Bila itikadi Imara CCM haing'oki

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kwanini tunataka kuiondosha CCM ? Hili ni swali ambalo napenda kujiuliza na pengine wananchi Wengine makini wangependa kueleweshwa hadi kuelewa pasipo kuweka propaganda zisizo na maana, Ili watu makini waweze kujitolea maisha yao kwa ajili ya jambo fulani ambalo lenye maslahi kwa taifa lazima walielewe kwanza. Kwahiyo wapinzani wanapaswa kuwaeleza wananchi kwanini tunapaswa kuiondoa CCM kwa lugha nyepesi na inayoeleweka.

Na watu wakielewa inakuwa rahisi kwao kujitolea kwenye movement yeyote ambayo wapinzani wataitisha. Wananchi hawaogopi polisi hawaendi kwenye maandamano yanayoitishwa na wapinzani kwasababu hawajapewa sababu za kuridhisha kuingia barabarani au kujiunga na movement ambazo wapinzani wanaitisha. Siamini kama wananchi wa Tanzania ni waoga hawajapewa sababu za kuridhisha za wao kuhatarisha maisha yao . Maisha ya binadamu yanathamani mno na hakuna mtu atayejitolea maisha yake kwa movement isiyoeleweka au ya watu wasiokuwa na maono.

Vyama vingi tulivyonavyo haviungozwi na ideology; Vyama vilivyo vingi ni vikundi vya watu wanaotafuta madaraka tu hiko ndio kitu kilichowaunganisha na sio ideology. Ni muunganiko wa watu wanaotafuta ubunge, udiwani na wengine pengine uraisi ili wafanye biashara, ni usaka tonge tu. Ni struggle ya madaraka isiyoongozwa na ideology. Na ndio maana vyama hivi huongozwa na matukio. Litokee tukio fulani waoongee na kupiga kelele kisha likitokea tukio jingine wanabadilika tena. Kuna shida kubwa mno ya kiitikadi katika vyama hivi. Waelewe wapinzani hakuna kitu kinachosukuma watu kuleta mabadiliko kama ideology. Kama watu hawana conviction katika idea fulani na hiyo idea ndio inayo move watu kutafuta madaraka kamwe ni vigumu sana kupata POWER. Kwasababu IDEA ndio inayounganisha watu kinyume cha hapo utakuwa na muunganiko wa watu ambao ni opportunistic na self seekers kwenye chama. Na watu wa namna hii ambao hawana mizizi katika itikadi fulani ni rahisi kununulika. Wanasiasa wengi na wafanyabiashara tu na wanataka ku generate pesa. Wananchi wengi wanaachwa pembeni.

So wananchi sio wajinga au waoga bali hawajashawishika kujitolea maisha yao au hawajapewa sababu za kimsingi za wao kutoka kwenye nyumba zao kuandamana. Na kama wangekuwa na conviction ya kutosha wasingekaa nyumbani wanapoibiwa kura. Wanachoona wananchi ni watu wenye malengo yale yale tu. Kwahiyo wapinzani wanatakiwa kubadilisha mwelekeo wa fikra zao. Kama chama hakina itikadi na kinaongozwa na mikate viongozi wenu watakamatwa na kutiwa ndani hata mamia kwa mamia na hakuna kitu kitakachotokea. Na itakuwa vigumu sana kuiondoa CCM madarakani bili itikadi imara. N a watu ndani ya vyama hivi wataendelea kununuliwa hadi hapo wanachama wao watakapojengwa kiitikadi na kuwa na mwelekeo wa wanachohitaji. Wanaweza kukosoa chama kilicho madarakani lakini sio kukosoa kila wakati na kwa kila kitu.

Lazima uwepo wakati wa kuelezea maono na itikadi ya chama katika nyanja mbali mbali. Binafsi kwa mwelekeo huu sioni kama CCM itatoka hivi karibuni unless wapinzani wabadilike. Kukandamizwa na kuonewa kunatokana na misingi ambayo wameilea. CCM wanajua wanaweza kufanya chochote na hakuna upinzani utakachofanya kwakuwa misingi ya vyama hivyo sio ideology ni mkate na hawana conviction ya kutosha ya wanachohitaji. Wanajua watapiga kelele tu na hawato ACT na wakitishiwa polisi watauvyata na kwakuwa ideology ya vyama vyao haijamea kwa wananchi hatawakikamata viongozi wao hakuna mtu atakayedhubutu kuandamana.

Nasema hivi wananchi hawajashawishiwa vya kutosha. Wakishawishiwa vya kutosha na vyama vya upinzani vikikubalika vya kutosha, tume iwe huru au isiwe huru CCM itatoka tu madarakani, shida ni kwamba wananchi hawajashawishiwa vya kutosha na wapinzani wanatakiwa waelekeze nguvu huko. Kama wapinzani wanakubalika vya kutosha Tume ya uchaguzi sio kikwazo. Shida ni awareness ya wananchi. Kama Tume ikiwa overwelmed na kura za wapinzani kwenye sanduku la kura watapindua vipi matokeo? Kuna shida ya kukubalika kikamilifu wapinzani wanakubalika robo robo huwezi pindua the will of majority ukifanya hivyo utamuongoza nani? Na waliojaribu kufanya hivyo waliona na moto. nataka wapinzani wajue hilo focus yao ni lazima iwe ku win mioyo ya wananchi sio kupambana na CCM. Na Tume ya uchaguzi sio kikwazo kama unakubalika vya kutosha.

Narudia tena hakuna awezaye kiongozi yeyote yule kuzuia the Will of the people. Shida ya upinzani haujakubalika vya kutosha tatizo wala sio tume. Pamoja na mambo yote wachukue muda kujijenga sio Kushinda MARIA SPACES. Yanayojadiliwa kule ni kutwanga maji kwenye kinu. You can not stop a popular leader to get power. Uongozi ni watu na yule mwenye watu wengi Automatic ataongoza tu. Kwahiyo tunahitaji kuaminiwa na wananchi wengi zaidi na kuonyesha kwamba sisi ni watu responsible na tuko tayari kuongoza nchi. Na Tujitaidi kutayarisha watu wetu kuwa hivyo kuchukua madaraka kwa kuwajengea nidhamu na uwezo wa kufikiri. Kuna aina za Siasa na aina za watu ambao wako upinzani ambao hausaidii sana vyama vya upinzani kufikia malengo yake na itachukua miaka kama hatutabadilika.

Sio rahisi kuondoa chama kama CCM madarakani kama upinzani hauna watu wenye maono na wenye uwezo mkubwa wa kupanga mbinu za maana na wenye ushawishi wa kutosha kwa watu muhimu katika taifa hili kama viongozi wa dini na watu wengine. Uwezo wa kushawishi kwamba wao ni chama bora ambacho kinaweza kuleta mabadiliko katika nchi na kina watu wenye staha na nidhamu ya kutosha . Lazima wauze idea yao kwa watu. Ideology yao lazima ifike na imee ndani kwa watu na waielewe. Watu watakapopata picture wakiingia madarakani wataenda kufanya nini itakuwa rahisi kwao kufanya maamuzi. Wasipofanya hivyo watadharauliwa na wataonekana ni watu wasio na agenda. Wataonekana wahuni na wapiga kelele.

Mahitaji ya mabadiliko lazima yaonekane wazi kwa watu. Kwahiyo upinzani lazima uje na plan ya mabadiliko kwenye Elimu, kwenye uchumi, kwenye siasa na kwenye jamii na waelezee hayo in a great details, waonyeshe wanajua matatizo ya nchi hii na utatuzi wa changamoto hizo. Tunahitaji kujua the way forward. Tunashindwa kufanya haya sababu tatizo letu kubwa ni mkate. Na mkate huu ndio unaoligawa Taifa. Na tunakosa vision ya kwenda mbele.


Tuache kulia lia tume sio kikwazo. Tafuta wanachama, sambaza itikadi ya chama badilisha mindset sio kulalamika na na kuongozwa na matukio.
 
Siku moja nilisema kuwa CDM si chama cha wananchi bali watu wa fursa nikaonekana mchawi. Kiukweli bila kuwashawishi wananchi juu ya faida watazopata wakiiondoa CCM itakuwa ni ngumu kuwango'a. Ukiwaaminisha walima mahindi, korosho kahawa nk kuwa wakiitoa ccm watapata bei nzuri nk, CCM haitachukua round kuanguka.
 
Wanaendesha vita dhidi ya CHADEMA ili wabaki madarakani na watoto wa Kitanzania waendelee kusoma katika mazingira haya. Huu ndio ugaidi. Ndio maana tunadai Katiba Mpya yenye misingi ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
Unaamini kwamba mambo ambayo mnatumaini mtayapata baada ya kuandika katiba mpya? Mnaamini kwamba Tanzania mpya itakuja mara baada ya katiba mpya?

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Okay. Mimi binafsi sidhani. Nina sababu. Natafuta muda nielezee kuhusu hili. Siamini kama Afrika iko nyuma kimaendelee na katika masuala ya utawala bora sababu katiba zao ni mbovu.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Sawa na mimi nikipata muda nitakuletea umuhimu wa katiba mpya kiujumla
 
Back
Top Bottom