Bila aibu shoga asimulia maisha yake

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,333
Vitendo vya Ibrahim Mohamed Anti Suzy havikuwapendeza watu wengi hasa wanaume. Alipingwa mitaani, barabarani na maisha yake yakawa ya kujificha mithili ya panya.

"Niliwahi kupanga nyumba karibu na msikiti, majirani na viongozi wa msikiti wakaamua kunifukuza wakasema nitawafundisha watoto wao tabia mbaya. Wakanirudishia kodi yangu nikaenda kupanga chumba kingine"anasema

Si hivyo tu, bali anazomewa barabarani, kutukanwa, wakati mwingine watu kukataa kumpa mikono au hata kumsaidia anapougua.

Anti Suzy anasema, moja ya tabu zake kuu ni kuingiliwa na wanaume na kubakwa mara kwa mara jambo ambalo linamkosesha raha hasa ukizingatia nyumba yake ni chakavu.

"Juzi waliniingilia wanaume wanne, walifika usiku saa tisa, wakasukuma mlango kwa nguvu, wakanibaka wote," anasema.

Kijana huyu anasema pamoja na kuwa na tabia za ushoga, mwendo wake, sauti na jinsi alivyo havifichi kubaini kuwa ni mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Anasema anapovaa mavazi ya kiume, ndipo watu humshangaa kwani anakuwa na sura ya kike, mwendo wa kike, sauti ya kike kasoro mavazi tu.

"Lakini nikivaa khanga au sketi ndefu, hakuna mtu anayejua kuwa mimi ni mwanamume na nimeshawahi kupata mwanaume alidhani mimi ni mwanamke alipofika chumbani alitimua mbio" anasema.

Mwaka 2010 Anti Suzy alikwenda kupima virusi Vya Ukimwi na hapo alipewa majibu yaliyomshtua ambayo hata hivyo hakuyaamini majibu hayo.

Anasema hakuweza kuamini majibu ya kuwa ana VVU kwa sababu alikuwa na afya njema, alikuwa haumwi chochote kile.

"Nilipima hospitali zaidi ya tatu, Bugando, Muhimbili na Kilimahewa na majibu yalikuwa yaleyale kuwa ni nimeathirika" anasema

Anti Suzy hata hivyo hakuacha tabia hiyo, aliendelea akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kujipatia kipato chake cha kila siku, hadi mwaka jana hali yake ilipokuwa mbaya zaidi.

Alipoanza kuugua, ilimpasa kwenda hospitali na kinga ilionekana imeshuka kwa kiasi kikubwa hivyo akashauriwa kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU.

"Nilianza kutumia dawa hali yangu ikawa nzuri tu, lakini tabia haina dawa, bado sikuacha tabia za ushoga, ninaendelea nazo mpaka sasa" anasema

Hata hivyo, Anti Suzy anasema, ana neno la mwisho ambalo anataka kuwaambia Watanzania wote kuhusu maisha ya ushoga na vijana wa sasa.

"Ninajua siwezi kuumaliza mwaka huu kabla sijafa. Ninajuta kuwa katika hali hii, lakini naamini mazingira na wazazi kutokujua jinsi ya kuniongoza ndicho chanzo cha haya yote" anasema

Anti Suzy pia anasikitika kwa jinsi wanaume ambao humbaka bila kutumia kinga wakiwa hawajali kama ana VVU ama la.

Hata hivyo, Anti Suzy aliwahi kuishi na mwanamume, nyumba moja kama mume na mke kwa muda wa miaka minne.

Maisha duni ya ushoga

Ukimtazama usoni Ibrahim Mohamed huwezi kugundua kwa wepesi kuwa ni mwanaume. Hasa akiwa amevaa vazi lake analolipenda, yaani khanga, top dress na viatu aina ya ‘sandals'.

Lakini pia kwa sauti, ukosefu wa ndevu kidevuni na nywele zake ndefu pia ni sifa tu ambazo zitakufanya usikubali kwa haraka kuwa unayemtazama mbele yako ni mwanamume.

Namkuta kijana huyu katika makazi yake yaliyoko pembezoni mwa Mto Msimbazi, karibu na Barabara Kuu ya Morogoro. Sitakosea nikisema kuwa makazi ya Anti Suzy ni duni. Anaishi katika jumba bovu ambalo licha ya kuwa na paa chakavu lakini pia amezungukwa na maji yaliyotokana na mvua zilizonyesha hapa jijini siku za karibuni.

