Bibi kizee wa miaka 70 nusura azikwe hai Maswa............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi kizee wa miaka 70 nusura azikwe hai Maswa.............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Feb 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Wazee walaani mwenzao kutaka kuzikwa hai


  na Stephano Mango, Songea


  [​IMG] WAZEE nchini wamelaani vikali tukio lililotokea hivi karibuni kijiji cha Ipililo, wilaya ya Maswa, mkoani Shinyanga, baada ya kutaka kumzika hai mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mwana Nandi mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 kwa madai ya uchawi.
  Akitoa tamko hilo jana kwa niaba ya wazee mkoani hapo mbele ya waandishi wa habari, katibu mkuu wa Mtandao wa Kinga Jamii Nchini, Iskaka Msigwa, alisema kuwa walisikitishwa na kitendo cha vijana hao cha kumkamata Nandi na kutaka kumzika kwenye kaburi la marehemu kaka yake.
  Alisema kuwa wanalaani tukio hilo na kupinga vikali kwani ni tukio la kudhalilisha huku likijenga taswira ya kuhamasisha jamii kuendelea kuwanyanyasa wazee kwa tuhuma ambazo hazina uthibitisho.
  “Tumesikitishwa sana na vyombo vya dola kushindwa kutoa tamko la kulaani unyanyasaji huo uliofanywa dhidi ya Mwana Nandi na kwamba hatua hiyo imeonyesha jinsi wazee tusivyothaminiwa na mamlaka mbalimbali,” alisema.
  Alisema kuwa wanataka vyombo vya dola kuchukua hatua kali dhidi ya watu waliohusika na unyanyasaji huo kwa kuwa wanafahamika.
  Alifafanua kuwa takwimu zinaonyesha kuwa wazee 300 wamekuwa wakipoteza maisha kila mwaka kutokana na kutuhumiwa za uchawi na kuwataka wananchi kufahamu kuwa wazee sio wachawi kama wanavyofikiri.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  PHP:
  WAZEE nchini wamelaani vikali tukio lililotokea hivi karibuni kijiji cha Ipililowilaya ya Maswamkoani Shinyangabaada ya kutaka kumzika hai mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mwana Nandi mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 kwa madai ya uchawi.
  Ushirikina ndiyo sababu ya msingi kwa nini nchi hii ni masikini..........................Mwenyezi Mungu hafurahishwi nasi....................
   
Loading...