Tulizungumza sana wakati wa uchaguzi kwamba CCM inachukua pesa kutoka kwa wafanya biashara iwe kwa mtindo wa kuchangia (kinafiki) au kwa kulazimishwa (kutishwa). Katika hali hii tulitazamia kuona bidhaa zinapanda bei ikiwa ni njia ya watu hawa kurejesha pesa zao walizotoa kwa ajili ya kampeni za CCM. Kitendawili hiki kimeteguliwa baada ya bidhaa mbalimbali kutangazwa kupanda bei katikati ya wiki iliyopita. Songea mfuko wa sementi unadaiwa kupanda kutoka 14,000/= hadi 18,500/=; Da es Salaam sementi ni 13,500/= kutoka 12,500/=. Kilo ya ngano sasa ni 1,000/= kutoka 800/=.
Katika hali hii, je, tutafika?
Katika hali hii, je, tutafika?