kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
Tanzania ni kati ya nchi zinazokuwa kidemokrasia na kiuchumi, pamoja na kwamba makuzi haya hayaendani na kasi halisi pamoja na hitaji la ongezeko la watu. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ikiacha mbali sana ongezeko la uchumi na ajira. Ukuaji huu unaleta hamasa kwenye ukuaji wa demokrasia wananchi wakiwa na kiu kubwa ya maendeleo huku idadi kubwa ya vijana wakimaliza elimu ya sekondari na vyuo mbalimbali na kufanya mahitaji yao kuwa ya kisasa zaidi.
Mawasaliano ya kikua kwa kasi, na dunia kuwa kiganjani inawafanya watawala wa sasa kuhitaji kuwa na kasi kubwa sana ya uwezo wa kialkili na kutambua kwa kasi mabadiliko ya dunia na hitaji halisi la watu wanaowatawala. Ukifanya tathamini utaona kuna disconnectoin kubwa kati ya watawala na watawaliwa. Wananchi wakiwa wanaeleimika siku hadi siku kujua haki zao za msingi na mahitaji hasa baada ya kulipa kodi, watawala bado wapo usingizini wakifikiri wanaweza kuendelea kucheza mechi chumbani na kutangaza mshindi wa mezani kama ilivyo zooleka siku zote za utawala wa Tanzania.
Makundi yalioko ndani ya serikali ambayo yanawania au yanataka kuingia magogoni 2015, yakiongozwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, kimadaraka au kiikulu yataipeleka nchi kuzimu 2015. Yapo makundi ndani ya serikali yanaoyoamini lazima wawe ikulu kwa gharama zozote, makundi ya mafisadi tayari yamepenyeza uwezo wao na kutengeneza nyezo za kuwafanya kuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii ili kuingia magogoni. Mkuu wa kaya naye akiwa na kundi analo amini ndilo linafaa kumrithi kuingia ikulu. Wapinzani tayari wanajipanga vizuri kuhakikisha kuwa wanapata kura za kutosha kuingia ikulu.
Watawala wakijua kuwa uchaguzi huru na wa haki hauwezi kurudisha chama tawala ikulu, wameamua kucheza na muda ama kutotekeleza swala la katiba mpya, au kuiwekea viraka ambayo anbayo ipo na kuacha kurekebisha mambo muhimu kama tume ya uchaguzi, haki za binadamu, majukumu ya raisi, uhuru wa mahakama, bunge nk havitaguswa. Tutaingia 2015 tukiwa fully hasira.
Nawaomba watawala wa sasa hasa Mh JMK kuwa bila uchaguzi huru 2015 sio sisi tu akina pangu pakavu tutakuwa na hali mbaya kiusalama, ila ni wao wanaohitaji heshima na sehemu ya kuitwa raisi mstaafu ndio watakuwa na hali mbaya. Watajuta ni kwanini hawakufanya haya mapema wakati nchi ikiwa imetulia. Viongozi wa Libya, Misri, Tunisia, Yemen, nk wanatamani wangesikiliza washauri na kilio cha watu wao mapema na kurekebisha hali. Fedha mlizo waachia wapambe waibe na kujifanya mabilionea bila kulipa kodi, zitatugharimu sote. Wanataka kujilinda kwa kuhakikisha wanabaki madarakani.
Kila mtanzania mwenye mapenzi mema, akubali tuwe na katiba huru yenye kuwabana wote wenye nia mbaya na tanzania yenye neema. Katiba yenye tume huru, mahakama huru na bunge huru. Tukiwa na mihimili huru itatusaidia kuwabana wote wenye nia ya kuipeleka nchi kuzimu.
Ni mimi Mzee wa kijiji