Bila Barakoa, Muhimbili huingii kuanzia leo. Msindikizaji mmoja tu

KakaJ uliagiza kontena la barakoa nini? Sio kwa uhamasishaji huu. Tutavaa tu tukienda hapo hakuna namna ni kutii sheria bila shurti
 
Hii itafaa👇
IMG_20210623_060348.jpg
 
Kwa hakika serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa vitendo kutuvusha salama. Wimbi la tatu si la kufanyia mzaha hata kidogo.

Kongole kwenu serikali ya mama Samia.


Bila Barakoa kuanzia leo haingii mtu Muhimbili. Hili ni la kheri sana kwani kinga ni bora zaidi kuliko tiba.

Hii ni habari njema kabisa. Wigo na uongezwe sasa, kufika kote kuliko na mazingira hatarishi yaani kuliko na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Kwenye usafiri wa umma, masokoni nk kusiachwe bila usimamizi.

Inapobidi kutumia kiwango fulani cha nguvu kama hivi kwa wasiotaka kuelewa kwa hakika ni sawa kabisa.

Pole pole, kwa pamoja mbona tutavuka tu?
Ila tuwaombe waondoe hiyo "sauna bath" ya kujifukiza enzi hizo. Inaleta taswira mbaya kwenye taasisi yenye heshima kama Muhimbili.
 
Si zile USD 500+ tulishaahidiwa, tutavaa mask hadi chooni ili hiyo trilioni na ushee tuipate.
 
Kwani lile dude la kujifukiza walisha liondowa? Wataalamu wetu wanaumbishwa sana na siasa, sijui kwa nini?

Nchi ilikuwa ikiongozwa na wanyonge tokea chini hadi juu. Kama dude la nyungu lingalipo litakuwa lilikwisha pigwa lockdown!

Wanyonge = wapiga debe, boda boda, mama lishe, sungu sungu, machinga na wa namna hiyo.

Kukubalika awamu ile ilihitajika jitihada za makusudi za kuwamo katika kundi hilo. Kina mparamagamba, daktari gwaji, kina daktari michembe, daktari makumbi nk walikubalika zaidi. Huenda njaa zao hazikuwa na simile hata kidogo.
 
KakaJ uliagiza kontena la barakoa nini? Sio kwa uhamasishaji huu...tutavaa tu tukienda hapo hakuna namna ni kutii sheria bila shurti

Sifanyi biashara hizo ila kuamriwa fate na hasa ihusuyo uhai na wale wanyonge wa awamu ile kuna kera sana. Kwani hata shule tulikwenda kutembea?

Wanyonge = machinga, wapiga debe, boda boda, mama lishe, na wa namna hiyo:


Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom