Bila Hayati Magufuli; Wabunge, madiwani na wenyeviti wa vitongoji leo wasingekuwa kwenye hizo nafasi

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,565
2,000
Hayati Magufuli ndiye aliyesababisha wabunge wengi kurudi bungeni kwa ubabe wake alioufanya.

Madiwani nao wamebebwa kushika hizo nyadhifa kwa hisani ya ubabe wa hayati Magufuli.

Wenyeviti wa vitongoji ndiyo kabisaa hata uchaguzi hatukufanya walipitishwa bila kupingwa, yote hiyo ni hisani ya ubabe wa hayati Magufuli.

Kwa mifano michache tu wabunge wafuatao kamwe wasingerudi Bungeni kama ubabe wa hayati Magufuli isingetumika.

1. Ndugai
2. Lukuvi
3. Mkuchika
4. Mbunge wa Kilwa ( kule kwa bwana Bwege)
5. Tulia Ackson
7. Mbunge wa Ikungi( kwa Lissu)
8. Mbunge wa Hai
9. Mrisho Gambo
10. Mbunge wa Mikumi
11. Mbunge wa Iringa mjini
12. Mbunge wa Mbarali
13. Mbunge wa Kigoma mjini ( kwa Zitto Kabwe)
14. Salma Kikwete
15. Wabunge Pemba yote
16. Majimbo 10 Unguja
17. Mwita Waitara
18. Askofu Gwajima
19. Mkoa wa Lindi wote except ( Mtama na Ruangwa)
20. Mkoa wa Mtwara wote (except majimbo matatu tu).
21. Mbunge Bukoba mjini
22. Abood (Morogoro mjini)

Hiyo ni mifano michache, lakini 40% ya wabunge waliopo Bungeni wamebebwa kwa hisani ya ubabe wa hayati Magufuli.

Sasa maadamu Mama Sami S Hassan ataruhusu watu wachague kwa haki, tuombe uzima 2025 muone kitakacho watokea CCM.
 

kamarah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
847
1,000
Ongeza Kawe, pemba yote na kadhaa ya unguja, Muheza, mikumi, Mtama kwa Nape, Ifakara, Kilombero, Arusha na Kilimanjaro yote, Dar yote, Mbeya yote, Dom wangegawana pasu, Mwanza pasu, Geita pasu, Pwani pasu, Moro yote, Lindi yote, Mtwara yote, Ruvuma pasu.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,500
2,000
Ongeza Kawe, pemba yote na kadhaa ya unguja, Muheza, mikumi, Mtama kwa Nape, Ifakara, Kilombero, Arusha na Kilimanjaro yote, Dar yote, Mbeya yote, Dom wangegawana pasu, Mwanza pasu, Geita pasu, Pwani pasu, Moro pasu.
Hata Katelefoni majaliea ashukuru Mungu alitumia takukuru kumzuia Mgombea asirejeshe fomu apite bila kupingwa. Ni jahili yule asijifanye anaenda kufunga ramadhani.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,519
2,000
Ongeza Kawe, pemba yote na kadhaa ya unguja, Muheza, mikumi, Mtama kwa Nape, Ifakara, Kilombero, Arusha na Kilimanjaro yote, Dar yote, Mbeya yote, Dom wangegawana pasu, Mwanza pasu, Geita pasu, Pwani pasu, Moro pasu.
Wapuuzi wale wakubwa na MUNGU akasema liwe fundisho
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,694
2,000
Hilo sasa ndilo lilimkasirisha MUNGU na akatoa adhabu kali kwa mwendazake. Unaiba kura zote kibwege halafu unasema niombeeni kwa MUNGU? Mungu gani wa Magufuli alitaka tumuombee?

Baada ya kuiba kura kwanza ameteseka kwenye mashine za oxygen na amekaa na Utawala wa wizi kwa siku 120. Ogopa sala za watu wengi waliodhuumiwa.
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,929
2,000
Hayati Magufuli ndiye aliyesababisha wabunge wengi kurudi bungeni kwa ubabe wake alioufanya.

Madiwani nao wamebebwa kushika hizo nyadhifa kwa hisani ya ubabe wa hayati Magufuli....
Mtoe Mbunge wa Iringa Mjini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom