Bidhaa za viwandani zinapanda bei kwa kasi, mazao ya wakulima yanashuka Bei, hujuma hizi

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Mfuko wa cement unauzwa 1900 na 23000 kutoka 12000-14000 mwaka 2015, hujuma

Sukari haishuki 26000

Mafuta ya kula lita tano ya Alzeti 30,000 kutoka 14000 mwaka 2015

Mafuta ya magari nayo yanakimbilia huko juu sijui Kuna Nini

Vifaa vya ujenzi vimepanda zaidi ya nusu Bei kuanzia mwaka Jana.

Haya yanatokea huku Too nazo zikiwa juu na tukiaminishwa kwamba tunajenga nchi lazima tuumie. Wakati tukiumia hao mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya, wabunge na Wakurugenzi kila mmoja analishwa, analipiwa nyumba, analipiwa vocha na kugharamiwa usafiri.

Lakini pia tukumbuke Hawa wanasiasa ni wanahisa kwenye viwanda vya sukari, nondo, cement na pia niwamiliki wa viwanda vya kuchujia mafuta hivyo kupanda Bei kwa bidhaa hizi kwao ni neema.

Wakati bidhaa hizi zikipanda hakuna zao ambalo tunaambiwa Bei imepanda nakunufaisha wakulima, badala yake serikali imefunga mipaka na Kuchukua fedha kununua mahindi kwa wakulima Jambo ambalo kwa serikali ilivyo haitatoa bei nafuu bali itayakomba mahindi kwa wakulima nakuyafungia ndani Jambo ambalo litasababisha mahindi kuadimika na automatically Bei kupanda. Tukumbuke wakati Bei inapanda mkulima hatokoa na chakula ndani hivyo atalazimika kwenda kununua mahindi aidha imported au kwa walanguzi. Kwanini tusiwe na serikali inayotafuta soko ndani na nje na hivyo kuifanya Bei kutabirika?

Wanaohujumu wananchi ni wanaolipwa na wananchi.....kilio kiendelee
 
Umenikumbusha poem moja inaitwa "Building the nation", ikiwabainisha viongozi wa serikali wakitumbua, kula na huhemewa wakati mwananchi hoe hae anaugua ulcers kwa kukosa mlo na kuzongwa shida kibao. Kibaya zaidi hawa wote wana deni la kushirikiana kuijenga nchi. Vitu kama hivi ndo upelekea hata mapinduzi ama ya kiraia ama ya kijeshi endapo kama hakutafutwi suruhu ya haraka sana ..mfano mzuri ni mapinduzi ya ufaransa na hivi juzi pale Guinea, Tz sie bado tupo tupo tu hatujielewi
 
Mfuko wa cement unauzwa 1900 na 23000 kutoka 12000-14000 mwaka 2015, hujuma

Sukari haishuki 26000

Mafuta ya kula lita tano ya Alzeti 30,000 kutoka 14000 mwaka 2015

Mafuta ya magari nayo yanakimbilia huko juu sijui Kuna Nini

Vifaa vya ujenzi vimepanda zaidi ya nusu Bei kuanzia mwaka Jana.

Haya yanatokea huku Too nazo zikiwa juu na tukiaminishwa kwamba tunajenga nchi lazima tuumie. Wakati tukiumia hao mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya, wabunge na Wakurugenzi kila mmoja analishwa, analipiwa nyumba, analipiwa vocha na kugharamiwa usafiri.

Lakini pia tukumbuke Hawa wanasiasa ni wanahisa kwenye viwanda vya sukari, nondo, cement na pia niwamiliki wa viwanda vya kuchujia mafuta hivyo kupanda Bei kwa bidhaa hizi kwao ni neema.

Wakati bidhaa hizi zikipanda hakuna zao ambalo tunaambiwa Bei imepanda nakunufaisha wakulima, badala yake serikali imefunga mipaka na Kuchukua fedha kununua mahindi kwa wakulima Jambo ambalo kwa serikali ilivyo haitatoa bei nafuu bali itayakomba mahindi kwa wakulima nakuyafungia ndani Jambo ambalo litasababisha mahindi kuadimika na automatically Bei kupanda. Tukumbuke wakati Bei inapanda mkulima hatokoa na chakula ndani hivyo atalazimika kwenda kununua mahindi aidha imported au kwa walanguzi. Kwanini tusiwe na serikali inayotafuta soko ndani na nje na hivyo kuifanya Bei kutabirika?

Wanaohujumu wananchi ni wanaolipwa na wananchi.....kilio kiendelee
Mama anashughulikia uchumi kwanza…
 
Back
Top Bottom