Bidhaa kutoka nje ya nchi kuwekwa alama maalum za utambuzi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
6ed83d7ed3c5d405de96ccf6d0e3cdb5.jpg


Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ipo katika hatua za mwisho za kuandaa mpango maalum wa kupima, na kutambua na kuziwekea alama ya ubora bidhaa zinazoingia nchini, lengo likiwa ni kuondokana na athari zinazotokana na matumizi ya bidhaa hizo ikiwa hazikudhibitishwa

Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka wizara hiyo Bw. Christopher Nassari amefahamisha mpango huo katika hafla ya kutoa leseni za Ubora kwa bidhaa 96 ambazo uzalishaji wake umekidhi matakwa ya viwango

Amesema Mpango huo pia unalenga kuzitambua bidhaa za nje katika suala zima la ulipaji kodi ya mapato ya Serikali na kudhibiti mianya ya uingizwaji holela wa bidhaa zisizokuwa na ubora katika Masoko ya hapa nchini

Ili kufanikisha mpango huo shirika la Viwango Tanzania TBS limeanzisha kitengo maalum cha upimaji wa bidhaa hizo na kuziweka alama maalum ya utambuzi.

Chanzo: Channel Ten
 
Back
Top Bottom