Maji hayo si nje ya nyumba tu, bali yamo hata ndani ya chumba hicho jambo lililosababisha kupanga matofali ndani ili kuzuia miguu yake isiyakanyage. Ndani ya chumba hicho, kuna kimeza kidogo chenye vikombe viwili, birika, bakuli pamoja na kitanda.

Ukutani kuna msumari ambao ametundika mfuko wa plastiki ambao una nguo zake kuukuu kadhaa,vipodozi na vifaa vyake vingine.


"Baba na mama walinigundua mapema sana kuwa sina tabia za kiume, nilikuwa na vitendo vya kike tangu mdogo," anasema ant i Suzy

Anasema badala ya kucheza mpira wa miguu alipenda kucheza rede, badala ya kupenda kazi za bustani au kukata kuni, alipenda kupika, kuchota maji na kuosha vyombo.

"Siku moja niliiba sketi ya shule ya mdogo wangu nikaivaa nikaenda nayo shule, mwalimu alipogundua alinishangaa mpaka akashindwa kuniadhibu… alidhani labda nina wazimu," anasema anti Suzy

Wazazi wake walipogundua tatizo hilo, walichukua uamuzi wa kumpeleka hospitali wakiamini kuwa pengine ushauri wa wataalamu utawapa mwanga wa kumtoa mtoto wao katika vitendo vya kike na kuwa mwanamume kimwili na kitabia.

"Baba alikuwa anataka niwe mwanaume, alichukia sana mimi kuwa na tabia ya kike," anasema Suzy

anti Suzy anasema wazazi wake walimpima na madaktari wakagundua kuwa ana vichocheo zaidi vya kike kuliko vya kiume na hicho ndicho chanzo cha yeye kuwa hivyo alivyo.

Wazazi wake, hawakusita kuendelea kutafuta tiba ya kumtoa mtoto wao katika janga hilo.Walifunga safari hadi Muhimbili ambako alipimwa tena na jibu lilionyesha vilevile.

"Lakini tulipofika Muhimbili baba aliambiwa anaweza kupata tiba ya kuipa nguvu jinsia ya kiume nje ya nchi, akatajiwa nchi zinazotoa tiba hiyo kuwa ni India, China na Korea Kusini, tatizo lilikuwa fedha," anasema

Wakati huo Anti Suzy alikuwa bado yupo shule ya msingi na wazazi wake walipokuja kushtuka, waligundua tayari mtoto wao amekwishaanza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

"Siku wazazi walipogundua walinipiga sana, wakataka nimtaje mtu anayenifanyia huo mchezo lakini nilikataa , wakaamua kuniadhibu kwa kunipeleka mahabusu kumbe huko ndiko walikwenda kuniharibu zaidi," anasema Anti Suzy

Alipotoka jela, Anti Suzy alirudi shule kwa muda mfupi na baada ya kuona mazingira ya nyumbani yanambana zaidi aliamua kutoroka na kuja jijini Dar es Salaam.

"Nilianza maisha ya kujiuza, katika baa, hoteli na kwa kweli maisha yangu hayakuwa ya kupendeza hata kidogo, nilikuwa ni kahaba kabisa" anasema.


Kauli za wataalamu

Akizungumzia tabia kama ya Anti Suzy Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsiawa Wanawake, TGNP, Usu Malya, anasema kuwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja hawana budi kupewa elimu ya kina kuhusu UKIMWI.

Lakini anasema kuwa pamoja na kuwa tabia zao haziwafurahishi wengi katika jamii, siyo vyema kuwaadhibu kwa kuwatukana au kuwapiga.

"Hii ni mifumo katika jamiiinayoruhusu watu kujichukulia sheria mkononi, si kwa jamii ya mashoga peke yao,tusipokuwa makini, ukatili huu utaendelea hata kwa albino, vikongwe, na walemavu wengine," anasema Mallya

Mwanaharakati mwingine mwanaume ambaye hakutaja jina lake lichapishwegazetini anasema suala la ‘mashoga' ni zito na linahitaji hekima kubwa kulichambua.

Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Meshack Shimwale anasema kuwa pamoja na mashoga kuwaudhi watu wengi katika jamii za Afrika, lakini wanahitaji kupewa huduma za afya.

Anasema miongoni mwa viapo vya udaktari ni kumfanya mgonjwa asidhani anawajibika au ana makosa kwa ugonjwa wake aidha kwa kumcheka au kumshangaa.

Kuhusu mashoga kudai wamezaliwa na vichocheo vya jinsia ya kike, Dk Shimwale anasema hakuna ukweli kuhusu hilo.

"Kama wapo waliozaliwa na vichocheo hivyo basi ni mmoja kati ya laki moja. Wengi wamedumu katika hili baada ya kujitengenezea au kutengenezewa mazingira," anasema.

Anasema kuwa ushoga ni miongoni mwa ugonjwa wa mtizamo

(perception disorder), ambao kama mtu akiuendekeza unaweza kudumu maishani mwake.

Anaongeza kuwa, wanaume waliojikuta katika hali hiyo bado wana nafasi ya kupona na kuwa marijali tena.

Profesa Paul Cameron, Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti nchiniMarekani anasema ushoga ni tabia ambayo watu hujifunza na wala si matatizo ya kibaolojia wala ya kurithi.

Anasema utafiti uliofanywa mwaka1983 na taasisi yake ambao uliwahoji mashoga 147, asilimia 35 walisema tabia zao ni za kurithi na zimesababishwa na vichocheo, lakini asilimia 80 katika mashoga wengine 3400, walisema walifundishwa na wenzao mashuleni, nyumbani na watu wanaowazunguka.



SAM.jpg


Haya ndiyo makazi ya Anti Suzy pembezoni mwa mto Msimbazi jijini Dar es Salaam. Picha na Florence Majani
 
Pole zake,maisha yake magumu hasa. Sijui wa kulaumiwa ni nani hapo. Wazazi, yeye mwenyewe au jamii.
 
[h=3]Shoga ‘Aunt Suzy' avamiwa, anusurika kifo[/h]
Aunty Suzy



BAADA ya shoga maarufu jijini Dar es Salaam, Ibrahimu Mohamed ‘Anti Suzy' (25), kutoboa siri kwenye vyombo vya habari jinsi watoto wa kiume wanavyoharibiwa na wanaume na kueleza namna alivyobwagiwa mtoto wa mwaka amtunze, mwanamume aliyembwagia mtoto ameibuka na kumjeruhi kwa visu akitaka kumuua.

Mwanamume huyo mwenye mke, awali alikuwa akiishi na Anti Suzy kama mume na mke eneo la Jangwani, baada ya kumkimbia mkewe na alikorofishana na shoga huyo baada ya kumfanyia fujo na kumuibia.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo jana nyumbani kwake, ‘Anti Suzy' aliyejitangaza kuwa ni muathirika wa Virusi Vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 10 sasa, alisema mwanamume huyo alikuwa akimsumbua warudiane, lakini yeye alikataa na kumtaka aishi na mkewe na kutunza watoto badala ya kumng'ang'ania.

"Nilimwambia simtaki, vituko alivyonifanyia ukiacha kuniletea mtoto wa mwaka na nusu wa kike nimlee hapa nyumbani, alikuwa akinipiga, kunitukana na aliniibia vitu vyangu vyote. Kwanza nilishamwambia nimeathirika na Ukimwi ananifuata nini?" Alihoji shoga huyo.

"Jana (juzi) alinipigia simu akinitaka turidiane nikamwambia asinifuate kwanza nimeshaenda kwenye vyombo vya habari."

Alisema alimwambia hivyo ili asimfuate, lakini baada ya kumweleza hayo, alimvamia nyumbani juzi kati ya saa nne na tano asubuhi akiwa na panga na visu akimtishia kumuua kama hawatarudiana na kama ataendelea kwenda kwenye vyombo vya habari kumuanika mambo yake.

"Nilikimbilia ndani na yeye akanifuata humo, akarusha panga anikate shingoni huku akisema ataniua, nikakwepa, lakini likanijeruhi shingo, kama haitoshi akachukua kisu alichokuwa nacho akanikata vidole.

"Damu ikaanza kutoka nyingi, alivyoona hivyo akanikaba kooni ili aninyonge, majirani waliposikia nakoroma, wakavunja mlango na kuniokoa," alidai Anti Suzy.

