Bidhaa 20 za Sayansi na Teknologia kutoka Iran zasajiliwa Kenya

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Bidhaa 20 za sayansi na teknolojia kutoka Iran zasajiliwa Kenya

Bidhaa 20 za sekta za sayansi na teknolojia kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimesajiliwa nchini Kenya na hivyo zinaweza kuuzwa katika soko la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Sayansi bidhaa hizo zinapatikana katika Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Iran (IHIT) mjini Nairobi.

Kituo hicho kilizinduliwa mwezi Januari mwaka huu wakati Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia, Dakta Sorena Sattari alipotembelea Kenya.

Tokea kituo hicho kifunguliwe hadi sasa bidhaa 20 za uga wa sayansi na tekonolojia ambazo zimetengenezwa Iran zimesajiliwa na sasa zinapatikana katika soko la Kenya na zinaweza kuuzwa pia katika nchi jirani. Baadhi ya vifaa vilivyosajiliwa ni vile vinavyotumika katika chumba cha wagonjwa mahututi, vipima joto, mavazi maalumu ya hospitali n.k. Hadi sasa bidhaa zenye thamani ya dola 70 elfu za sayansi na teknolojia zimetumwa Kenya tangu kituo hicho kifunguliwe. Aidha baada ya wiki kadhaa shehena ya bidhaa za Iran za kukabiliana na corona zinatazamiwa kuwasili nchini Kenya.

[https://media]Balozi wa Iran nchini Kenya Dkt. Jaafar Barmaki (kushoto) akiwa katika Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Iran (IHIT) mjini Nairobi

Mwezi uliopita ujumbe wa ngazi za juu wa wadau wa sekta ya sayansi na teknolojia nchini Kenya ulikuwa safarini katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika sekta hiyo.

Ujumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mashirika ya sekta ya sayansi na teknolojia nchini Iran mbali na kutembelea mashirika kadhaa. Mazungumzo baina ya ujumbe wa Kenya na wenzao wa Iran yalihusu ununuzi wa bidhaa na huduma baina ya pande mbili. Hali kadhalika mazungumzo hayo yalijikita katika uwekezaji wa sekta za mashine na bidhaa za kilimo.

Safari ya ujumbe huo wa wawakilishi wa sekta ya teknolojia kutoka Kenya ilitimia katika fremu ya utekelezaji wa mapatano yaliyofikiwa katika safari ya Dkt. Sattari nchini Kenya.

4bxxab350c82371t27q_800C450.jpg
 
View attachment 1840569
Kumbe waajemi wanaandika kimalkia
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom