BigBon na uchinjaji mbuzi usiku, nini maanake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BigBon na uchinjaji mbuzi usiku, nini maanake?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 11, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,413
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280
  Wapendwa kuna mambo mengine unawezasema ni uchawi lakini sitaki kufika huko
  hawa waheshimiwa wa sehemu yaa kuuzia mafuta pale bigbon kariakoo nilisikiaga
  wanachinja mbuzi watatu usiku mmoja mweusi,mweupe na mwingine madoa doa
  sikutaka kuamini ijumaa nkaita pale usiku nkakuta lundo la watu wana subiri kupewa
  nyama ya mbuzi....niliposhuuka na kuanza kudadisi nkaambiwa yale yale sikusita kuwasha
  gari na kuondoka nkasema yawezekana Mungu ameamua kuwapitishia neema watanzania
  sasa kama wewe unaitaji nyama bure kuanzia kilo 2 nk njoo usiku

  swali langu kuleta kwenu hii ni je mtu akila hii nyama ana kosa ama ina madhara???nasikia magodown mengi tu pugu oad wao wanachinjamchana live na kugawa kwa wafanyakazi na damu kumwaga kwenye mageti...anyway sitakikufika zaidi tujulishane kwa hili
   
 2. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Kuna m2 humu ndani alikua anaomba ushauri wa kufuga majini. Naamini kufuga majini ni Next stage after this. Nikiwa na maana kwamba hii stage ameshapita. Ningemuomba kama yupo karibu atupe msaada. Leo inaweza kuwa mwisho wangu wa kujaza mafuta pale.
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  SAMSON MFALILA nakuomba usirudie tena kwenda kushuhudia wachawi! maana wakikugundua siku ingine wewe utakuwa kafara yao chunga sana ndugu yangu bado tunakuhitaji
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Ngoja niende ijumaa hii usiku pale BigBon Sinza huenda namimi nikakpata Mbuzi sijui hata hao Waarabu wanawaita ndugu zao wa kiarabu kuja kupata hiyo nyama au ndio wamatumbi tu na ulofa wetu,kisa bure,jamani bure aghali eh shauri yenu
   
 5. s

  sha Senior Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  NDUGU YANGU SAMSON BIBLIA INATUAGIZA "vyakula vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo; chakula ni kwa tumbo na tumbo ni kwa chakula, BALI MSILE CHOCHOTE KILICHITOLEWA SADAKA.UKILA UNASHIRIKI UOVU WAO.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,413
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280

  ni kweli mpendwa ila kuna shemu wanasema viingavyo si najisi najisi vitokavyo inakuwaje ...naomba msaada

  APPOSTEL
  SAM
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Msiende kuchukua hizo nyama za makafara.
  Zina maagano na mashetani na mapepo, sio nzuri kwa afya yako ya imani na ya kimwili pia.
   
 8. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kuwa makini Mtu wa Mungu,hiyo ni ibada ya mashetani na hizo nyama ni kama chakula cha shetani....don't be part of it. kuna maneno au misemo inayoambatana nayo ambayo inadhihirisha kuabudu miungu mingine badala ya Mungu aliye hai yaani YEHOVA.
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hiyo ni nyama a makafara ukila ni dhambi na ww utakuwa umeshiriki ibada ya mashetani epuka
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Si vizuri hata kuzikaribia, around kunakuwa utukufu wa mapepo na mapepo yenyewe hata hao wanaokwenda kuchukua hizo nyama za bure yawezekana si watu ni majini. Ni vyema kuwa waangalifu na yanayotukia pia, si kila kinachotokea lazima ukishuhudie.
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni moja ya mila walizopewa na waganga wao kuwa LAZIMA KUCHINJA HAO MBUZI LASIVYO WATAKUFA PAMOJA NA VIZAZI VYAO VYOTE ama WATAFILISIKA.......Utajiri kazi jamani lol! :decision:
  Nilikuwa napenda kwenda pale kujaza mafuta na kununua gesi kwanzia leo nimekata mguu sikanyagi tena pale
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Post yenyewe hiyo hapo juu.
  Hakika mwanzo wa ngoma ni le le le
   
 13. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  :mad2:VP na mafuta yao tuwasusie, kwani yenyewe hayana kafara?
   
 14. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hahahaha lazima watambike kama wanajua mafuta yao wanayapata kupitia mzee wa giza... hayo ndo malipo wanayotoa na mbaya ni kwamba wanawalisha watu nya hiyo waliyoitoa sadaka mh bila shaka baada ya muda hao walaji huhamishwa kimsukule kwenda kuchimba mafutaaaaa hahahahahah du kazi ipo.
  Jamani mrudieni Mungu maana hizi ni zama za uovu mweeee.
   
 15. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tuchunguze pia na ajali nyingi zinazotokea humu mjini yayo magari/pikipiki zilijazia wapi mafuta!! unaweza kuta hao jamaa wanawatoa hata watu
  muhanga. Tuwe makini.....:eyeroll2:
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,413
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280
  wachungaji wanasema fata ninayosema usifanye ninayotenda sasa sijui tukilamba mafuta yao tunazindika ama??embu wachungaji tusaidien kwa hil rev masanilo tusije ulizwa kwenye ufalme wa baba wa mbinguni
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,413
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280
  tuangalie na risiti zao unaweza kuta maa alama ya free mason mnayajaza kwenye gari kumbe lohhh tanzania
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kheri anae chinja mbuzi kama kafara kuliko anae ua makumi ya watu barabarani.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,413
  Likes Received: 5,682
  Trophy Points: 280

  ni kwelii lakini alaaniwe atumiaye mbuzi kuua watu barabarani
   
 20. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Iwapo mbuzi alikuwa na afya nzuri kabla ya kuchinjwa, haina tabu kumla alimradi mtu ana imani kamili na ulinzi wa Mungu wake. Mashetani /mapepo hayammwezi Mungu
   
Loading...