Bifu zito kati ya Ajib na Yondani, washindwa kupeana mkono uwanjani....

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,567
2,000
Ni wakati wa Mechi ya Simba na Yanga leo jumamosi Feb 16,2019.

Tukio limetokea wakati kapteni wa Yanga Ajib anawatambulisha wachezaji wake kwa mgeni rasmi alipofika kwa Yondani akagoma kupokea mkono wa salam kutoka kwa kapten na kukimbilia kuushika mkono wa mgeni rasmi, bahati nzuri tukio limenaswa vizuri sana na Camera za Azam tv.....

Kuna jambo haliko sawa hapa inabidi litaftiwe ufumbuzi mapema sana katika harakat za kuwania ubingwa.

Screenshot_20190216-172434.png
 
Manofu

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
1,311
2,000
Nafikili yondani ana matatizo makubwa kuliko nilivyokuwa namfikilia. Kama issue nikitambaa cha unaodha mbona tatizo sio Ajibu siangeenda kumlalamikia kocha. Hivi anafikili mashabiki wamejenga picha gani pale? Kubwa zima akili matakoni.
 
Patroman

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
647
1,000
Yondani amefanya kitendo cha aibu ukizingatia yy ni mchezaji mzoefu na umuhimu wa mechi, Nadhani Ajibu atakuwa amekwazika sana. Viongozi yanga kazi kwenu.
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
6,998
2,000
Ajibu bado ana mahaba Na Mikia ..mkataba wake ukimalizika arudishwe kwao
.mechi ya NNE ya Derby kiwango ovyo kabisa
 
jogoo_dume

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
2,190
2,000
Nimem
Ni wakati wa Mechi ya Simba na Yanga leo jumamosi Feb 16,2019.

Tukio limetokea wakati kapteni wa Yanga Ajib anawatambulisha wachezaji wake kwa mgeni rasmi alipofika kwa Yondani akagoma kupokea mkono wa salam kutoka kwa kapten na kukimbilia kuushika mkono wa mgeni rasmi, bahati nzuri tukio limenaswa vizuri sana na Camera za Azam tv.....

Kuna jambo haliko sawa hapa inabidi litaftiwe ufumbuzi mapema sana katika harakat za kuwania ubingwa.

View attachment 1024211
Nimemshangaa sana yondani, uzoefu wote bado anaonyesha kabisa in public utoto wake.
 
MAGO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,172
2,000
Yondani ana mambo ya kizamani aka ushamba.. mnaweza kuwa na bifu sawa ila kumkaushia teammate kwa mech kama hii mbele ya waziri ni uzuzu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,567
2,000
Ajibu hajielewi, sasa hapo alikua anasalimia au anatambulisha wachezaji? Mi naona Yondani alikua sawa, Ajibu majukum yake hayatambui kama Captain. Hadi kumpokea Mwakyembe alishituliwa na Karia
Sheria gani inakataza kapten asiwashike mkono wachezaji wenzake wakati wa kuwatambulisha?
 
sweetlee

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
4,047
2,000
Yondani hana akili kabisa

I'm the girl from nowhere,... the one no one will miss .... that's why they choose me...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom