Bibi abwia unga na kujisi fresh.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Bibi mmoja ambae alikuwa hajisikii vizuri na kuumwa umwa hakwishi alikutana na mjukuu wake ambae ni mbwia unga ila bibi mwenyewe hajui wala hana habari za mambo ya unga lakini hapo nyumbani ndugu wengine wanajua kama ndugu yao wa kiume ni mbwia unga mashuhuri.
Siku moja ilibahatika nyumbani hapakua na mtu ila alibakishwa bibi peke yake sasa kijana mbwia unga kurudi nyumbani akakumbana na bibi yake ,hapo bibi yake akamwaga mashitaka mengi tu ,sijui leo ya ngapi ninaumwa wameshika ndugu zako kunipa vidonge wala havinisaidii hivi mjukuu wangu hiyo tokatoka yako hujapata dawa za maumivu ? Kijana akasema dogo tu hilo ngoja nikakuletee basi akaingia chumbani kwake na kutoka na kiasi kidogo cha unga na kumwambia bibi yake hiyo ni dawa mjarabu kwa maradi ya mwili na viungo ,basi akamwambia anuse kama tumbaku ,bibi bila ya kuyajua mambo ya mjini akavuta na kunusa .Basi baada ya muda kidogo tu alijiona ana nguvu na maumivu yote yametoweka anaimba nyimbo za kale. Kijana huyo akaondoka
,wandugu waliporudi nyumbani wakamkuta bibi yao kalala anakoroma na alipoamka yupo fresh, anazungumza ikawa kazi ni hiyo kijana anampenyezea bibi yake dawa ila siku moja jamaa alikuwa hayupo kwa siku mbili sasa bibi maradhi yakaanza kumrudia na kumuulizia kijana yupo wapi ampe dawa wandugu wakamuuliza dawa gani hiyo akikupa akawaambia hata siijui ila ananiwekea kwenye kiganja na kuniambia nivute kama tumbaku na hapo hujisikia mzima tena ninakuwa kama nipo peponi mambo yote kwangu ni mazuri ,dah wandugu wakamaka na kusema ameshakupa unga na ni kitu kibaya sana ndio unasikia kuwa kuna watu wanakamatwa sababu ni unga huo unaharibu akili na baadae kukuleetea mzubao ,bibi yule kusikia habari na visa vya unga wacha arapu na kumtukana mjukuu wake bila fulustopu.
 
Back
Top Bottom