Bibi amchoma mjukuu wake akimtuhumu kuiba Sh5,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mkazi wa Kijiji cha Azimio Kata ya Salawe, Felister Mdoshi amemchoma moto mjukuu wake kwa kutumia mfuko wa nailoni aliomfunga mkononi, akimtuhumu kumuibia Sh5,000.

Licha ya kumfanyia ukatili huo mjukuu wake anayejulikana kwa jina la Elizabeth Mussa (8), mwanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Azimio, bibi huyo aliamua kumfungia ndani kwa muda wa siku 11 bila kumpatia matibabu tangu kufanyika kwa tukio hilo Agosti 13 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Azimio Twiga Mashimba alisema juzi kuwa alichomwa moto Agosti 13, mwaka huu lakini tukio hilo limegundulika Agosti 24 baada ya majirani kutoa taarifa juu ya kitendo hicho baada ya kubaini kilichofanyika dhidi ya mtoto huyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule alipotafutwa kwa njia ya simu juu ya tukio hilo, alisema yuko kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga hivyo hataweza kulizungumzia tukio hilo kutokana na mazingira alipo.

“Tukio hili linasikitisha mtoto huyu kafanyiwa kitendo cha kikatili na bibi yake na sisi tulipopata taarifa tulienda hadi nyumbani kwa bibi huyo na kweli tulimkuta mtoto ana hali mbaya, tulipomhoji kwanini kafanya kitendo hicho alikiri na kudai ana mazoea ya kuiba fedha zake mara kwa mara ndiyo maana kamchoma moto,” alisema.

Mganga Mfawidhi Msaidizi Kituo cha Afya, Salawe Anastazia alikiri kumpokea mtoto huyo akiwa na majeraha makubwa yaliyotokana na kuungua na moto, ambapo alibainisha kuwa hali yake siyo nzuri kutokana na vidonda kuanza kuoza.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Yunis Mazige ambaye alikuwa akiishi mbali na mtoto wake kutokana na kuolewa na mwanamume mwingine, alisema hana chakumfanya kwasababu kitendo hicho kimefanywa na mama yake mzazi kwani alimuamini na kumpa mtoto wake na walikuwa wakiishi vizuri kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.

Diwani wa Kata ya Salawe, Joseph Buyugu licha ya kulaani kitendo hicho, pia alisema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi la polisi.

mwananchi
 
Huwa naamini Mtoto kuwa mdokozi dokozi sababu kubwa huwa ni njaa.
kuna mama mmoja aliua mwanae wa miaka mitatu yupo jela sasa..
mtoto alikua na njaa.chakula cha mchana kilichelewa sababu anakula sawasawa na watu wazima yani mara tatu kwa siku.
sasa mvhana mama yupo jikoni mama anakaanga samaki wa mboga ya mchana.mtoto akapita na kudokoa kipande kidogo..mama akamfuma na kupanic...akamwasha kofi kali kwenye shavu..mtoto akaanguka hapohapo kimyaa!
akaanza kypiga kelele..mara wampempee..wammwagie maji..
kufika hosp docta akamwambia mama mtoto kashafariki zamani tu huyu...

tujifunze kuzuia hasira zetu jamani..mtoto akifanya jambo la kukosea kabla ya kumwadhibu muulize.
 
tujifunze kuzuia hasira zetu jamani
..mtoto akifanya jambo la kukosea kabla ya kumwadhibu muulize.

Hapo ndipo ugumu unapoanzia, watu wengi hatuwezi kuzizuia hasira zetu kwa muda matokeo yake ndio inakuja "ningejua"!

Sijawahi kupiga mtoto maishani mwangu kisa tu eti amedokoa kitu fulani zaidi ya adhabu ndogo ndogo maana najua ni njaa tu ndio iliyompelekea kufanya hivyo.
 
MWANAFUNZI wa chekechea Elizabet Musa (8) anadaiwa kuvalishwa mikononi mifuko ya plastiki kisha kuchomwa moto na kufungiwa ndani siku 11 na bibi yake aliyekuwa akiishi naye katika kijiji cha Azimio, kata ya Salawe, wilayani Shinyanga.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi na bibi yake Felister Mdoshi na alimvisha mifuko ya plasitiki mikononi na kuwasha moto kwa kutumia kiberiti baada ya kumtuhumu kuiba kiasi cha Sh 5,000.

tesa_mtoto_210_120.jpg

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Twiga Mashimba akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa tukio la kuchomwa moto kwa mtoto huyo limetokea Agosti 13, mwaka huu na majirani walipogundua walitoa taarifa, Agosti 24, mwaka huu baada ya bibi yake kufanya kitendo hicho na kumzuia kutoka nje akiwa ndani siku zote amekaa na majeraha hayo. Mashimba alisema mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la awali, shule ya msingi Azimio.

Alikuwa akimfungia ndani nyakati za mchana na humfungulia nyakati za usiku na alfajiri kutoka nje wakati watu wamelala. “Kabla ya kupelekwa kituo cha polisi bibi huyo tulimhoji kwa nini kafanya kitendo hicho, alikiri na kudai kuwa ana mazoea ya kuiba fedha zake mara kwa mara ndio akachukua uamuzi wa kumchoma moto ili kumkomesha asirudie kufanya kitendo hicho… ila mimi nasema kuwa kitendo alichofanyiwa mtoto huyo ni ukatili wa kinyama,” alisema.

CHANZO: Habari Leo
 
Habari Leo ndio wameeleza vizuri. Sasa hao Mwananchi wameeleza Salawe tu hata hawajasema iko wapi...

Huu ukatili haukubaliki.
 
Back
Top Bottom