Biashara zangu 5 za wakati wote kwa Dar

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
4,625
2,000
Dar ni sehemu ninayowambia watu wengi sana kuwa kama atashindwa kutafuta maisha eneo hili basi ana safari ndefu sana ya kufanikiwa,ni sehemu ambayo biashara nyingi zinakubali na zinakutoa kwa kipindi kifupi kama ukiamua kujitoa Afe kipa Afe beki.

Nimeona biashara nyingi sana ila hizi ni biashara zangu 5 ambazo mtu mwenye mtaji wa Laki 5 kushuka chini anaweza akazifanya zikamtoa haraka kuliko mategemeo yake yeye.

1.Kuuza Majiko ya Mkaa

Majiko ya mkaa ni biashara ambayo wengi hawaifikirii,sijui ni kukosa elimu ya kutosha jinsi ya kuifanya hii biashara au vipi huwa sielewi kwann hawaifanyi wakati ni biashara inayoweza kukurudisha nyumbani jioni na faida isiyopungua 15,000 na wakati mwingine mauzo kufika mpk 100,000.

Biashara hii haitaki mtaji mkubwa maana majiko bei ya jumla yanauza 1500,2000,3000,nk ambapo unaweza ukachanganya kuweka na vinu,mitwangio,mifuniko ya sufuria ile ya kawaida ya aluminium,mabanio ya mkaa,ungo(nyungo)nk biashara hii kuyumba ujiyumbishe mwenyewe ila sio wateja.

2.Vinywaji

Uuzaji wa vinywaji dar ni biashara inayotoa watu wengi sana,hapa hatuchanganyi biashara nyingine yeyote ni vinywaji TU maana yake ni kwamba dukani friji lako unalijaza juice zote zinazouzwa chini ya 1000,maji yote yanayotengenezwa Dar,(bila kusahau super kandoro)soda zote,nk

matokeo ya hii biashara ni kwamba wakati wenzako wanalia hali mbaya wewe utalia nao ila utalia si kwamba utakua mfukoni huna kabisa hela au umefungua biashara hujafanya kabisa ila utalia kwasababu ulikua umezoea faida kubwa ila sasa imepungua,ni biashara bora sana kwangu hii.

3.Viungo Vya chakula/Chai

Biashara hii ni biashara nzuri na bora kwangu na naipenda sana kwa sababu ni biashara ambayo viungo unatengeneza mwenyewe,unapaki mwenyewe,unaweka taste unazotaka wewe na kizuri kupita yote Bei unapanga mwenyewe,ukitaka elewa kwann nimeipa hii biashara heshima IFANYE.

4.Gesi

Hapa naongelea gesi za kupikia majumbani kama oryx,mihan,lake,taifa,nk hii biashara mimi naiita BABA LAO ni biashara flani ya kibabe sana inayoweza kukufanya uwe na jeuri mjini Japo ili ufaidi hii n lazima mtaji atleast usiwe chini ya 800,000 na ujue nini unafanya ktk biashara,maana gesi zipo kila kona ila kufanya watu waje kwako yahitaji ujue unachokifanya.

5.Chakula

Hii biashara hai hitaji promo kukwambia kama inaweza kukutoa au haiwezi,najua wapo mliofanya hii biashara ikawapga amba kati (poleni) leo naongelea kwa upande wangu mimi,nionavyo mimi si lazima iwe sawa kwako ila Biashara ya chakula ni biashara bora kwa wakati wote.

Hizi ndio TOP 5 zangu ukitaka kujua kwann nimezipa TOP 5 ingia zifanye hizi biashara then tuleteane mrejesho,vigezo na masharti ili biashara yyte iende vizuri lazima vizingatiwe.
 

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
6,525
2,000
Controla...ipo siku ntakurushia kibunda ki1 cha asante..sabab kupitia mabandiko yako nmefanikiwa kufungua biashara 3 tofaut tofaut na zinaendelea vzur kiukwel

Moja ni ile ya kukodisha mabanda ya biashara..nilitengeneza mabanda ma 4 tho yalinicost tofaut na nilivokadiria.banda moja lilikula kama 1.2 hiv..ila nilifanikiwa yote kuyakodisha na kula kodi ..

Nili fight kuyaweka sehem nzur sana tofaut tofaut..nakula kodi now..kodi ndogo kabisa kwa mwez nakula 100k..mengne nakula 150k...kwa moja

Asante mkuu..ntakutafta......kuna biashara moja nyingne nataka iongeza ila nna mashaka nayo...
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,324
2,000
Dar ni sehemu ninayowambia watu wengi sana kuwa kama atashindwa kutafuta maisha eneo hili basi ana safari ndefu sana ya kufanikiwa,ni sehemu ambayo biashara nyingi zinakubali na zinakutoa kwa kipindi kifupi kama ukiamua kujitoa Afe kipa Afe beki.

Nimeona biashara nyingi sana ila hizi ni biashara zangu 5 ambazo mtu mwenye mtaji wa Laki 5 kushuka chini anaweza akazifanya zikamtoa haraka kuliko mategemeo yake yeye.

1.Kuuza Majiko ya Mkaa

Majiko ya mkaa ni biashara ambayo wengi hawaifikirii,sijui ni kukosa elimu ya kutosha jinsi ya kuifanya hii biashara
Binafsi naona biashara nyingi zinakuwa kwenye kipindi cha "Kujitafuta"

Unaweza kuona biashara inawapa watu wengi faida lakini ukifanya wewe "ikakukataa" kabisa.

Watu wengi biashara fulani ziliwatoa baada ya kujaribu biashara kadhaa.

Pale utakapoona biashara fulani imekukubali komaa nayo.
 

Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,977
2,000
Majiko ya Mkaa+Majiko ya Gesi+Chakula+Viungo vya Chakula=ITAPENDEZA ZAIDI
 

Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,977
2,000
Location + Kujitangaza + Bidhaa Bora = Super Profit
Ni kweli kabisa japo si biashara zote zinataka location

muhimu n ujue jinsi ya kujitangaza,hata kama upo uvunguni

watu watakufata wakuulize kuhusu bidhaa yako unayouza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom