Big up kwa madaktari 258 furahieni matunda ya ujasiri wenu

Boloyoung

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
682
652
Kwa mujibu wa wataalam wa saikolojia ya mafanikio adui mkubwa wa mafanikio ya binadamu huwa ni hofu na woga wa kuthubutu unaoigubika akili yake. Hili limethibitika katika ujasiri wa madaktari wazalendo ambao pamoja na kujazwa hofu walijitoa kwenda kufanya kazi nchini Kenya bila kujali lolote litakalowapata huko ugenini.

Sasa ona ujasiri na uthubutu wao kwenda Kenya umewafanya waajiriwe na serikali ya Tanzania wakiwaacha wenzao waliojionea huruma na kudhani kujitolea kwenda Kenya ulikuwa ushamba.

FUNZO: Hakuna mafanikio halali ambayo ni lelemama. Ukiendekeza hofu na woga utachelewesha mafanikio yako mwenyewe au kwa lugha nyingine utajikuta wewe ndiye mchawi wa mafanikio yako mwenyewe..

Big up kwa madaktari 258 furahieni matunda ya ujasiri wenu.
 
Ndo maana lazima tukubali kuwa kati yetu kumi wanne wanauhonjwa wa akili.
Una uhakika kama ambao hawakuomba hawana ujasiri na uzalendo???
Utaratibu wa kuomba kazi nchini upoje??
Binafsi nafikiri ni bora wangetangaziwa na wengine waombe hapa kwetu then kipaumbele wangepewa hao
 
safi sana Mbowe aliwajaza hofu kwa sababu ya wivu wake tu kwa sababu hao madaktari watalipwa mshahara mnono kumzidi....Mbowe ana wivu sana
 
Back
Top Bottom