Biden azidi kupungukiwa na fahamu, mara hii amepotea njia ya kuelekea ofisini kwake White House!

Ni punguani peke yake ndiye anaweza kulinganisha Marais na upupu.Tanzania ina Rais au ina upupu?Rais gani ambae anashindwa hata kutoa muongozo wa maziko ya watu wanaokufa kwa Corona?Wewe unaona kuna Rais hapo?Ule ni upupu!
Kumbe hamna msimamo. Mara hii mnamgeuka kipenzi chenu? Hii ni ajabu
 
Kumbe hamna msimamo. Mara hii mnamgeuka kipenzi chenu? Hii ni ajabu
Kipenzi chetu kipi hicho?Wapi niliwahi kusema kuwa Samia ni kipenzi changu?Mimi nilianza kumpinga Samia kabla hata hajaapishwa kwa sababu alishirikiana na Magufuli katika kufanya uhalifu dhidi ya binadamu.
 
Cha ajabu kipo sana tu kama taasisi hazipo imara.Unajua Rais ni mtu ambae akili yake inatakiwa kuwa fit sana.Uzee mwingi na Urais haviendani kabisa kwa sababu vyote viwili huwa vinakula sana akili lakini kwa kuwa Marekani ina taasisi imara hakutakuwa na shida yoyote.

Jambo kama hilo likitokea katika nchi za Afrika kama vile Tanzania ambapo Rais ndiye bunge,ndiye mahakama,ndiye polisi,ndiye TISS,ndiye mawaziri na kadhalika ni hatari sana kwa usalama wa nchi na ustawi wake.
Yaani mkuu kwa katiba yetu hii siku tukipata rais kama sabaya au makonda, hata ccm wenyewe watalia na kusaga meno, hamna atakayebaki salama, mfano mdogo tumeonjeshwa na JPM
 
Kuna binadamu watasema Trump anamroga Biden...

Biden ukiachilia mbali na umri mkubwa aliokua nao, ila pia hilo tatizo la kuchanganya mambo alikua nalo kitambo sana...
 
ana stress nyingi Sana huyu mzee,hasa baada ya urusi kumtia tumbo joto vya kutosha,Ukraine inachukuliwa na Hana Cha kufanya .kaweka vikwazo halafu ,urusi Wala haiumii badala yake yeye ndo anayeumia na Asia pamoja na NATO yake.akisikia Russia mwez dec.inazindua mpango wa kuisaidia Africa,tumbo lina muunguruma .kupotea njia lazima kwa stress alizonazo.ndio maana majuzi Obama alimuita Biden ni makamu wake .
 
Rais Joe Biden wa Marekani ameendelea kuonyesha kuwa, mbali na kuboronga katika uzungumzaji, anazidi kupungukiwa na fahamu pia baada ya kupotea njia ya kuelekea ofisini kwake katika Ikulu ya White House.

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, akiwa kwenye uwanja wa Ikulu ya White House, Biden alipotea njia na kuhitaji kuongozwa kuelekea ofisini kwake na afisa wake mmoja wa siri.

Tukio hilo la siku ya Jumatano limejiri katika hali ambayo, kuendelea kuboronga katika uzungumzaji, kupungukiwa na fahamu na kufanya vitendo vya ajabu ajabu pamoja na hali ya ubabaikaji ambayo ameonyesha kuwa nayo rais huyo wa Marekani kwa miezi kadhaa sasa tangu alipoingia madarakani, vimepelekea watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Magharibi kutoa maoni ya kumdhihaki na kumfanyia stihzai kiongozi huyo huku wakosoaji wake wakitilia shaka ufahamu wake na uzima wake wa akili.

[https://media]Joe Biden

Video mbali mbali zinazomuonyesha Joe Biden akiboronga katika uzungumzaji tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani, ikiwemo kuyasahau majina ya maafisa wa serikali yake katika vikao na waandishi wa habari, zimezidi kutilia nguvu shaka iliyopo kuhusu uwezo wa kiakili na kimwili wa kiongozi huyo.

Katika kikao chake cha kwanza na waandishi wa habari, Joe Biden alilitaja kimakosa jina la rais wa Afghanistan alipolitamka 'Kiyani' badala ya Ashraf Ghani...

View attachment 1892180
Kwani Baraka Obama unajuwa alivyotamka neno Tanzania na baadhi ya maneno ya kiswahili alivyokuja kipindi kile? hayo majina ya Afghanistan hata wewe ufundishwe wiki nzima hutalitamka linavyotakiwa ni magumu sana kutamka kwa wasiokuwa waislamu
 
Cha ajabu kipo sana tu kama taasisi hazipo imara.Unajua Rais ni mtu ambae akili yake inatakiwa kuwa fit sana.Uzee mwingi na Urais haviendani kabisa kwa sababu vyote viwili huwa vinakula sana akili lakini kwa kuwa Marekani ina taasisi imara hakutakuwa na shida yoyote.

Jambo kama hilo likitokea katika nchi za Afrika kama vile Tanzania ambapo Rais ndiye bunge,ndiye mahakama,ndiye polisi,ndiye TISS,ndiye mawaziri na kadhalika ni hatari sana kwa usalama wa nchi na ustawi wake.

Litokee mara ngapi?
 
Juzi alipeana mkono na kivuli,sjui ilikuwaje wamarekani wakachagua huyu mzee
Wamarekani wanaomba yasije kuwakuta kama yaliyotukuta Tanzania Biden akafa yule mama akachukua nchi kwani wanajua madhara ya mwanamke kua kichwa cha nchi.
 
Back
Top Bottom