Bila busara uchaguzi 2015 ni vita na vurugu-mwisho wa amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila busara uchaguzi 2015 ni vita na vurugu-mwisho wa amani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Oct 11, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni kati ya nchi zinazokuwa kidemokrasia na kiuchumi, pamoja na kwamba makuzi haya hayaendani na kasi halisi pamoja na hitaji la ongezeko la watu. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ikiacha mbali sana ongezeko la uchumi na ajira. Ukuaji huu unaleta hamasa kwenye ukuaji wa demokrasia wananchi wakiwa na kiu kubwa ya maendeleo huku idadi kubwa ya vijana wakimaliza elimu ya sekondari na vyuo mbalimbali na kufanya mahitaji yao kuwa ya kisasa zaidi.

  Mawasaliano ya kikua kwa kasi, na dunia kuwa kiganjani inawafanya watawala wa sasa kuhitaji kuwa na kasi kubwa sana ya uwezo wa kialkili na kutambua kwa kasi mabadiliko ya dunia na hitaji halisi la watu wanaowatawala. Ukifanya tathamini utaona kuna disconnectoin kubwa kati ya watawala na watawaliwa. Wananchi wakiwa wanaeleimika siku hadi siku kujua haki zao za msingi na mahitaji hasa baada ya kulipa kodi, watawala bado wapo usingizini wakifikiri wanaweza kuendelea kucheza mechi chumbani na kutangaza mshindi wa mezani kama ilivyo zooleka siku zote za utawala wa Tanzania.

  Makundi yalioko ndani ya serikali ambayo yanawania au yanataka kuingia magogoni 2015, yakiongozwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, kimadaraka au kiikulu yataipeleka nchi kuzimu 2015. Yapo makundi ndani ya serikali yanaoyoamini lazima wawe ikulu kwa gharama zozote, makundi ya mafisadi tayari yamepenyeza uwezo wao na kutengeneza nyezo za kuwafanya kuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii ili kuingia magogoni. Mkuu wa kaya naye akiwa na kundi analo amini ndilo linafaa kumrithi kuingia ikulu. Wapinzani tayari wanajipanga vizuri kuhakikisha kuwa wanapata kura za kutosha kuingia ikulu.

  Watawala wakijua kuwa uchaguzi huru na wa haki hauwezi kurudisha chama tawala ikulu, wameamua kucheza na muda ama kutotekeleza swala la katiba mpya, au kuiwekea viraka ambayo anbayo ipo na kuacha kurekebisha mambo muhimu kama tume ya uchaguzi, haki za binadamu, majukumu ya raisi, uhuru wa mahakama, bunge nk havitaguswa. Tutaingia 2015 tukiwa fully hasira.

  Nawaomba watawala wa sasa hasa Mh JMK kuwa bila uchaguzi huru 2015 sio sisi tu akina pangu pakavu tutakuwa na hali mbaya kiusalama, ila ni wao wanaohitaji heshima na sehemu ya kuitwa raisi mstaafu ndio watakuwa na hali mbaya. Watajuta ni kwanini hawakufanya haya mapema wakati nchi ikiwa imetulia. Viongozi wa Libya, Misri, Tunisia, Yemen, nk wanatamani wangesikiliza washauri na kilio cha watu wao mapema na kurekebisha hali. Fedha mlizo waachia wapambe waibe na kujifanya mabilionea bila kulipa kodi, zitatugharimu sote. Wanataka kujilinda kwa kuhakikisha wanabaki madarakani.

  Kila mtanzania mwenye mapenzi mema, akubali tuwe na katiba huru yenye kuwabana wote wenye nia mbaya na tanzania yenye neema. Katiba yenye tume huru, mahakama huru na bunge huru. Tukiwa na mihimili huru itatusaidia kuwabana wote wenye nia ya kuipeleka nchi kuzimu.

  Ni mimi Mzee wa kijiji
   
 2. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena vyema na mwenye kusikia na asikie ila kwa kuwa walio wababe wamejaa kiburi na tusubiri siku watanganyika watakapo fikia mwisho wa kuvumilia na hapo ndipo tutasikia vilio kila kona ya nchi hii.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Haya si maneno CCM wanapenda kusikia .Ni machungu na ushauri wote ni msamiati mzito kwao so nina mashaka mno .Wacha nivute subira .
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapo umenena ukweli hata mimi hiyo hatari ni kama naiona bila mabadiliko ya tume ya uchaguzi moto utawaka
   
 5. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  bila mabadiliko makubwa ya sheria mama ya nchi - katiba - ni kweli tutaingia kwenye vurugu kubwa sana 2015...kama tutaifikia hiyo 2015 salama...kitu ambacho binafsi sikioni kikitutokea kama nchi
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Sasa mtu kwenye kampeni za uchaguzi unagawa MAHINDI - maelezo eti serikali inagawa misaada kwa wananchi - haya ndiyo madharau yatakayopeleka tutwangane tu ili tuheshimiane.

  Mtu anakula dili - tunakuja kupata mgawo wa umeme masaa 18 giza totoro, ukiuliza eti utavunja amani - amani gani gizani wakati kwake umeme unawaka masaa 24 - haya ndiyo madharau yatakayofanya Tutwangane ili tuheshimiane.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,933
  Trophy Points: 280
  Nyie wote kwanini msimgongee "like" kama mmeipenda thread aliyoianzisha?Acheni ubinafsi ambayo ndo tabia yenu kubwa.Mnachangia eti nimeipenda.Show it stupid,dont just say it.Inaudhi sana.Sasa mnadhani hicho kitufye kimewekwa ili iweje?Na hii ni kwa wote hapo juu mliochangia kuwa mmeipenda hii thread lakini hukui "like".Mimi nimeipenda pia na nime onyesha hivyo ili kumuencourage mleta hoja.Damn!
   
 8. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kwamba ili CCM ijihakikishie kuwa madarakani, wanataka Umri wa kushiriki katika chaguzi uongezwe badala ya kuanzia miaka18 uende mpaka 24 hii ni baada ya kugundua kundi kubwa la vijana ndiyo wapenda mabadiliko, amini usiamini hili litawekwa kwenye katiba na idea hii itatolewa na kiongozi wa chama cha upinzani mamluki.
   
 9. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ccm itaendelea kutawala kutokana na hazna ya ujinga wa watanzania ambayo bado wanayo
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Segwanga, sikubaliani na hoja yako. CCM wanatawala kwa hila na kushinda chaguzi kwa kuchakachua, kutumia vitisho vya dola-polisi na JWTZ (rejea kauli ya Lt Gen Shimbo mwaka jana baada ya kuoneka jahazi la CCM likisukwasukwa).

  Kwa taarifa yako kama nloyataja hapo juu kama hayapo, CCM kwishney. Ulitegemea Wapinzani kushinda Kasulu, Kibondo, Nguruka, Meatu, Bukombe, Ukerew na Biharamulo?
   
 11. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa hali ilivyo sasa kwa mfano mdogo tu kwa yale yaliyofanyika Igunga.......kama itakuwa hivi hivi 2015....Hatukwepi kumwaga damu hii hii haitakwepeka kabisa......Kama hatuna katiba mpya ambayo itakuwa na matakwa ya wote yenye kutoa haki sawa kwa wote.......damu kumwagika ni Lazima....na baada ya hapo CCM wasijidanganye kuwa wataweza kutawala tena sio kweli ......tutamwaga damu na mwishowe wao ndio itakula kwao!!!!!
   
 12. T

  Typical Tz Member

  #12
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa mkuu, nini kifanyike ili kuondoa huo ujinga ambao watanzania wengi wanao hasa walioko vijijini?
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu huyu anayetaka kuja na ya miaka 24 atakuwa anatumia masaburi tu. Ina maana anataka kubadilisha kitu ambachokilishakua stadard duniani kote? Tell him/her he/she is the only stupid in this world!
   
 14. h

  hahoyaya Member

  #14
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa uongozi huu wa sasa wa Ccm Mkama,Nnauye,Nchemba na Wasira hakika 2015 hatuwezi kuvuka salama.Matamshi waliokuwa wanayatoa Igunga yanaashiria shari ni suala la wkt tu.Hivi 2lishajiuliza wale vijana walionekana siku ya kutangaza matokeo wakiwana mapanga,pinde na mishale wanalipwa na nani?na kwa manufaa gani?Kulikuwa na taarifa kuna mtu aliingia duka moja akanunua mapanga 30,je baada ya huo uchaguzi hayo mapanga yamehifadhiwa au yametupwa!Na kama yamehifadhiwa,yatatumika wapi baada Igunga?Hawa mabazazi ni hatari kuliko tunavyofikiria.
   
 15. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni kweli watanzania wengi walioko vijijini bado wanapata habari na elimu kwa kasi ndogo. Ila siku zinavyozidi kwenda elimu ya uraia na mahitaji yao yanapanuka na kuanza kuona machungu na kujua haki zao. Wengi wa watoto waliozaliwa miaka ya 80 ndio wanakuwa kina baba na mama na wapiga kura 2015. Wengi wao wamemaliza walau darasa la saba. Chaguzi zilizopita utaona ziligubikwa na propaganda za uongo. Ila siku zinavyozidi kwenda wananchi wanataka haki na ukweli wanahitaji mahitaji ya msingi ambayo huwezi kuendelea kuwadanganya tena. Matumizi ya rushwa yatatuletea vita kwani rushwa huzaa usaliti.

  Ni busara tu na viongozi wanaopenda kuona mbali na heshima ya kweli wanaweza kuona hatari hii na kuizuia. Ila kwa Tawala zetu za kiimla watasubiri mpaka wote tuwe kwenye chumba cha gesi ndio waanze kuomba hewa. Elimu ya uraia inakuwa kwa kasi kubwa. Kila kona ukienda watu wanaongelea mahitaji yao na kumjua mbaya wao. Wala rushwa wameongezeka kwa kiwango cha kutisha, uhujumu umekuwa kama kazi, madaraka yamekuwa kama kiwanda cha mtu binafsi. Tabaka la walionacho na wasionacho linaoneka. Chuki za masikini dhidi ya walionacho inakuwa.
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,171
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  wakati mnafikiri kupandisha umri wa kupiga kura wenzetu waliostarabika wanafikiria kuushusha umri huo kuwa miaka 16!
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Bomu hili linatengenezwa na ccm wenyewe.na kiukweli hili halikwepeki kabisa kwa sababu hawa watawala wa leo wanawaza madaraka ya milele na ndio maana wao leo wanagombana maana wameshaanza maandlizi ya kutengeneza makundi ndani ya chama wakati huo huo watalazimisha katiba ya zamani itumike,wala hatakubali kuwa na tume huru,je unategemea nini?na hasa moto utawaka kwenye katiba mpya maana wanajijua wana maovu mengi hivyo hofu ya kushitakiwa itawafanya wa-delay kuandikwa kwa katiba mpya,na kwa kuwa watnzania watataka katiba mpya na tume huru basi hapo matumizi ya nguvu ya dola-polisi na jeshi yatakapoanza,lakini wategemee upinzani nkali kutoka kwa wananchi kwa hali ambayo inaonekana leo.
  watanzania hakuna kulala mpaka kieleweke
   
Loading...