Bila CHADEMA huenda mpaka leo tusingefahamu ufisadi na Madudu ya watawala wetu.

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,733
7,611
Upinzani umesaidia leo hii hata mlala hoi wa kule kwetu sigimbi anafahamu maana ya ufisadi upinzani si uadui bali ni wenye mrengo wa kusaidia pale ambapo serikali imejisahau kukumbusha.
Leo hii bila upinzani tujiulize tungekuwa wapi?
Upinzani ni ukombozi wetu kifikra leo tunatembea kifua mbele kwasababu ya changamoto ya upinzani.
Bila upinzani makini leo hii Raisi angekuwa Membe au Lowasa.
Upinzani ndio zao lililo wezesha Mheshimiwa Magufuri kuwa Raisi.

Bila upinzani hakuna changamoto watawala watajisahau wakidhani ni miungu watu.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 
Umenena mkuu! Bila upinzani hata bashite,chalamila,sakaya,..na wamwambafai wengine wasingelikuwepo walipo,Bila upinzan kubudu asingelala hoteli Manhattan. Tutakukumbuka mzee wetu Mtei kwa juhudi zako,bila kusahau mchango wa lipumba&Mrema japo walikuja kengeuka.
 
Back
Top Bottom