawe magumu kwa ajili ya mtu anayekuja nakuondoka kesho!!
 
USAFIRI MWENDOKASI: Uongozi wa UDART leo umetangaza kuwa kuanzia Agosti Mosi 2016, hakuna mtu mzima atakayepanda mabasi hayo bila kutumia Kadi, mfumo wa tiketi utatumiwa na wanafunzi pekee.

=======

Kampuni ya Usafirishaji ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDART) inatarajia kusitisha matumizi ya tiketi za karatasi ifikapo Julai 30 mwaka huu.

Uamuzi huo unalenga kudhibiti foleni za kununua tiketi za karatasi kutokana na idadi kubwa ya abiria; kati ya 150,000 na 200,000 wanaotumia usafiri wa mabasi hayo kwa siku. “Kwa siku abiria wapatao laki moja na nusu hadi laki mbili wanatumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka kila siku, sasa kumekuwa na foleni vituoni na pia tunakusanya magunia na magunia ya karatasi na kuna maeneo mengine uchafu unakuwa mwingi,” Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa aliwaambia waandishi wa habari jana.

Hata hivyo, kusitishwa huko kwa tiketi za karatasi, kunalenga watu wazima pekee wanaolipa Sh 650. Wanafunzi wanaolipa Sh 200, wataendelea kutumia tiketi za karatasi ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye vituo vya mabasi.

Mgwasa alisema licha ya hatua hiyo kulenga kupunguza foleni kwenye vituo, pia itaondoa uchafu unaotokana na tiketi za karatasi.

Wakati huo huo, alisema kutokana na mpango huo wa kusitisha tiketi, kuanzia leo kampuni imepunguza gharama ya ununuzi kutoka Sh 5,000 kwa tiketi za hadi Sh 2,000, Sh 500 itakuwa gharama ya kadi na Sh 1,500 ni nauli. “Kuanzia kesho (leo) kadi zitauzwa kwa gharama ya Sh 2,000 kwenye vituo vyote vya mabasi ya mwendokasi,” alisema.

Mgwasa alisema tangu kuanza kuuzwa kwa kadi hizo kwa gharama ya Sh 5,000 tayari kadi 55,000 zimeshanunuliwa na kubakia kadi 150,000 ambazo ziko kwenye promosheni ya kuuza kadi kwa Sh 5000.

Alisema baada ya kadi hizo kuisha, abiria atalazimika kununua kadi hiyo kwa thamani ya Sh 5,000 bila kuwekewa fedha za nauli kama ilivyokuwa awali.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Maxcom Afrika (MaxMalipo), Deogratius Lazari alisema wamejipanga kuhakikisha tiketi za kadi zinapatikana kwenye vituo vya mabasi. Aliwataka wateja kuhakikisha wanaweka salio katika vituo hivyo. “ Kampuni za simu ziko katika hatua ya mwisho za kukamilisha mifumo yao ili abiria aweze kuongeza salio kupitia mitandao ya simu ila kwa sasa abiria wanatakiwa kutumia vituo vyetu vya mabasi
Akimaliza 10, tumuongeze mingine 10.-Hapo umenena
 
CAG alitoa ushauri kuhusu matumizi ya Card. watu walishangilia sana na kuanza kuilaumu serikali ya JPM. leo hii UDART wanahimiza Card tayari watu wameanza kulia lia humu wanalalamika. hawa ndo watanzania hata ukiogelea kwenye bwawa watakwambia unawatimulia vumbi
 
Kwa hesabu ipi ?
Kama abiria kwa siku ni laki mbili wanapanda asubuhi na kurudi jioni
200,000 * 1300=260,000,000
wastani kwa siku wapata kati 200m. mpaka 240m. kuna wanafunzi pia.

Basi moja linapakia abiri wangapi kwa route moja?
Basi moja kwa siku linapiga route ngapi?
Mabasi yapo Mangapi?

Basi 1 x idadi ya safari kwa siku x Idadi ya mabasi = ????
 
Aisee kuna wakurupukaji wengi sana humu nchini..
Kuna waziri mmoja eti anawamindi JICA kisa wanafanyia mkutano hotelini.. Tena kwa pesa yao... Kuna siku tutachaguliwa cchupi za kuvaa.. Wote tutatakiwa kuvaa VIPI
 
Huyo Mkurugenzi ni mzembe anatakiwa atumbuliwe tu. Abiria wa kivukoni
wanalalamika usafiri kutoka fire kwenda kivukuni ni shida yeye mpaka sasa
amekosa ubunifu kidogo tu wa kutatua hilo tatizo?
Wahuni tuu hawa
 
USAFIRI MWENDOKASI: Uongozi wa UDART leo umetangaza kuwa kuanzia Agosti Mosi 2016, hakuna mtu mzima atakayepanda mabasi hayo bila kutumia Kadi, mfumo wa tiketi utatumiwa na wanafunzi pekee.

