Bidhaa zaanza kupanda bei Kariakoo

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
15,990
35,670
Bila ubishi kwa miaka kama kumi Kariakoo ilijipatia umaarufu kwa biashara hususani nguo, maduka yaliota kama uyoga, wafanyabiashara kutoka nchi jirani walikuja kufuata mzigo Kariakoo.

Siri kubwa kuna kampuni ilikuwa inawaletea mizigo toka china kwa bei ya kutupa, sasa tangu kampuni hiyo ijifanye imekufa na bandarini kukomaa na kodi, bei ya bidhaa hususan nguo zimepanda sana. Je huu ndio mwisho wa umaarufu wa Kariakoo?
 
Wajiandae kulipa kabla siku 7 hazijaisha vinginevyo sheria itachukua mkondo wake,mara mana hakuna jinsi sasa eenhh!
 
Hakuna Dhambi Kuleta Kontena Bandarini, Na Wengi Wanaleta Bakhresa, Zakaria, Mohamed Enterprises Nk Sio Dhambi HSC Kuleta.
Pili Nijuavyo HSC Walikuwa Wakombozi Wa Wafanyabiashara Wadogo Wadogo.
Zamani Watanzania Wakienda China Tafuta Bidhaa Wanakaa Hata Mwezi Hotelini Ili Atafute MTU wa Kujaza Kontena Ndio Aondoke Kurudi Tanzania Anatumia Pesa Nyingi Kwa Malazi Na Chakula.
HSC Walianzisha Kampuni CHINA Na Warehouses Kusaidia Watanzania Wenzao Walikuwa Wakifika China Tu Wananunua Mzigo Receipts Wanapeleka HSC, HSC wanafuata Mizigo Wenyewe Dukani Wanahifadhi Katika Godown Yao Wanakubaliana Bei Na Mteja ya Kusafirisha Mpaka Nchini.
Mteja Anaondoka Immediately BAADA ya Kununua Mzigo Na Kurudi Tanzania ANAOKOA FEDHA AMBAZO ZAMANI ANGEKAA HOTELINI KUSUBIRI MELI NA MTU WA KUSAFIRISHA MZIGO WENGI NI WAFANYABIASHARA WADOGO WENYE MITAJI MIDOGI SANA KATONI 10,7,Nk Wanachanga Kontena Moja Watu Hata 40.
HSC Kwa Pesa Zao Wanakodi Kontena Na Kulipia Freight Ya MELI Mpk Bandari ya DAR.
Wanateja Wanachofanya Ni Kuwalipa HSC Gharama Za Usafirishaji Na Faida Kidogo Katika Waliyokubaliana Kwa HIARI.
Shida Ipo Wapi???
WAFANYABIASHARA NI MASHUHUDA WA HSC ILIVYOWASAIDIA.
 
Nadhani wafanya biashara wataleta bidhaa zenye ubora kutoka na mianya ya kodi kutiwa kufuli, tbs inahitajika kusafishwa
 
Mbona kila kitu kimepanda, mafuta ya kupikia, nyama, maji etc. Huu mpango wa elimu bure utaliza wengi. Subirini tu. Muda mchache mtaanza kulia.
 
Nalitonesa jipu: HSC

HSC haijawahi kujishughulisha na utoaji bidhaa bandarini. Na hiyo kampuni umeyeyushwa ili kugawana mali na sasa mali hizo zimegawanywa kwa wabia abao wote ni ndugu na kila mmoja anajishughulisha na mali zake za mgawanyo na maduka yamefunguliwa kwa majina mengine na wanachapa kazi kama kawaida.

Wamefikia hatua ya kugawana mali kwa kuwa watoto zao wameshakuwa wakubwa na kuna uhai na kifo, na binaadam hakuna ajijuae, wamefanya hivyo kuepusha mitafaruku inayoweza kujitokeza kifamilia kwani mali zimekuwa nyingi na wabia wameshakuwa na watoto wengi na kila mmoja ana uwezo wa kutazama mali zake na wanawe.
 
HSC inamilikiwa na Nani?
Mbona si tumenyweshwa uji kuwa Rizione ndie mmliki
 
Faiza Foxy hebu tuweke unazi na ushabiki kando, tuko wengi tumepitisha makontena kupitia huyu banana, tunakiri makosa ni tamaa tu ya utajiri.
 
Bora tuishi kwa kulipia kodi wote sio kwa baadhi huku wengine hawalipi.
 
HSC inamilikiwa na Nani?
Mbona si tumenyweshwa uji kuwa Rizione ndie mmliki

Wewe huwajui bavicha? Wanavumisha kila uongo ili mradi wapakazie tu.

Ndiyo maana wakaswekwa ndani branch ya vitengo vyao vya uongo wa mitandaoni.

Uliza muongo maarufu wa mitandaoni anaejiita Yericko Nyerere yuko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom