MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
natambua kuwepo na magomvi mbalimbali kwa sababu ya dini tofauti na hata wafuasi wa dini moja kupambana. lakini kusingekuwapo na dini kabisa, haka ka amani na ka haki kadogo na ustawi na maendeleo ya jamii visingekuwepo kabisa. kwani dini zimeleta yafuatayo:
1. zinafundisha upendo, umoja, amani na haki
2. zinajenga taasisi kama shule, hospitali na viwanja vya michezo. na hapa wengi tumefaidika sana.
3. zimesaidia kutatua migogoro mbalimbali
4. zinafundisha maadili mema na kukemea maovu.
Naamini bila dini tungeuana sana na tungeishi ktk mazingira hatari kuliko ilivyo sasa. asante Mungu kwa dini. swali? Dini ipi ya kweli? kila mtu atatetea ya kwake. cha kufanya ishi kadiri ya dhamiri yako na usipuuze nini dini ya mwenzako inasema, bali tafakari na yaliyo mema yachukue. ila jiamini na tenda unachoamini ni haki na chema. yapo mambo ambayo kwa akili na sheria ya asili(natural law)aliyotupa Mungu tunaweza kuyajua juu ya uhalali wake. watu wa dini tofauti tuvumiliane. atakayeshindwa kumvumilia mwenzie na kumjeruhi ndiye atakayemchukiza Muumba. Asanteni