Bila HESLB yenyewe kutimiza wajibu wake, hakuna mikopo kwa wanafunzi

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Mar 14, 2013
165
39
Salaam ndugu zangu katika imani,nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya na uzima aliotupa sote hata tunaweza leo kuandika na kusoma maandiko mbalimbali.
Niipongeze pia serikali kwa kuendelea kulinda wananchi na mali zao kila siku,ikumbukwe hilo ndilo jukumu msingi la serikali yoyote duniani.

Nahitaji kusema neno juu ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu yaani HESLB ,nimeamua kuandika nikiamini ndicho chombo pekee kinachoweza kumsaidia mtanzania kupata elimu anayoitaka.
HESLB ni chombo kilichoundwa na sheria ya bunge ambapo jukumu lake ni kuhakikisha watanzania wanapata mikopo ili kuweza kumudu gharama za masomo na maisha wawapo vyuoni.

Kwa miaka mingi sasa kumekuwapo malalamiko ya wanafunzi wengi kutokupata fursa ya kukopeshwa ili kukamilisha ndoto zao,lakini kuna sehemu chombo hiki hakijafanya ili kunusulu tatizo la ukosefu wa fedha kwa vijana.

Naomba tujiulize ni kwa kiasi gani HESLB mnahakikisha wanufaika wa mikopo hii wanarejesha mikopo yao kwa wakati?

Kwa Jiji la Dodoma tu ambalo binafsi nimetembelea shule 54 za jiji ni shule za serikali pekee ndizo wanufaika wa mikopo wanalipa mikopo yao,zaidi ya shule binafsi 20 wanufaika wa mikopo hawalipi kiasi chochote cha mikopo ili hali wanakipato kinachoweza kuwawezesha kuanza kulipa mikopo yao.

Naomba wenye mamlaka mshughulike na mhakikishe wanufaika wote wanalipa mikopo yao kwa wakati ili kuwezesha watanzania wengine kunufaika na huduma hii iliyoanzishwa kwa nia njema ya kuwasaidia watanzania kumudu gharama za masomo.

Watendaji wa HESLB acheni kungoja majina kutoka sekta mbalimbali bali tokeni na mkakague taasisi zote zinazotoa ajira ili kuhakikisha wanufaika wanaanza kurejesha mikopo yao.
Binafsi nimegundua wanufaika wengi wanakwepa kulipa hivyo wanakwamisha maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla.

Nawaomba viongozi watendaji anzeni kupita shule binafsi na huko ndiko walipojificha wanufaika wa mikopo,pitieni shule zote hasa za Dodoma naamini mtapata idadi kubwa ya wanaokwepa kulipa mikopo yao.

Tabia ya kukaa ofisini na kungoja majina yaletwe na taasisi husika nafikiri sio uzalendo bali fanyeni kazi yenu kama wafanyavyo uhamiaji,vile vile niwaombe mnapogundua kuna taasisi imeficha majina ya wanufaika wa mikopo fateni sheria pasi aibu wala kupepesa macho.Nasema hili kwa sababu natambua kuna taasisi zinawazidi nguvu kwa kuwafunga midomo msiweze kushughulikia mambo haya ipasavyo.

Lai yangu kwa watanzania ni kuhamasisha wanufaika wa mikopo kulipa mikopo kwa wakati ili kuwezesha watanzania wengine kunufaika.

HESLB TIMIZA WAJIBU WAKO
 
Vijana wapo toka 2015 mtaani tu hakuna ajira Serikali inakopesha wanafunzi mabilioni ya fedha alafu haiwezi kuuajiri popote sasa hao heslb watawapataje??
Au unataka na hawa wauza mishkaki wenye degree nao wakalipe heslb?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom