BigBon na uchinjaji mbuzi usiku, nini maanake?

Wapendwa kuna mambo mengine unawezasema ni uchawi lakini sitaki kufika huko
hawa waheshimiwa wa sehemu yaa kuuzia mafuta pale bigbon kariakoo nilisikiaga
wanachinja mbuzi watatu usiku mmoja mweusi,mweupe na mwingine madoa doa
sikutaka kuamini ijumaa nkaita pale usiku nkakuta lundo la watu wana subiri kupewa
nyama ya mbuzi....niliposhuuka na kuanza kudadisi nkaambiwa yale yale sikusita kuwasha
gari na kuondoka nkasema yawezekana Mungu ameamua kuwapitishia neema watanzania
sasa kama wewe unaitaji nyama bure kuanzia kilo 2 nk njoo usiku

swali langu kuleta kwenu hii ni je mtu akila hii nyama ana kosa ama ina madhara???nasikia magodown mengi tu pugu oad wao wanachinjamchana live na kugawa kwa wafanyakazi na damu kumwaga kwenye mageti...anyway sitakikufika zaidi tujulishane kwa hili
Samson wewe utakuwa mwongo na mwenye lengo la kuwaharibia watu. Umetoa shutuma zako Mount Meru Petro Station leo umehamishia BiGBON. Mtu achinje mbuzi watatu ndiyo ukute rundo la watu wakisubiri hiyo nyama? Tuwe wakweli maneno ya uzushi na uchonganishi wala hayafai. Kuna watu wengine wanatamaduni za kuwagawia watu kile ambacho Mungu amewapa. Wengine wanasomesha yatima na wengine hutoa chakula. Sasa mawazo kama haya yamekaa kizushi. Pia samahani kama nitakukwaza, jaribu tafadhali kuangalia unavyoandika uwe unakumbuka na nukta.
 
Kuna m2 humu ndani alikua anaomba ushauri wa kufuga majini. Naamini kufuga majini ni Next stage after this. Nikiwa na maana kwamba hii stage ameshapita. Ningemuomba kama yupo karibu atupe msaada. Leo inaweza kuwa mwisho wangu wa kujaza mafuta pale.
hata mi hiyo post nshawahi kuisoma hapa jamvini
 
Back
Top Bottom