BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

jellyFish

JF-Expert Member
Mar 6, 2013
316
127
Naamini watanzania wengi wanajaribu kuota kupata fedha za BIKO. Kwa kifupi mchezo huo hauna uwazi kama watanzania wanavyofikiri. Wakati wa kuchezwa ni watu wachache tu wanakuwepo ambao wanaweza kukubaliana. Hauchezwi wazi kama LOTTO ya Taifa.

Kwa hiyo mshindi wa milioni 20 anaamuliwa na wao. Jana tarehe 13/06/2017 walijichanganya baada ya kumwandikia mmoja wa wachezaji sms iliyoonyesha ameshinda na kilichotakiwa ni huyo mchezaji awasiliane nao kwa maelezo zaidi.

Alipojaribu kuwasiliana nao hawakupatikana au hawakupokea simu na kesho yake mtu mwingine katangazwa mshindi. Ujumbe huo ulisomeka hivi:-

Bado masaa 5 tu ushinde 20M ya kesho JUMATAMU. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0711869823; 0711609097; 0682093176; 0682906929; 0743657569 na 076351126

Swali ni moja tu, kama hajashinda kwanini awasiliane nao? Wangeendelea kusema ''kaza buti'' au bado nafasi 10 za kushinda hadi 1M, cheza kwa mpigo.

Dhulma kama hizi haziwezi kuachwa ziendelee, lazima kifanyike kitu, tena sasa wala sio baadae. Polisi, TAKUKURU hili linawahusu.
 
Nchi nzima imegeuka ya wacheza kamari... wachumi hawajashtuka ni jinsi gani kamari inabomoa kabisa uchumi wa nchi kwa kutengeneza lundo la maskini adicted katika kamari.. kampuni mbalimbali za kamari zinaendelea kuja shamba la bibi kuzoa fedha wa wapenda short cut katika maisha. Ilianza sport betting sasa kila mtaa kuna mashine za kudumbukiza fedha ambazo zamani zilikuwa haziruhusiwi kuwekwa mitaani zaidi ya kwenya makasino,,,, kuna tv kila mtaa michezo ya kukimbiza mbwa hii yote ni hatari kwa nchi.
 
ukiandikiwa bado masaa matano ushinde maana yake umeshashinda? wajuvi tafadhali mnifumbulie fumbo hili
Kwanini aombwe kuwasiliana nao. Kwa taarifa yako mchezo hauchezwi saa sita usiku, unachezwa five hrs before saa sita, hivyo mshindi anaandaliwa kwa kupewa maelezo. wamejichanganya
 
Ile ni programmed but let me mind you one thing if you have an access to the database you can do anything ....
 
Soma vizuri habari. Why should they bother request his call and list down five mobile contacts --what for!!!!

c6e24b0651d824a27e9bac1333496acb.jpg

Kwahi hawa hawajaweka no ya simu?!...
 
Naamini watanzania wengi wanajaribu kuota kupata fedha za BIKO. Kwa kifupi mchezo huo hauna uwazi kama watanzania wanavyofikiri. Wakati wa kuchezwa ni watu wachache tu wanakuwepo ambao wanaweza kukubaliana. Hauchezwi wazi kama LOTTO ya Taifa.

Kwa hiyo mshindi wa milioni 20 anaamuliwa na wao. Jana tarehe 13/06/2017 walijichanganya baada ya kumwandikia mmoja wa wachezaji sms iliyoonyesha ameshinda na kilichotakiwa ni huyo mchezaji awasiliane nao kwa maelezo zaidi.

Alipojaribu kuwasiliana nao hawakupatikana au hawakupokea simu na kesho yake mtu mwingine katangazwa mshindi. Ujumbe huo ulisomeka hivi:-

Bado masaa 5 tu ushinde 20M ya kesho JUMATAMU. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0711869823; 0711609097; 0682093176; 0682906929; 0743657569 na 076351126

Swali ni moja tu, kama hajashinda kwanini awasiliane nao? Wangeendelea kusema ''kaza buti'' au bado nafasi 10 za kushinda hadi 1M, cheza kwa mpigo.

Dhulma kama hizi haziwezi kuachwa ziendelee, lazima kifanyike kitu, tena sasa wala sio baadae. Polisi, TAKUKURU hili linawahusu.
ndugu kiswahili kimekupitia pembeni nn? hakuna palipoandikwa umeshinda hapo
 
Back
Top Bottom