=======

Kampuni ya Usafirishaji ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDART) inatarajia kusitisha matumizi ya tiketi za karatasi ifikapo Julai 30 mwaka huu.

Uamuzi huo unalenga kudhibiti foleni za kununua tiketi za karatasi kutokana na idadi kubwa ya abiria; kati ya 150,000 na 200,000 wanaotumia usafiri wa mabasi hayo kwa siku. “Kwa siku abiria wapatao laki moja na nusu hadi laki mbili wanatumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka kila siku, sasa kumekuwa na foleni vituoni na pia tunakusanya magunia na magunia ya karatasi na kuna maeneo mengine uchafu unakuwa mwingi,” Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa aliwaambia waandishi wa habari jana.

Hata hivyo, kusitishwa huko kwa tiketi za karatasi, kunalenga watu wazima pekee wanaolipa Sh 650. Wanafunzi wanaolipa Sh 200, wataendelea kutumia tiketi za karatasi ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye vituo vya mabasi.

Mgwasa alisema licha ya hatua hiyo kulenga kupunguza foleni kwenye vituo, pia itaondoa uchafu unaotokana na tiketi za karatasi.

Wakati huo huo, alisema kutokana na mpango huo wa kusitisha tiketi, kuanzia leo kampuni imepunguza gharama ya ununuzi kutoka Sh 5,000 kwa tiketi za hadi Sh 2,000, Sh 500 itakuwa gharama ya kadi na Sh 1,500 ni nauli. “Kuanzia kesho (leo) kadi zitauzwa kwa gharama ya Sh 2,000 kwenye vituo vyote vya mabasi ya mwendokasi,” alisema.

Mgwasa alisema tangu kuanza kuuzwa kwa kadi hizo kwa gharama ya Sh 5,000 tayari kadi 55,000 zimeshanunuliwa na kubakia kadi 150,000 ambazo ziko kwenye promosheni ya kuuza kadi kwa Sh 5000.

Alisema baada ya kadi hizo kuisha, abiria atalazimika kununua kadi hiyo kwa thamani ya Sh 5,000 bila kuwekewa fedha za nauli kama ilivyokuwa awali.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Maxcom Afrika (MaxMalipo), Deogratius Lazari alisema wamejipanga kuhakikisha tiketi za kadi zinapatikana kwenye vituo vya mabasi. Aliwataka wateja kuhakikisha wanaweka salio katika vituo hivyo. “ Kampuni za simu ziko katika hatua ya mwisho za kukamilisha mifumo yao ili abiria aweze kuongeza salio kupitia mitandao ya simu ila kwa sasa abiria wanatakiwa kutumia vituo vyetu vya mabasi
Niwaombe tu wakimaliza kadi zote wasitengeze nyingine bali watangaze kutumika kwa njia zote mbili
 
Basi moja linapakia abiri wangapi kwa route moja?
Basi moja kwa siku linapiga route ngapi?
Mabasi yapo Mangapi?

Basi 1 x idadi ya safari kwa siku x Idadi ya mabasi = ????
Hesabu ya abiria kwa basi moja huwezi ipata kiurahisi tiketi zilizouzwa kwa siku ni rahisi kujua kwa siku wanapata
au kusafirisha abiria kiasi gani.
 
UDA-RT wamesema wanasafirisha abiria kati ya 150,000 mpaka 200,000 kwa siku
na wameshauza CARD 55,000 zimebaki 150,000.
watu hata post hawasomi, wanachojua ni kupinga tuu!! hapo wangesema wanapata abiria 1000 ndio wangefurah, ungeona vipost humu" mabasi ya mwendokasi yasusiwa, mwendokasi yabuma" na sherehe wangefanya!!
 
KAULI YA MKURG WA UDART HIVI KARIBUNI KUANZIA TAR 01 AUG WANANCHI WAKUBWA WATATUMIA KADI TU SASA LEO HII SIKU YA PILI WANANCHI WAMEENDELEANKUTUMIA MARATASI

IKUMBUKWE HAWA JAMAA WALITANGAZA HILI BAADAYA KUSHTUKA KUNA WIZI MKUBWA WA TKT NA WATU KUENDELEA KUTUMIA TKT ZILIZOTUMIKA

MNAMAONI GANI KUACHANA NA HAYO MAKARATASI YANAYOWAPA HASARA??
 
Back
Top Bottom