BIBLIA noma!!!!

akashube

JF-Expert Member
Dec 24, 2009
401
23
Enzi nikiwa naishi Manzese ndipo nilipojifunza kuwa Biblia ni kiboko. Sikuzote tulikuwa tunadhibiti panya bila matatizo, na walipokuwa wakitokea nyumba za jirani bado tulikuwa na sumu ya panya na mitego ya panya na hakukuwa na tatizo kuwadhibiti.

Siku moja usiku mchuzi ulidondokea kwenye biblia na tukawa tumeiacha chini bila kuiokota lakini ikiwa kwenye hali mbaya kwa kulowa na mchuzi. Tulipoamka asubuhi yake tukakuta biblia imeliwa karibu robo tatu. Tangu hapo hatukuweza kukamata panya tena na ilibidi tuuze nyumba kuwakimbia panya.

Mambo yenyewe yalikuwa hivi:

Kuna siku panya waliingia kupitia chini ya geti na nilipotoka na rungu kuwafukuza nikasikia wakisema 'kila mtakapopakanyaga nimewapa'. Nilikasirika nikarusha rungu nikamkosa yule panya akakaa pembeni akakunja nne akasema 'no weapon formed against me shall prosper'.

Baada ya siku mbili nikaweka mtego mkubwa na badala yake nikakuta kuku wetu wa mayai kanasa halafu wakati najaribu kutoa mzoga wake nikasikia panya anaimba 'shimo wamenichimbia mie watatumbukia wenyewe humo'...halafu panya wengine wanajibu.

Mwishowe nikaamua kufuga paka, siku iliyofuata usiku nikashangaa paka anafukuzwa na panya mkubwa (fuko) halafu panya ambaye nahisi ndiye aliyekula biblia akasema 'aliye ndani yetu ni mkuu kuliko aliye nje'.

Mwisho tukaamua kuhama nyumba...siku tunahama kila mtu alihamia anakokujua yeye, na wakati naondoka nikasikia yule panya aliyekula biblia anasema 'Adui zako watakujia kwa njia moja lakini watakimbia kwa njia saba'.

BIBLIA NOMA!!!
 
bora ungetumia mfano wa kitu kingine but not bible.nitashangaa kina mods wakiiacha
 
nadhani panya walikua wakisimama kwa ujasiri mbele yenu kwasababu kila siku ya ilitanguliwa na neno kuu kwao kwamba USIOGOPE
 
bora ungetumia mfano wa kitu kingine but not bible.nitashangaa kina mods wakiiacha

Jamani, I think its about time watu tuwe tunaelewa maana ya haya majukwaa. Hili ni Jukwaa la Utani, so chochote kilichopo ni utani usichukulie serious ki hivyo, utapasuka bureeeee.........

Umenifurahisha sana uliyeleta mada, unaonekana kirietivu kidogo
 
Lazima watu wajue aina ya utani wanaoleta. Tunashukuru ni uhusu bible kingekuwa kitabu kingine ingekuwa shughuli hapa lazima utani uambatane na heshima. Angetaniwa mzazi wako ungejisikiaje?
:A S angry:
 
As long as ni utani, mimi nipo very okey, si mzazi tu hata ukinitania mimi mwenyewe. Jamani, hakuna kitu kinachofaa kutaniwa na kisichofaa kutaniwa, ninaesema hivi ni muumini wa hii bible ambayo huyu ametumia ku'create utani, ni uelewa wa mtu tu unahitajika, utani always utabaki utani, unless huyu mtu angeweka hili kwenye jukwaa la dini, hapo hata mimi ningechangia tofauti.

But this is utani man, you dnt have to be serious, infact mimi jukwaa hili ndilo la kwanza kuingia always ili niweze kucheka, so its helpful, kama mtu hapendi utani na haelewi maana ya utani, namshauri asiwe anaingia jukwaa hili, atuachie sisi tunaoelewa maana ya utani,,,,,
 
Kashfa kama izi zipo nyingi wala wee si wa kwanza kusema upuuzi kama huu. Angalia jaman mambo ya kaizari mpe kaizari na mungu pia.
 
Kama umeona haikufai IPOTEZEE TU MKUU SI LAZIMA UCHANGIE
Hivi mtu haruhusiwi kutofautiana na maoni yako??!!!!!!!!!! Watu wengine mnashangaza sana unajua.........Jibu swali wat is the point mimi pia bado sijapata point ya huyu bwana.
 
Hivi mtu haruhusiwi kutofautiana na maoni yako??!!!!!!!!!! Watu wengine mnashangaza sana unajua.........Jibu swali wat is the point mimi pia bado sijapata point ya huyu bwana.

Niliposoma maandishi yako ilibidi niende kumuuliza yule panya kule Manzese, kwa sababu niliona si vema kumjibia wakati sio mimi niliekula biblia.

Nikamuuliza 'whats the point? , yule panya akanitazama kwa kujiamini sana kisha akaniuliza, ni swali lako au kuna mtu unamuulizia ili ukampe jibu?...Nikamwambia kuna mtu anaitwa Da Womanizer.

Akaniambia rudia hilo jina tafadhali...nikajibu Da Womanizer.

Akaniambia mwambie Da Womanizer asome Biblia Isaya 4:1 kwa ajili ya jina lake ndipo atajua 'what the point is'.
 
hahahaha haya mkuu nimekusoma
 
Back
Top Bottom