Bidhaa kutoka Zanzibar ni nafuu zaidi kuliko hapa Tanganyika kwanini

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,421
Habari wakuu?

nimeliweka hili kwenu tuweze kulijadili kwamapana yake bidhaa mafano Mafuta, ya kula na Sukari zinapatika kwa bei nafuu kuliko hapa Tanganyika viwanda vyetu vya hapa Tanganyika wanapata wapi ugumu wakuzalisha hizi bidhaa Hadi bei iwe juu zaidi kuliko Zanzibar wakati kule hawana viwanda wanatumia kuagiza kutoka nnje



Na kwanini Serkali ya Tanganyika wanapiga marufuku bidhaa hizi zisivuke kuangia huku kwetu wakati bei ingekua cheap zaidi na ingetoa hafueni





100_2873.JPG


Wafanya biashara wahizi bidhaa wanapata wakati mgumu sana kutokana na maslahi yao wanachukua kama bidha haramu kutoka Zanzibar nawakikamtwa namamlaka zatanganyika wanapigwa faini au kuchomwa Moto nakutiwa hasara


Kwanini hili linaendelea kutokea wakati hii nnchi moja inatwa Tanzania kwanini wasiache competition yakibiashara ili watumiaji wanufaike na unafuu wabei
 
Bidhaa nyingi Zanzibar huingizwa kutoka uarabuni hasa Dubai na Oman na kwa uhakika kodi hua ipo chini sana kwa Zanzibar, kwa mfano mafuta ya Alizeti kusafirisha hadi yanafika Tanzania yanakua na bei ndogo sana kuliko haya ya kwetu.
 
Mfumo wao wa kodi halafu huku Tanzania bara kuna ujinga wa kusema tunalinda bidhaa za ndani mfano saruji toka Pakistan mpaka ifike hapa ni bei rahisi pamoja na kwamba kuna gharama za usafiri wakati teknologia ni ileile.
Sukari ya malawi ukiingiza hapa bei.ni ndogo kulinhanisha na hii ya kwetu
 
Vitu vinavyofanya Bei ipande au ishuke ni:-
1. Kodi
2. Demands
3. Gharama za uzalishaji
N.k

Nafikiri tunatofautiana pakubwa na Zanzibar Katika hvyo vtu viwili kodi na demands.
 
Back
Top Bottom