zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 18,892
- 28,482
Habari za jioni wana JF leo nina mada sensitive kidogo ila ni muhimu sisi waafrika tujifunze mambo haya ili tuweze kufahamu historia yetu na wapi tunaelekea ila nahitaji utulivu unaposoma ili ujifunze kitu na ningeomba pia tusikashifiane kidini maana sio lengo la uzi huu, nashukuru kwa ushirikiano wenu.
UTANGULIZI
Tukirudi nyuma marekani mwaka 1619, ambapo ulikuwa mwanzo wa karne mbili za wanadamu wa jamii ya Negroid yaani ngozi nyeusi kutoka bara la Afrika kutumikishwa kwenye mashamba na makazi ya wazungu lakini cha kushangaza zaidi na kinachoumiza zaidi ni kwamba uhuni huu ulipewa support kubwa na viongozi wa dini na makanisa ya huko marekani sio tu madhabahuni bali pia madarasani.
Kwa mfano kati ya miaka 1700 mchungaji William Graham alikuwa anakaribishwa kwenye vyuo mbalimbali huko Washington hasa siku za mahafali ili kuwaeleza umuhimu wa biashara ya utumwa na mbaya zaidi alitumia biblia kuhalalisha hilo.
BIBLIA INASEMAJE??
TITO 2
9 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,
10 wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote.
EFESO 6:5
5 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
Walawi 25:44
44 Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi.
45 Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.
Kutoka 21:20
20 Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa.
21 Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake
SABATO
Hata wakati ukoloni ukichachamaa huko America Nabii wa kisabato Hellen G White alionyesha wazi kusupport ukoloni wa watu weusi kwa kutumia Biblia hata kwenye mkusanyiko wa maandiko yake yaliyoitwa selected messages (Book 2) Hellen alisema "Kusiwepo na muingiliano wa ndoa kati ya weupe na watu weusi". Na akaenda mbali zaidi na kusema watu weusi wasijaribu kujiweka daraja moja na weupe sababu wao ni watumwa hivyo kibiblia hawawezi kuwa level moja na Bwana wao (wazungu) hapa nanukuu kutoka kitabu cha Testimonies volume ya 9
"The Colored People should not urge that they be placed on an equality with White People."
UKATOLIKI
Wakatoliki nao hawakuwa nyuma kwenye kutumia biblia kuhalalisha ukoloni, tokea mwaka 1517, hata Askofu mmoja aitwaye Las Casas wa uingereza aliagiza meli yenye watumwa kutoka Afrika na ombi lake likakubaliwa na mfalme Charles wa 5. Kibaya zaidi hata mapadre wa kikatoliki maarufu kama Capuchin missionaries walifungiwa na kanisa katoliki baada ya kudai watumwa wapandishwe hadhi huko marekani. Hata waasisi wa mwanzo wa kaniasa kina St.Augustine kwenye maandiko yake alisema utumwa ni taasisi iliyotokana na Mungu hivyo ni faida kwa mtumwa na Bwana wake. Na hata uongozi wa juu kabisa wa kanisa yaani ofisi ya Papa walisupport utumwa mfano Papa Martin 1 mwaka 650 AD alitoa waraka kuagiza kutimuliwa kanisani kwa viongozi wowote watakaofundisha watumwa kujikomboa ama kupinga ukoloni?? Na mafundisho haya walitumia vifungu hivi vya Biblia kuhalalisha.
HOJA
1.Sasa basi mie najiuliza swali moja kama Mungu alituumba wote kwa usawa kwanini basi kuna wanadamu wanahesabika ni daraja la pili hadi aruhusu wauzwe na kununuliwa kama bidhaa na kuwa mali ya mtu milele?
2. Kama utumwa ni halali kibiblia je ina maana wote waliopinga utumwa na ubaguzi wa rangi hapa duniani wote wamefanya dhambi hivyo wataishia kuzimu?
3. Je msimamo wa kanisa wa sasa kupinga utumwa haukinzani na mafundisho ya biblia juu ya kuhalalisha biashara hii ambayo wanaiita haramu kwa sasa??
HITIMISHO
Huenda Biblia ilitumia muktadha wa kipindi hicho kuelezea suala hili la utumwa ila viongozi wa kanisa wakayatafsiri vibaya maandiko haya kwa maslahi yao ila ningependa tufahamishane kuhusu suala hili kama lina baraka za biblia kweli au viongozi wa kanisa walidanganya wao kama wao kwa sababu zao binafsi??
Naomba kuwasilisha