Bila CCM madhubuti upinzani imara nchi yetu itayumba...

Ni wazi na imeendelea kudhihiri kuwa upinzani wa Tanzania umeyumba. Wamepoteana wamechanganyikiwa. Ni vyema na muhimu kwa sasa Kama taifa tuone umuhimu wa kupatikana upinzani wa dhati. Hawa akina Ole Medeye na wenzake waliohamia UDP wanaweza ku sound valid. Chadema imezama..CUF hoi...ACT zii...jamani NCCR wee!!!!
wewe na ccm yako ndo mmeyumba mmechukua sera za upinzani mkaweka kwenu na bado zinawashinda
 
Ndugu, usitokwe sana mapovu. Mna mahakama tiss na takukuru na majaji na magereza. Mnachoshindwa kuvitumi hivyo vyombo vyenu kumkamata na kumshtaki ni nini? Au polisi na intelijensia yenu ni ya kuzuia mikutano yao na kutawanya maandamano yao ya amani tu? Na hao majaji wenu wana kazi ya kusikiliza kesi za kubambikiwa wapinzani ila ya ufisadi inabidi mkawakodishe kutoka Afrika kusini!? Acheni ubabaishaji wajibikeni kwani mlijipa mamlaka ya kuwafisidi wananchi ili kuwahadaa na issue ya ufisadi huku nanyi mmejaa kuimeng'enya nchi.
Arudi aje kufanya nini kwenye chama ambacho hakifahamiki. Mtamwitaje mtu fisadi wakati huo huo mnammezea mate? Ndio maana wananchi walishindwa kuwaamini. Leo mnawaita watu mafisadi keshi mnawakaribisha kwenye chama chenu kama na nyie sio mafisadi ni nini.
 
Kuna viashiria gani vinavyowafanya waringe?

Tathimini imeonyeshakuwa katika kipindi hiki kumekuwa idadi kubwa ya wasafiri wanao ninginiza miguu kwenye madirisha ya mabasi baada ya uchunguzi kufanyika zaidi ikagunduliwa ni wasukuma.
Walipo shauriwa waache kuninginiza miguu walitishia kwamba watatoa ripoti kondakta na Dereva watumbuliwe kwa kiwakataza.
Teh teh teheeeee.
 
Kwa yeyote yule ambae hakijui chama cha ACT wazalendo.asome azimio la tabora kwanza.
 
Ni wazi na imeendelea kudhihirika kuwa upinzani wa Tanzania umeyumba. Wamepoteana wamechanganyikiwa.

Ni vyema na muhimu kwa sasa Kama taifa tuone umuhimu wa kupatikana upinzani wa dhati. Hawa akina Ole Medeye na wenzake waliohamia UDP wanaweza ku sound valid. Chadema imezama..CUF hoi...ACT zii...jamani NCCR wee!!!!

Kama CCM itaendelea kuwa chamadola na kushabikiwa iwe hivyo huwezi kuwa na upinzani imara. Sasa kama chama cha siasa kinazuiwa kufanya siasa unategemea nini. Juu la hilo weka katiba mbovu. Vyama mfu ndio vinapigiwa jaramba na CCM au washabiki wake . Walisemaga vyama vya upinzani ni vya msimu jamaa wamejipanga sasa wanapiga marufuku hata mikutano ya ndani. Imagine mkuu wa chama anazuiwa kutembelea matawi ya chama chake-halafu mtu anakuja kutueleza udhaifu wa vyama vya upinzani. Kule Zanzibar vile vyama mfu ndio viko serikalini umeona wapi? Pamoja na mapungufu yao tunahitaji kuvipa support vyama vya upinzani au sivyo hatuta pumua. Katiba nzuri zaidi inahitajika sio ile ya 6 inayoendeleza tanganyika kuvaa koti la muungano, constitutional dictatorship (kama alivyosema JKN) na kuwa na CHAMADOLA kinachobomoa bank kuu ili kishinde uchaguzi na kuzuia wapinzani wasifanye siasa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ccm itabaki kuwa juu daima..haijajengwa kwa misingi ya udini ,ukanda wala ukabila.Kupanda ngazi ndani ya CCM ni rahsi na inawezekana ila UPINZANI hua wana watu wao..hawawezi kufanikiwa kamwe kama hawatojibadilisha
 
