Bibi wa Miaka 107 Anatafuta Mume wa 23 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi wa Miaka 107 Anatafuta Mume wa 23

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 25, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>


  Bibi Wook Kundor

  Bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia ambaye alishaolewa na kuachika mara 21 amesema yuko tayari kuolewa na mwanaume mwingine kwa mara ya 23 kwasababu anahofia kuwa mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine mwenye umri mdogo.


  Baada ya kuolewa na wanaume 21 na kuachika, bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia amesema kuwa anahofia kukimbiwa na mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa ambaye miezi miwili iliyopita alikamatwa akitumia madawa ya kulevya.

  Bibi Wook Kundor alipata umaarufu duniani baada ya kuolewa kwa mara ya 22 na mwanaume ambaye amemzidi jumla ya miaka 70.

  Hivi sasa bibi Wook hana imani kabisa na mumewe Muhammad Noor Che Musa mwenye umri wa miaka 37 ambaye hivi sasa yuko kwenye kituo cha kurekebisha tabia akipatiwa matibabu ya kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya.

  Bibi Wook ameishaanza kusaka mume wa 23 kwani anahofia Muhammad akishatoka kwenye kituo hicho na kuacha tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine wa rika lake.

  "Katika siku za hivi karibuni kuna hofu imeniingia" alisema bibi Wook huku akiwa ameshikilia picha yake.

  "Najua kwamba mimi ni mwanamke niliyezeeka. Sina umbile la kuvutia tena na kwa umri wangu siwezi kumvutia mwanaume yoyote"

  "Nia yangu ya kuolewa tena ni kuepuka upweke na si kwa sababu yoyote ile" alisema Wook na kuongeza kuwa anajihisi mpweke sana wakati huu ambao mumewe yuko mbali.

  Bibi Wook alisema kuwa angependa kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr wiki ijayo akiwa pamoja na mumewe.

  Wook alisema kuwa ana mpango wa kumtembelea Muhammad kwenye kituo chake cha kurekebisha tabia jijini Kuala Lampur iwapo majirani zake watampeleka huko kwa gari.

  Muhhamad alifunga ndoa na bibi Wook miaka mitatu iliyopita akisema kuwa urafiki wa karibu na heshima uligeuka kuwa mapenzi ya kweli.
   
 2. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  bIBI NAYE ANA MAMBO. hAYA KAZI SIJUI BADO ANAWEZA....
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Kazi ipi aisee? Ungefafanua hapo.....
   
 4. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  bIBI AMA MAMBO HUYU? KIJANA HUYO AKIMPATA ATAMTOSHELEZA?
   
 5. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  kUCHEZA SEBENE............ AU KAMA JINA LAKO LA PILI KWAKE LIKO SAWA
   
 6. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Oooh! Ngwasumaaaaah! Nahsi wamo bado....... ha ha ha
   
 7. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mhh....Kiun.....?
   
 8. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo kwa kweli.
   
 9. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo bibi kaeleza vizuri sababu yake ya kutafuta mume: Kuondoa upweke. Ni upweke unamtesa na kumsononesha. Lakini je huyo wa kumwondolea huo upweke bila shaka atataka huyo bibi naye amuondolee tatizo lake lingine fulani, ndiyo kama ile wanaita symbiosis.

  Kumbe basi alikosea kuolewa na mume kijana kiasi hicho, maana wanaume wa marika hayo wanachohitaji kwa wanawake ni kile ambacho pengine huyo bibi hakiwezi tena. Angetafuta mzee mwenzake, babu mwenye shida ya company kama yeye.
   
 10. J

  JackieJoki Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 24, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh kweli hapo kuna kazi, Dr unamshauri nin huyo Bibi
   
 11. J

  JackieJoki Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 24, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Babu mwenzake ata bore sana
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyu Bibi wa ukweli atakuwa amumbwa kwa nguvu zingine zisizo za kawaida ..mika hiyo bado anataka parformance lolo i cant believe kwa kweli bwana
   
 13. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unamshauri apate mzee mwenzake?
   
 14. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu hata 'nanihii' si itakuwa ishaziba? Kama angekuwa na mihela hata hapa najua wadau mngeomba contacts.
   
 15. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa kipi bora, babu na boredom, au kijana na sex urge ambayo bibi haiwezi? Matokeo ya kushindwa kumtimizia kijana ndiyo hayo, kijana ataondoka akatafute saizi yake. Au anakaa kwa bibi kuchuna, akitamani mambo flani anaenda kuhonga wenzie na hizohizo hela za bibi. Na kwa kuwa kwa kinamama wivu ni inborn trait (regardless of age!) bibi atasononeshwa na wivu sana. Hapa bongo tu kwenye magazeti juzi kuna bibi wa miaka 70 alijinyonga alipogundua mumewe mwenye miaka 76 ana kimada 'ndogondogo'!

  Huyo wa miaka 107 atafute mwenzie wa miaka 100, atamfaa maana umri huo hata wanaume jogoo huwa anastaafu, au kama akijitutumua ni mara moja kwa mwaka (ambayo inachukua kama dakika 5 tu, bibi hashindwi kuvumilia hiyo japo na lubrication). Na uzungu nadhani umewavamia hao jamaa kwa kasi, ingekuwa huku Afrika bibi hawezi kusononeka na upweke, maana wajukuu kibao wapo kumpa kampani, anawasimulia hadithi hadi wanasinzia na yeye analala zake.
   
Loading...