- Feb 10, 2006
- 4,322
- 13,948
Nimekuwa nikifuatilia Big Brother Africa kwa muda sasa lakini nilichokuja kugundua ni kuwa hili ni shindano moja chafu sana. Halipendezi kuingiwa na mtanzania.
Haya ni mawazo yangu binafsi. Sifurahishwi kabisa na kitendo cha cameras kumulika maeneo ya bafuni wakati wanaume na wanawake wanaoga. Huu ni udhalilishaji ili kupata milioni 100 tu. Binadamu anapoharibiwa utu wake kwa kiwango hiki nashindwa kuelewa nini maana yake kwa Afrika.
Mwanamke heshima yake ni kuficha maziwa yake na nyeti zake. Zinapoanikwa wazi wazi tena kwenye televisheni ni hatari sana. Hii ndiyo maana halisi ya Big Brother Africa? Wale wasiokuwa na Dstv hamwezi kuona ushenzi unaoendelea kwenye jumba hili hadi muoneshwe. Kwa wale wenye kubahatika kuona vema naamini watakubaliana nami kuwa udhalilishaji umezidi kiwango cha kawaida.
Napendekeza waandaaji kuondoa mara moja huu udhalilishaji wa kuonyesha vijana wetu wakiwa uchi na hata kuwahamasisha wengine kutamani kuingia kwenye jumba hili kufanya ufuska kama walivyoonekana kufanya karibuni.
Kwa bahati, tamaduni za nchi zetu Afrika karibia zinaelekeana, hakuna ambako vitendo hivi vinaungwa mkono hata kidogo.