Bibi wa Miaka 75 Auza Picha zake za Ngono ili Kuganga Njaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi wa Miaka 75 Auza Picha zake za Ngono ili Kuganga Njaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Oct 13, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>


  Bibi Marianne L.
  Tuesday, October 13, 2009 2:30 AM
  Bibi mwenye umri wa miaka 75 wa nchini Ujerumani amelazimika kuuza picha zake za utupu alizopiga akiwa kijana ili aweze kupata pesa za kuganga njaa na kulipia bili zake.


  Bibi Marianne L. mwenye umri wa miaka 75 mkazi wa mji wa Berlin, Ujerumani alichukua uamuzi wa kuziuza picha zake za utupu baada ya vibaka kumuibia vitu vyake vyote muhimu na kuamuacha akitaabika na pesa kidogo za kiinua mgongo.

  Marianne anaishi kwenye nyumba moja ndogo mjini Berlin akiwa hana sofa wala kiti baada ya kuibiwa karibia vitu vyake vyote wakati alipokuwa akihama nyumba.

  "Niliibiwa kila kitu kuanzia pafyumu mpaka picha pekee ya mama yangu", alisema bibi Marianne.

  Baada ya kulipa pango la nyumba yake na bili zake za umeme, maji na gesi, Bibi Marianne hubakia na euro 146 kutoka katika pesa zake za kiinua mgongo.
  Pesa hizo ni kidogo sana kulinganisha na gharama za mahitaji yake.

  Bibi Marianne alisema kwamba alikuwa hana njia nyingine ya kujipatia pesa zaidi ya kuuza hazina yake pekee ya picha zake za utupu alizozipiga alipokuwa na umri wa miaka 20 miaka 55 iliyopita.

  Picha hizo huzitunza kwenye bahasha ambayo huificha kwenye droo ya kabati lake.

  "Picha hizi zilipigwa na aliyekuwa mume wangu mwaka 1954", alisema bibi Marianne na kuongeza "Nasikia siku hizi wanaume wananunua picha kama hizi kwenye internet, nahitaji pesa vibaya sana".

  Kama bibi Marianne atafanikiwa kuuza picha zake, ana mpango wa kuzitumia pesa hizo kununua sofa na viti.

  Hajui picha zake zitanunuliwa kwa kiasi gani lakini anaamini kwamba vya kale vina thamani zaidi.
  </SPAN>
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Bibi alikuwa extreme kw kw teh
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  haaaaah
   
 4. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaaaaaaaaaazi kwelikweli
   
 5. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dunia imekwisha...........
   
Loading...