Bila Demokrasi Hakuna Maendeleo!

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Ni ukweli tupu kuwa, watanzania wanahitaji maendeleo. Lakini haiwezekani ikawa kweli kuwa, maendeleo hayo yanaweza yakapatikana pasipo na demokrasi. Na inafahamika waziwazi kuwa, dhana ya maendeleo ni dhana iliyo pana sana, na kimsingi ni dhana ambayo mjadala wake ni bado unaendelea hata sasa. Kwa maana hiyo ni mjadala endelevu!

Hata hivyo, ili kuweza kuyafikia maendeleo hayo, ni dhahiri kuwa ni lazima kwanza tuweze kuendelea kwenye demokrasi. Ikumbukwe kuwa demokrasi ni hali ya kuwa. Hivyo, kwa jinsi hiyo mchakato wa kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi yanapatikana ndani ya Tanzania kwa watanzania wote, basi ni lazima hali yetu ya kuwa na haki na usawa na uhuru binafsi ndani ya jamii, ipate kuwepo: Hali hiyo ni lazima nayo ipate kuwa nzuri, kwa maana ya demokrasi safi nchini.

Hata hivyo, ni kweli kuwa, kupitia demokrasi, nchi yetu itapata kuboreshwa na kujengwa na sisi sote, kwani ni demokrasi ya uwajibikaji na ya uzalendo ndio inataka hivyo: Kupitia demokrasi, kila raia atakuwa uhuru kwa kutoa nje mawazo yake ambayo ni lazima yawe na tija kwa taifa: Kupitia demokrasi, nchi haitaongozwa kwa utashi wa kiongozi pekee, ila ni kwa msingi wa utawala wa sheria (yaani katiba ya nchi). Kwa hiyo ni ngumu kuitenganisha demokrasi na maendeleo. Maendeleo ni tunda la demokrasi; na demokrasi ndio chachu ya ustawi wa maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Na kwa jinsi hiyo tangu uhuru hata sasa, taifa letu chini ya serikali inayoundwa na CCM, ililitambua hilo. Na kwamba ili kwanza tuweze kuendelea, ilitakiwa kwanza tuipate demokrasi ya uhuru. Na hata baada ya kuwa huru, serikali za CCM za awamu zote zimeipa kipaumbele suala zima la demokrasi ili kuweza kulipatia taifa letu maendeleo katika nyanja zote muhimu. Ifahamike kuwa ni CCM inaamini kuwa, demokrasi kwanza kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
 
Tafsiri rahisi ya demokrasia ni watu kuwa uhuru kuji express maishani mwao.

hakuna kipindi ambacho nchi zetu za Africa zilivyokuwa zinapiga maendeleo makubwa ya vitu (miundombinu, nk) kama wakati tupo chini ya mkoloni. lakini bado mwalimu Nyerere na wenzake walipambana kuwaondoa hao "waleta maendeleo". kwa nini? walikuwa wanaitafuta demokrasia (aka uhuru).

awamu ya 5 haiko tofauti na wakati wa mkoloni, imekazania maendeleo ya vitu huku ikiwakandamiza Watanzania katika nyanja zote (civil servants, wakulima, wanafunzi, wanasiasa, wafanyabiashara, wasio na asili ya kanda pendwa hususani wale wa kanda ya kaskazi, nk).

we need our freedom back!!!
 
Hasara ya Udikteta ni kubwa sanaa

Mafao ya wastaafu wanakata

FAO LA KUJITOA wamefyeka..

Hii ni kwa sababu ya Uamuzi wa mtu mmoja
 
... unapotoa hoja consider all possible dimensions. Demokrasia ndio nini? Maendeleo ni nini?

China ina demokrasia? China ina maendeleo? With reference to China, hivyo viwili ni lazima viende pamoja? Jiandae kujibu hoja.
 
Dudus

Demokrasi kama nilivyosema awali kuwa, ni hali ya kuwa! Demokrasi ni utaratibu ambao serikali unautumia kwa kusudi la kuleta usawa mbele ya sheria (watu wote ni sawa ndani ya jamii), uhuru wa watu ndani ya jamii, ushiriki wa watu katika maamuzi ya taifa ama moja kwa moja au kwa kupitia uwakilishi, na ushirikishwaji wa watu katika kazi za serikali kwa manufaa ya watu wote ndani ya taifa.

Kwa hiyo kumbe, demokrasi ni madaraka ya watu ambao yanakabidhiwa kwa watu wachache (serikali) kwa ridhaa ya watu kwa uhalali kupitia chaguzi kwa mfano Tanzania.

Maendeleo: Kama ambavyo unaweza kusema kuhusu maendeleo kwa upande wako ni sawa. Lakini mimi nasema, kwamba Maendeleo ni hali ya kuwa ama kuwepo kwa mabadiliko yenye kujidhihirisha ama kwa hisia au kwa uhalisi kwa ajili ya kuboresha hali ya mtu ama watu ndani ya jamii. Kwa hiyo kumbe, maendeleo ni mabadiliko chanya ndani ya jamii ya watu, yenye lengo la kuboresha zaidi hali za watu katika uchumi, siasa na jamii.

Hata hivyo, utaweza kupima kwa kutumia vigezo vyako, nayo ni sawa. Lakini kwa kadiri ya siasa ya Tanzania. Maendeleo hupimwa kwa vigezo kadhaa: Afya ya ustawi wa watu ndani ya jamii; Elimu; kuinuka kwa hali ya maisha na upatikanaji rahisi wa mahitaji ya lazima ya watu. Na kwa bahati njema hapa unaweza ukashuhudia vyema katika awamu ya serikali ya sasa ya Rais J. P. Magufuli. Kwamba sekta ya afya na sekta ya elimu zimeweza kuboreshwa vyema. Na kwa kuwa maendeleo ni mchakato basi tegemea kushuhudia maendeleo zaidi kwa siku zijazo.

Muunganiko wa Demokrasi na Maendeleo

Kwa kuwa taifa ni sehemu ya watu na maeneo yote ambayo yanauhusiano na jiografia, kwa maana ya ardhi, mimea n.k ama itikadi na imani vilevile kwa maana ya siasa n.k. Hivyo basi, serikali imepewa jukumu moja, nayo ni kuwahudumia wananchi. Na hivyo kupelekea ulazima wa serikali hiyo kuruhusu kupokea mawazo ya watu hao katika kutimiliza adhima hiyo. Lakini pia ipo haja ya serikali kuruhusu watu wake kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za serikalo kwa ajili kuwahudumia watu hao. Kwa hiyo yote hayo ni kutokana na ushiriki na ushirikishwaji na uhuru na usawa wa watu wote mbele ya sheria.

Kwa jinsi hiyo, ndio tunasema wazi kuwa " Bila Demokrasi Hakuna Maendeleo!"
 
Nakumbuk hii ilikua Individual assignment kwny DS ya NTA level 6.
Ukwel wa hii kitu unategemea na mtizamo wa mtu mmoja-mmoja. Tofaut ya milengo ya watu ndo inaifanya hii mada iwe na mfanano wa 'kuku na yai nani ni wakwanza kufanyika!'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ukweli tupu kuwa, watanzania wanahitaji maendeleo. Lakini haiwezekani ikawa kweli kuwa, maendeleo hayo yanaweza yakapatikana pasipo na demokrasi. Na inafahamika waziwazi kuwa, dhana ya maendeleo ni dhana iliyo pana sana, na kimsingi ni dhana ambayo mjadala wake ni bado unaendelea hata sasa. Kwa maana hiyo ni mjadala endelevu!

Hata hivyo, ili kuweza kuyafikia maendeleo hayo, ni dhahiri kuwa ni lazima kwanza tuweze kuendelea kwenye demokrasi. Ikumbukwe kuwa demokrasi ni hali ya kuwa. Hivyo, kwa jinsi hiyo mchakato wa kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi yanapatikana ndani ya Tanzania kwa watanzania wote, basi ni lazima hali yetu ya kuwa na haki na usawa na uhuru binafsi ndani ya jamii, ipate kuwepo: Hali hiyo ni lazima nayo ipate kuwa nzuri, kwa maana ya demokrasi safi nchini.

Hata hivyo, ni kweli kuwa, kupitia demokrasi, nchi yetu itapata kuboreshwa na kujengwa na sisi sote, kwani ni demokrasi ya uwajibikaji na ya uzalendo ndio inataka hivyo: Kupitia demokrasi, kila raia atakuwa uhuru kwa kutoa nje mawazo yake ambayo ni lazima yawe na tija kwa taifa: Kupitia demokrasi, nchi haitaongozwa kwa utashi wa kiongozi pekee, ila ni kwa msingi wa utawala wa sheria (yaani katiba ya nchi). Kwa hiyo ni ngumu kuitenganisha demokrasi na maendeleo. Maendeleo ni tunda la demokrasi; na demokrasi ndio chachu ya ustawi wa maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Na kwa jinsi hiyo tangu uhuru hata sasa, taifa letu chini ya serikali inayoundwa na CCM, ililitambua hilo. Na kwamba ili kwanza tuweze kuendelea, ilitakiwa kwanza tuipate demokrasi ya uhuru. Na hata baada ya kuwa huru, serikali za CCM za awamu zote zimeipa kipaumbele suala zima la demokrasi ili kuweza kulipatia taifa letu maendeleo katika nyanja zote muhimu. Ifahamike kuwa ni CCM inaamini kuwa, demokrasi kwanza kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Mpaka leo falsafa ya Baba wa Taifa, Mwl Nyerere, kuhusu misingi ya maendeleo haijapata kupingwa ambayo ni Watu, Ardhi, Siasa safi, Uongozi bora.

Kujadili maendeleo mtu au mwanazuoni yabidi ajikite katika misingi hiyo mikuu. Swali ni [/I]je, demokrasia inaangukia wapi katika misingi hiyo?[/I]

Baba wa Taifa alikuwa na maana kwamba mambo hayo manne yanategemeana sana na moja likikosekana huenda mengine kushindwa kufanya kazi.

Ifahamike pia kwamba Mwl hakuyataja hayo mambo manne, kama misingi ya maendeleo, kwa kubahatisha wala hakuyataja kirahisi.

Hivyo basi tunapojadili demokrasia, kama ni msingi wa maendeleo, tuzingatie jinsi Taifa letu linavyotumia misingi hiyo kwa maendeleo yake. Km je, Tanzania ina watu wakuifanya iwe mahala salama pa kuishi? Kwa maana ya Taifa moja, lisilo na ubaguzi wala utengano, lenye umoja na mshikamano katika ukabila, dini, utajiri, umaskini na hali yote ile iwayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom