Biharamulo: Jumuhia ya Wazazi CCM yachangia matofari, shule ya wasichana Kagango

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,137
3,323
Katika kuazimisha wiki ya jumuhia ya wazazi CCM, leo wamezindua mchango wao wa tofali elfu moja walioutoa katika shule ya sekondari ya wasichana Kagango. Mgeni rasmi alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya taifa ya jumuhia ya wazazi taifa ndugu Suleimani Juma Kimei aliyemwakilisha mwenyekiti wa Jumuhia ya wazazi CCM Taifa ndugu Abdallah Bulembo ambaye alichelewa kufika wilayani Biharamulo.

Katika hafla hiyo, Jumuhia hiyo imetoa mchango wa matofali elfu moja yenye thamani ya milioni tatu.

Shule ya wasichana Kagango ni shule mpya iliyoanzishwa mwaka huu ambayo imemegwa kutoka shule ya Sekondari Kagango ili kuwezesha mabinti kupata elimu bora zaidi na uangalizi wa hali ya juu.

Hadi sasa shule hiyo ina changamoto nyingi sana kama vile upungufu wa vyumba vya madarasa, vyoo, mabweni, vyumba vya maabara, nyumba za walimu pamoja na upungufu wa walimu wa sayansi na hesabu.

Aidha mgeni rasmi amesisitiza zaidi walimu wa kiume waliopo hapo shuleni kuwa na maadili ambayo yatawazuia kutembea na wanafunzi hao.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na mkuu wa wilaya, mwenyekiti wa halmashauri, afisa elimu sekondari wilaya, mwenyekiti wa CCM wilaya, mwenyekiti wa jumuhia ya wazazi wilaya pamoja na makada wa chama, walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

Zifuatazo ni picha za tukio zima.
IMG_20170406_205330_289.jpg
IMG_20170406_205408_160.jpg
IMG_20170406_205514_101.jpg
IMG_20170406_205559_956.jpg
 
Hao viongozi wa ccm wameongea uongo ili kukwepa aibu.
Kwasababu msaada walio utoa hauendani na hadhi yao.

Hivi kwa Tanzania hii ni tofali gani moja linauzwa sh. 3000?
 
Hao viongozi wa ccm wameongea uongo ili kukwepa aibu.
Kwasababu msaada walio utoa hauendani na hadhi yao.

Hivi kwa Tanzania hii ni tofali gani moja linauzwa sh. 3000?
Alafu ni kweli bhana, hatukuligundua hilo. Japo ni vizuri wamefanya jambo jema pia.
 
Back
Top Bottom