Shoga huyo aliyeanza vitendo hivyo akiwa mkoani Mwanza, alisema aliamua yeye na mama mwenye nyumba kwenda Kituo Kidogo cha Polisi Jangwani kutoa taarifa na kupewa hati yenye namba MS/RB/10695/2011.

Alisema baada ya kwenda Polisi, aliandika maelezo na kutoa vielelezo likiwemo panga na kisu alivyovitumia kumjeruhi na aliandikiwa hati ya matibabu (PF3) na kwenda Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.

Polisi katika Kituo cha Jangwani walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini walisema mlalamikaji alijitaja kwa jina la kike ambalo ni Suzana Mohamed na tayari taarifa za suala hilo zimepelekwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa hatua za juu zaidi. Mkuu wa Kituo cha Msimbazi hakuwa tayari kutoa taarifa kuhusu suala hilo.

Aidha, Muuguzi aliyekuwa zamu juzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ambaye hakupenda kutaja jina gazetini, pia alithibitisha kumhudumia mgonjwa, Suzana Mohamed (25) mkazi wa Jangwani aliyejeruhiwa shingo na vidole kwa kukatwa na visu akiwa na PF3.

Mama mwenye nyumba anakoishi ‘Anti Suzy,' Manju Machu maarufu kama Bi Manju, alithibitisha jana kutokea kwa tafrani hiyo iliyosababisha mpangaji wake huyo akimbie kunusuru maisha yake.

"Alikuja hapa huyo mwanamume akamvamia akitaka kumuua, alikuwa na panga na kisu, tuliingilia maana alikuwa anasema lazima amuue, nikasema akimuulia hapa kwangu na mimi nitakuwa matatani, na nchi hii ina sheria, kama una kosa na mtu polisi si ipo? Sisi tulimpeleka huyu Polisi kutoa taarifa" alisema Machu.

Majirani wa Mohamed ‘Anti Suzy' nao walithibitisha jana kushuhudia vurugu hizo na kumshauri shoga huyo kurudi kwao Mwanza ikiwa vitisho vitaendelea.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mohamed alifanya mahojiano na gazeti la Habari Leo na kueleza namna vigogo aliowataja kwa jina la mapedejee wanavyowatumia wao kwa gharama yoyote, wawatafutie watoto wadogo walioko shuleni na mitaani akiwataka wazazi, serikali na jamii kuwa macho na watoto hasa wa kiume.

Aidha, pia aliwaonya wanaume wasimfuate kwa kuwa yeye ni mwathirika wa Ukimwi na kwamba mashoga kama yeye wameathirika na ugonjwa huo. Usikose makala maalumu ya mahojiano ya ana kwa ana baina ya gazeti la Habari Leo na Mohamed "Anti Suzy" katika gazeti hilo keshokutwa Jumatano.
 
huoni kama anaeleza tabu zake ili kuwa "funzo kwa wengine". I'm just sad he was a who.re

p.s. his house is really bad, nlipata huzuni nilipoiona
 
Mshahara wa dhambi ni mauti.
Nawaonea sana huruma hao jamaa wanne walioenda kumbaka.
Magonjwa na mabalaa mengine tunajitakia sisi wenyewe

haina haja ya kuwaonea huruma kwani wali-calculate risk zote halafu wakafanya maamuzi kwenda
 
Huyu shoga nina mashaka anataka kupata umaarufu na akimbie nchi kwa madai ya usalama mdogo wa mashoga

Endelea kuwa na mashaka hivyo hivyo...,
akimbilie nchi gani.....?ashindwe kusema hayo siku zote ndo aje aseme
leo kisa anataka kukimbia nchi

It cost nothing to be Logic in your thinking
 
Pole zake,maisha yake magumu hasa. Sijui wa kulaumiwa ni nani hapo. Wazazi, yeye mwenyewe au jamii.

yaan dume zma lkae ndn na kujpodoa kama mtt wa kke halafu uulze wa kulaumiwa n nan? Hayo ndo maisha alyochagua so ajilaum mwenyewe.
 
Hapo akifa utasikia michango ya mazishi lkn yupo hai badala ya kupitisha mchango wa kumponya na kuponya wengine... Hii ndio tz
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom