Big results now...nahisi kuna tatizo kubwa sana hapa

Who Cares?

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
3,509
3,353
Wadau salaam,
nimekuwa nikifuatilia hizi slogan za serikali na mbwembwe nyingi ambazo kila nikikaa na kutafakari kwa kina nashindwa kuelewa wanaoziandaa wanakuwa wakifikiria nini hasa.

Hii ya miezi kadhaa iliyopita kiimeibuka kitu kiitwacho big results now (brn), nashawishika kuamini kuwa ni mojawapo ya maazimio na kaulimbiu za kukurupuka pasi na uchunguzi au hata tafakari na tafakuri za kina kabla ya kuiwasilisha kwa hadhira ya watanzania takribani milioni 50 kwa uwingi wetu.

Nikiweka tafsiri rahisi ya kiswahili kwenye kaulimbiu hii naamini wanamaanisha "matokeo makubwa sasa", na kwa maana hii ya kiswahili ndipo misingi na dhima ya ukakasi juu ya hii kaulimbiu nimeijenga....inaeleweka na kuaminika na kila mwanadamu aishiye chini ya jua kuwa "matokeo yoyote huwa ni matunda ya matendo yaliyofanyika"...results zinatokana na actions.

Sasa basi, napenda kuwashauri wabunifu na watunzi wa hii slogan/ kaulimbiu ya big results now..warudi kwenye kazi ya awali ya kujiuliza..hizi results now zinatokana na actions zipi now?..na kama wanaongelea big positive results naamini wanatakiwa pia wafikirie effective actions ili matunda yawe possitive results.

Kama wanadhani itawawia ngumu sana kubadilisha wazo/slogani/kaulimbiu basi wafute maneno mawili ya mwanzo kwenye slogani waliyokwishaipiga mnada kwa wananchi na isomeke "effective actions now"...na waweke wazi hizo action watakazochukuwa na ndani ya muda gani ili muda huo utakapokwisha wananchi tufanye upembuzi/evaluation kujuwa how big was the results of our actions over a certain period of time.

hoja ya big results now..imejengwa katika taswira ya viongozi walio-results oriented bila ya action plans. Na kwa ulimwengu wa sasa watu wanahitaji effective actions and firm plans that will assure the best results...sisi kama wananchi hatuoni wala hatujui hizo actions ni zipi. Siamini kuwa serikali imeamua kuja na hii kaulimbiu ya big results now ili kukidhi kiu ya matokeo ya haraka kwa wanachi wake pasipokuwa mipango ya kuyapata hayo maendeleo/matokeo.

Mie ni mpenzi wa soka na timu ya taifa ya tanzania "taifa stars"..siamini kwa kauli kama hizi za big results now timu itachukuwa kombe la dunia 2018 pasipokuwapo na action plans...serikali itawaridhisha watu kwa slogans ambazo hazina njia sahihi ya kuzitekeleza na itarajie kuwa mambo yatakuwa kama yalivyotamkwa..big results now...naomba ibadilike iwe "effective actions now" na serikali iandae timu mbili za vijana from 14yrs -17yrs na iwekeze billions of money timu zipelekwe nje ya nchi ulaya na soth amerika zikajifunze soka kwa miaka isiyopunguwa mitatu kisha tushiriki michuano tukiwa na timu za vijana wenye 17yrs na 20yrs kisha tuone kama hatutopata hizo "big results na kushiriki world cup"...hii ni mojawapo kati ya maeneo madogo sana ya kuwekeza vitendo na sio maneno.

Ni hoja changanifu kwa wadau wote na wapiga zumari wa bendi ya "big results now"...heshma yako prof. Muhongo.
 

Sometimes

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
4,539
1,122
Jamaa wanachezea maneno ili miaka iende! "Mini Tiger",Kilimo First na "Big result now" ni mwendelezo wa ngonjera hizo!
 

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,915
Kila siku naona warsha, mikutano na makongamano makubwa makubwa kuhusu mikakati mikubwa ya maendeleo. Kitu kinachonishangaza ni kuwa wanaongelea mikakati ya mipango mikubwa wakati bado mahitaji muhimu kabisa ya mwananchi hayajawezwa kutimizwa kwa miaka mingi sasa.
 

Mlayjr

JF-Expert Member
May 7, 2013
418
155
NI UPUUZI KAMA ILIVYO TII SLOGANI YA TII BILA SHURUTI, TATIZO LA VIONGOZI WA CCM upeo wao wa kufikiri ni mdogo, wamejisahau, walafi, they are total evils, KILIMO KWANZA huku wanaagiza mchele kutoka nje ya nchi, wana wa frustrate WAKULIMA WETU, BIG RESULTS zinatokana na utekelezaji wa sera zipi??????? kama sio uongo?????
 

cyrilkomba

Member
Sep 26, 2011
69
27
Tanzanians we are very good in expecting good/big results without proper planning to the expected ending....!!

In addition to what you have said may you please ask them where have we reached to achieve the fyp (2010/11-2015/16 five year plan...?)

naona kama tuna tapatapa tu katika kufukia malengo ya milenia.....Na hii nikuwa tunaona hatujafikia kitu so tunajaribu kutach kila kitu kwa wakati mmoja..... Na kwa haraka.....!!

Hizo brn walikaa wataalamu tena waliobobea na posho walilipwa...
 

Who Cares?

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
3,509
3,353
kila siku naona warsha, mikutano na makongamano makubwa makubwa kuhusu mikakati mikubwa ya maendeleo. Kitu kinachonishangaza ni kuwa wanaongelea mikakati ya mipango mikubwa wakati bado mahitaji muhimu kabisa ya mwananchi hayajawezwa kutimizwa kwa miaka mingi sasa.

ni kati ya vitu vinavyonikera sana hapa nchini kwetu..we talk much n we do nothing and people especially civil servants and decision makers are very busy with per diems and allowances for attending those non-productive seminars and conferences.

Tunahitaji kuwa na accountability ya kila mwajiriwa wa serikali anayehudhuria seminar au conference juu ya kile alichojifunza na kimeleta vipi mabadiliko kwa taasisi anayofanyia kazi na nchi kwa pamoja.

Wapo watumishi wa serikali wao ni kiguu na njia kila siku nje ya nchi na kuzunguka dunia ila hakuna tija kutokana na ziara zao.

Mkukuta, mkurabita, big result now n the likes ni upuuzi mtupu..sorry to say so.
 

kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,681
2,209
Absolutely...expecting results without action plans is a big welcome to defeat..DEAD ON ARRIVAL. POROJO REPUBLIC STATE

Correct! You cannot have big results from 'business as usual'. What is the strategy to these big results? They were supposed to have come out with strategic plans first. They have put themselves infront of the cart. Maisha bora kwa kila Mtz.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Who Cares?

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
3,509
3,353
NI UPUUZI KAMA ILIVYO TII SLOGANI YA TII BILA SHURUTI, TATIZO LA VIONGOZI WA CCM upeo wao wa kufikiri ni mdogo, wamejisahau, walafi, they are total evils, KILIMO KWANZA huku wanaagiza mchele kutoka nje ya nchi, wana wa frustrate WAKULIMA WETU, BIG RESULTS zinatokana na utekelezaji wa sera zipi??????? kama sio uongo?????

kiongozi umenifurahisha sana kiasi nadhani ni wakati wa kulist down slogan/kaulimbiu za kipuuzi na zisizokuwa na tija au hata kueleweka kwa wananchi zilizowahi kutolewa na serikali au hata viongozi wa serikali:-
1- big results now
2-mkurabita
3-mkukuta
4- UTII BILA SHURUTI
5- WAKIANDAMANA PIGENI TUU
6- WANAOUA ALBINO NAO WAUWAWE
7- LIWALO NA LIWE
8-WANAPATA MIMBA SABABU YA VIHEREHERE VYAO
9-HATA TULE NYASI NDEGE NA RADA VITANUNULIWA
10- WATANZANIA WANAWIVU WA KIKE
11- HIVYO NI VIJISENT TUU
12-
13-

WADAU TUENDELEZE LIST HII...
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,522
4,982
Mlolongo wa projekti zisizo na kichwa wala miguu, zipo hasa kutokana na kukosekana kwa dira ya taifa, na pia inaonekana uongozi wetu wa juu hawana appetite na mipango ya muda mrefu sababu ni great man tu ndio anaweza kuthubutu kuanzisha mambo ambayo matokeo yake yataonekana muda mrefu baada ya yeye kuwa hayupo. "simple minds" huwa zinapenda kufanya kitu kionekane hapo hapo. hakuna mambo makubwa ambayo unaweza kuyafanya leo matokeo yake yakaonekana kesho. hiyo siyo chumvi inayokolea mara baada ya kuwekwa. mifano ya projekti kama hizo ni mradi wa shule za kata. jitihada za kweli za kuinua elimu lazima zianzie chini kabisa na ni ziwe endelevu. ili ziwe endelevu, tunahitaji makubaliano ya kitaifa ili isitokee tena akija mwingine akaingia madarakani asitufanyie MUNGAISM. nina maana ya yule waziri wa elimu most controversial, na zile move zake mbovu kabisa.

Kama hakuna will ya kuweka mipango ya muda mrefu na iliyo endelevu, tutaishia kuwekeza kwenye projekti za fasta fasta na matendo ya kulimbukeni yanayoambatana na vitu kama hivyo: kudeki barabara, kupulizia watu dawa ya mbu, nk.
 

kijereshi

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
389
280
Tukijikumbusha malengo ya Vision 2025 na sera nyingine sina hakika kama hata robo tumeweza kuyafikia achilia mbali ufahamu wa viongozi na watendaji kuwa na uelewa wa yaliyomo katika sera hizo na inawezekana kabisa ikawa kila utawala mpya unapoingia unakuja na mambo yake pasipo kuwa na uendelezaji wa mipango ya utawala uliopita kwamba kila anaeingia anakuja na yake na ndio maana katika kipindi cha kampeni huwa kunakuwa na ahadi zisizo na kichwa wala miguu kutoka kwa wanasiasa kila mtu akijaribu kujinadi.Kama nchi tumeshindwa kimfumo kwani mambo mengi yameishia katikati licha ya kutimia rasilimali nyingi kuyaandaa ikiwemo muda,rasilimali watu,fedha et al.Sasa haya ya big results now nadhani ni jamii moja tu hakuna kipya kitakacho patikana zaidi ya kupambwa kwa mbwembwe na ngojera za hapa na pale kama ni mikataba walisatiliana saini sasa sijui kama ndio mchezo wa siasa wenyewe huu maana huyo waziri wa nishati na madini ngonjera zimekuwa nyingi na majigambo kila siku.
 

sansiro12

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
259
57
Tanzanians we are very good in expecting good/big results without proper planning to the expected ending....!!

In addition to what you have said may you please ask them where have we reached to achieve the fyp (2010/11-2015/16 five year plan...?)

naona kama tuna tapatapa tu katika kufukia malengo ya milenia.....Na hii nikuwa tunaona hatujafikia kitu so tunajaribu kutach kila kitu kwa wakati mmoja..... Na kwa haraka.....!!

Hizo brn walikaa wataalamu tena waliobobea na posho walilipwa...
Hakuna Big Results bila kuwa na utekelezaji makini. Mipango mizuri tunayo. Tatizo ni kushindwa kuiteleleza kwa unakini na vitendo endelezevu. Tatizo la Tanzania au viongozi wetu ni kutojiamini au kuwaamini watalaamu wetu na kuwatumia ipasavyo. Tupo wataalamu wengi wenye kujua mengi, lakini hawatumiki ipasavyo. Tanzania tunayo rasilimali nyingi - asilia na watu. Hatujaitumia ipasavyo kuleta maendeleo yetu. Tusigegenee kuwa wageni tu ndio watakuletea maendeleo. Wanaweza tu ku-complement tu mipango wetu kama tutapanga vizuri na kutekeleza vizuri.Tutumie na tujenge rasilimali zetu - asilia na watu. Tuache mambo ya kupeana vyeo bila ujuzi. Tuwape wenye ujuzi na tuwatumie vizuri kuleta maendeleo Tanzania ni tajiri sana kuliko tunavyofikiria. Let work out of the box
 

orthodox

Member
Apr 29, 2012
44
6
Kuna huu mpango wa BRN serikal imeiga kutoka nchi za majuu. Swali ni kwamba kwa nature ya nchi yetu kwa ujumla tutaona mafanikio kwa muda mfup kama wanavyotaka kwel? naomben mawazo yenu wana JF.
 

Sticky

Member
Aug 9, 2014
54
3
Hakuna kitu hapo, BRN imekuja kubeba wanafunzi wote wapate vyeti tu lakn kichwani ZERO BRAIN
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,882
3,736
hakuna kitu hapo, mission failed! BRN means Brain Receive Nothing!

Hakuna kitu hapo ; huyo Issa ni dalali tu anakuja kumchanganya DHAIFU ili wapige fedha za upesi upesi kabla hajaondoka!! Huyu huyu Issa ndio alikuwa dalali wa kutuibia CELTEL toka TTCL!!!!
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom