Bibi Aokoa Mbwa Toka Kwenye Moto, Amsahau Mjukuu Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi Aokoa Mbwa Toka Kwenye Moto, Amsahau Mjukuu Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Mandy Hands aliokoa mbwa toka kwenye moto lakini alimsahau mjukuu wake</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Wednesday, June 09, 2010 2:35 AM
  Bibi mmoja nchini Uingereza alikumbuka kuwaokoa mbwa wake wanne toka kwenye nyumba yake iliyokuwa ikiwaka moto lakini alisahau kumuokoa mjukuu wake aliyekuwa amelala ndani ya nyumba hiyo.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 alisahaulika ndani ya nyumba iliyokuwa ikiwaka moto wakati bibi yake alipokuwa bize kuwaokoa mbwa wake.

  Bibi huyo wa nchini Uingereza, Mandy Hands, 45, alisahau kuwa mjukuu wake alikuwa amelala ndani ya nyumba hiyo wakati alipokuwa bize kunusuru maisha ya mbwa wake wanne.

  Zimamoto waliowahi kufika kwenye eneo la tukio, walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo.

  Mandy anasema kuwa anajuta kumsahau mjukuu wake kwenye moto. "Najisikia vibaya nikikumbuka nilimsahau mjukuu wangu kitandani moto ulipotokea".

  "Alikuja kututembelea toka Portsmouth na kwasababu ya kupaniki nilisahau kuwa yuko hapa", alisema Mandy.

  Moto huo ulizuka jumatatu asubuhi kutokana na hitilafu ya umeme. Mandy baada ya kuona moshi ukiingia chumbani kwake alifanikiwa kumuamsha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16 na ndipo alipoanza kuwaokoa mbwa wake wanne.

  Aligundua amemsahau mjukuu wake ndani ya nyumba hiyo wakati akiwa nje zimamoto walipomuuliza kama kuna mtu yoyote ndani ya nyumba hiyo.

  Zimamoto walifanikiwa kumtoa mtoto huyo toka kwenye nyumba hiyo akiwa hana majeraha yoyote ya moto.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
  </td></tr></tbody></table>
   
 2. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hao wanabusu mbwa hata mdomoni, wakati mbwa litoka kulama sehemu zake nyeti wakati huohuo...umagaribu unaharibu sana akili za watu, anafikiri mbwa naye ni kitu chenye haki kama mwanadamu...wametunga hadi sheria za kulinda hao mbwa ati..ajabu kweli..
   
Loading...