Kuoa bikra n ndoto za wanaume weng hao watoa mapovu n wale waliotolewa bikra zao zaman sasa wanatoa mapovu kujifariji tu
 
Habari wakuu.

Mada hii ni ngumu kidogo na inagusa watu muhimu kwenye jamii. kitu pekee nitakachokihitaji toka kwa wataonipinga na nukuu na aya kutoka kwenye Biblia.

Askofu/Mchungaji au kuhani yeyote aliyepakwa mafuta moja ya masharti yatakayomfanya atimie ni pamoja na kuoa mwanamwali yaani bikra na tena kuoa mke mmoja. Jambo hili ni kiashiria cha usafi na utakatifu kwa mtumishi wa Mungu. Sijui kwa nini jambo hili halizingatiwi ndio maana siajabu watumishi wengi wa Mungu hata waombe kwa kujirusha na kujikata kata lakini maombi yao hayajibiwi kutokana na kutofuata taratibu za kikuhani.

Siwalaumu wale wanaoenda kuombewa na watumishi hawa wasiofuata sheria za kikuhani.

Zifuatazo ni nukuu kutoka kwenye Biblia Zinazoonyesha kuwa mtumishi wa Mungu(Waliolengwa zaidi ni makuhani, wachungaji, Maaskofu n.k) kuwa wasioe mtu asiye bikra, mjane, kahaba wala aliyeachwa na mumewe.

Mambo ya walawi 21:
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

Mambo ya walawi 21;
7 Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.

Ezekiel 44;
22 Wala hawataoa wanawake wajane, wala mwanamke aliyeachwa na mume wake; lakini watatwaa mabikira wa wazao wa nyumba ya Israeli, au mjane aliyefiwa na mumewe kuhani.
23 Nao watawafundisha watu wangu tofauti iliyopo kati ya vitu vitakatifu na vitu vya sikuzote, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi.

Karibuni kwa mjadala nipo tayari kwa mafundisho lakini sitaki maneno matupu bali nahitaji Aya na nukuu kutoka kwenye Bible.
 
Back
Top Bottom