Upinzani umeyumba, wamechanganyikiwa na wamepoteana lakini pamoja na upinzani kuwa katika hali mbaya kiasi hiki Serikali bado inawahofia sana UKAWA ndani na nje ya Bunge hata kufikia dikteta Magufuli kuamua kubaka demokrasi nchini kwa kiwango cha juu sana kupitia polisiccm kwa kuzuia mikutano au maandamano ya UKAWA wakati huo huo MACCM yakiendelea na mikutano na maandamano yao.

Hawakukosea waliosema kwamba kamwe akili ndogo haiwezi kushinda akili kubwa.
 
Chadema ni saccoss ya comrade. Yupo pale hadi ajisikie kuondoka. Then upinzani unalilia demokrasia, hiyo saccoss haina demokrasia halafu mnalilia kitu hamuwezi kukiishi?
 
Ni wazi na imeendelea kudhihirika kuwa upinzani wa Tanzania umeyumba. Wamepoteana wamechanganyikiwa.

Ni vyema na muhimu kwa sasa Kama taifa tuone umuhimu wa kupatikana upinzani wa dhati. Hawa akina Ole Medeye na wenzake waliohamia UDP wanaweza ku sound valid. Chadema imezama..CUF hoi...ACT zii...jamani NCCR wee!!!!
Hivyo vikizama si ndio furaha kwenu au hata hilo nalo hamlitaki
 
12647110_1427276657286748_8135471195662354545_n-png.357227
 
Ni wazi na imeendelea kudhihirika kuwa upinzani wa Tanzania umeyumba. Wamepoteana wamechanganyikiwa.

Ni vyema na muhimu kwa sasa Kama taifa tuone umuhimu wa kupatikana upinzani wa dhati. Hawa akina Ole Medeye na wenzake waliohamia UDP wanaweza ku sound valid. Chadema imezama..CUF hoi...ACT zii...jamani NCCR wee!!!!

Inahitaji akili ndogo sana kufanya tathmin kama yako! Yaan kiufupi ni akili ya panzi kuamini upinzani umekufa. Ingekua upinzani umekufa CCM wasingepiga marufuku mikutano ya upinzani.
Huo ni woga wa upinzani tu ndo maana wameamua kufanya hivyo. Kama CCM wako sawa na hawaogopi upinzani, waruhusu mikutano!
Yaan wewe unaona kivuli chako tu, na wala huwazi mbali. Pole kama unaamini upinzani unakufa.


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nianze na kuweka wazi kuwa hapa andiko hili ni kwa wenye hekima tu watalielewa.

Kwa hali ya kawaida mtu akifanya initial credibility lazima atakosea na kunihukumu kwa kunihusisha na itikadi ya chama fulani.

Lengo sikuonesha itikadi bali kujadili falsafa ya maendeleo katika siasa za kidemokrasia ns hasa demokrasia ya kweli.

Kichwa cha habari hapo juu kinaelezea mada ya andiko hili kama ifuatavyo " HAKUNA CCM IMARA BILA UPINZANI IMARA NA KINYUME CHAKE".

Ninachotaka kusema ni siasa za Tanzania kama mfano wa siasa nyingi za bara la Afrika. Dhima ya demokrasia hasa demokrasia ya kweli (true/real democracy) imekuwa tatizo kubwa kwa nchi zetu kiafrica maarufu kama nchi zinazoendelea.

Zipo dhana potofu nyingi kuhusu uimara wa serikali zinazoongozwa na vyama tawala kuwa serikalo imara inatokana na kuwabana wapinzani katika mfumo wa vyama vingi kwa kutumia dola na sheria ambazo zinatungwa kwa makusudi maalum.

Nitatoa mifano ya hapa nchini kwetu, hali ya sintofahamu iliyogubika taifa letu ni ukosefu wa demokrasia ya kweli licha ya nchi kuwa ya kimodemokrasia kwa mana ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vinaruhusu ushindani wa kisiasa kwa sera na itikadi ya vyama vingi.

Zipo sheria kadha kama usajili wa vyama vya siasa,sheria ya usalama wa taifa na sheria ya vyombo vya habari na nyingine nyingi tu ambazo kusema kweli zinatumika vibaya katika mchakato wa kidemokrasia hasa kwa kuwabana wapinzani wasikue kwa kufanya ukandamizaji wa kisiasa mifano ipo mingi mara kadha kumekuwepo na makalipio ya msajili wa vyama siasa akivitishia kuvifuta baadhi ya vyama vya siasa kwa kuvihusisha na uchochezi chini ya sheria tajwa hapo juu.

Ukatazwaji wa mikusanyiko ya kisiasa na mikutano ya siasa ndani na nje ya vyama kufuatia tamko la mh. Rais na katazo la jeshi la polisi na matumizi mengine ya mabavu katika kuiminya demokrasia nchini mwetu, narudia kusema BILA UPINZANI IMARA SAHAU KUWA NA CCM IMARA na KINYUME CHAKE. Hili halina ubishi tumekuwa tunashuhudia CCM ikitolewa kamasi na kuamshwa usingizini na UPINZANI (CHADEMA) juu ya utendaji mbovu wa serikali na vitendo vya rushwa na ufisadi uliokithiri wa mali za umma. Ata mh. Rais na makamu wake pamoja na waziri mkuu wanakili upungufu huu hasa kwa serikali zilizotangulia.

Ipo shida kubwa ya wananchi kutoelewa dhana nzima ya kuwa na VYAMA VYA UPINZANI IMARA nchini, kwa nyakati tofauti nimemsikia mh. rais wangu akisema wananchi hawahitaji vyama vingi ili kupata maendeleo, dhana hii ni potofu na isiyo ns mshiko na niseme kwa dhati kabisa KAMA RAIS MAGURI HUONI UMHIMU WA VYAMA VYA UPINZANI KATIKA KUCHAGIZA MAENDELEO, hasa kwa kuifanya serikali isisahau majukumu yake na kusinzia basi nitasema na kurudia rudia kukutulia shaka kama una nia ya dhati ya kutuletea maendeleo nchini mwetu.

Kazi ya vyama vya upinzani katika kutoa elimu ta uraia ( civil education) imekuwa kubwa na kuwafanya wananchi kujua na kuhoji utendaji wa serikali na hivyo kuongeza kasi ya uwajibikaji wa serikali katika kutatua matatizo ya wananchi. Kwa serikali makini UIMARA WA UPINZANI NIBKIPIMO KIZURI cha utendaji wa rais na serikali yake. Namkubuka dr. Xavery Rwaitama aliwahi kusema hatamani kuona CCM kama chama cha upinzani chenye nguvu siku moja, akimanisha ata CCM ikitoka madarakani haiombei ife maana CHADEMA madarakani bila CCM imara tunaweza shuhudia hali mbaya zaidi ya hii.

Mwisho kabisa niwatie moyo Wapinzani kwa maana ya vyama vya upinzani kutokurudi nyuma katika kupigania demokrasia ya kweli na kuikumbusha serikali kuwa BILA UPINZANI IMARA CCM imara ni ndoto, na kwa wananchi hasa wasomi ambao uelewa wetu upo juu kidogo tushiriki katika kuijenga demokrasia kipitia vya vyetu tulio ccm na upinzani demokrasia haina chama ni mhimu kwa maendeleo ya nchi na mstakabali wa utengamano na amani ya nchi yetu.

Misingi ikiharibika wenye haki watafanya nini?

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Uwe na kiburi kwa serikali?
Uwe na unyenyekevu kwa serikali?
Usionyenyekea wala kuwa na kiburi ila maslahi yao yalindwe?
AU WEWE UNATAKAJE?
 
Back
Top Bottom