Biashara za magendo zinaongezeka kwa kasi nchini kwa sababu ya mfumo wa kijeshi wa kukusanya Kodi

fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
10,199
2,000
Mwaka 2012 nilijifunza kuwa na records za mawasliano yote, malipo na documents zangu zote ninazowapa TRA. Chochote kiwe malipo au mawasliano yawe ya maandishi au maneno nina records kamili.....maana staki kuingia gharama nikiyowahi kuingia
Mama D kuna siku utawa juwa hao jamaa ni mahakimu wasio kuwa na sheria inayo kupa nafasi ya wewe kujitetea wata kuhukumu watakavyo wao!
Wata kukuta na kakosa kadogo tu cha kibinaadamu apo watageuka kuwa mashetani tiari kwa kukuhukumu bila huruma
 
kitonsa

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
784
1,000
VAT wanachukua 18% ya mauzo yote, wakati walitakiwa wawe wanachukua asilimia 18 kwenye faida yaani ukizembea hapo kwenye VAT wanapita na mtaji wako bila huruma,
kwa hiyo kama mtaji wangu ni sh mia nikauza nikapata sh. mia kumi na nane , tra wanalamba hivyo kumi na nane?

hapo sijala ,nauli ,pesa kulipia choo cha soko juu yangu?
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,408
2,000
Mama D kuna siku utawa juwa hao jamaa ni mahakimu wasio kuwa na sheria inayo kupa nafasi ya wewe kujitetea wata kuhukumu watakavyo wao!
Wata kukuta na kakosa kadogo tu cha kibinaadamu apo watageuka kuwa mashetani tiari kwa kukuhukumu bila huruma
Wajibu wa TRA ni kuwasaidia wateja wake kuwapa miongozo sahihi ya kukuza biashara kwa kuwapa elimu pale wanapofanya makosa ya kiutendaji lakini bahati mbaya vijana wengi watendaji wa TRA wanawategeshea wateja wafanye makosa ili wawaadhibu.
Wanasahau kazi waliyotumwa, wanasahau baadhi ya adhabu za makusudi za kutegeshea wateja zinawahusu hata wao maana zinadhihirisha utendaji wao wa hovyo.
Ifike mahala wawajibike pale inapojulikana kwamba biashara imefungwa kwa uzembe wao
 
am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
534
1,000
Nilipokua chuoni nimeshuhudia vilaza wengi sana wakiajiriwa,sijui ni bahati ama connection lakini ukweli ni kwamba serikalini vilaza ni wengi sana na ndio chanzo cha haya mambo ya hovyo yanayoendelea,

Mifumo ya ukusanayaji kodi ilitakiwa ifanye watu walipe kodi pasipo kuleta mvurugano kwenye biashara,tatizo la sasa ni hao waliopo maofisini kuanzia juu mpaka chini ni zero.

Tanzania ya sasa TRA anaogopwa kuliko mwenyezi Mungu,

Naishauri serikali iongeze kujenga magereza kila wilaya na kila Kijiji kwani taratibu za kodi za utawala huu zitapelekea wafungwa kuongezeka kiasi cha mahabusu na magereza kuzidiwa.

Mlipaswa kujiuliza hivi licha ya adhabu kali zitolewazo kila siku,watu wanafungwa na wengine mnawapiga faini lakini watu ni kama hawasikii,kwanini?

Yani ni kama vile mtunge sheria kwamba ni marufuku kufanya mapenzi na yeyote atakayekamatwa kifungo ni miaka mitano,mnafikiri watu wataacha kujamiiana?

Yani serikali ya sasa yenyewe ni nguvu mbele akili nyuma,wakisikia watu wanalalamika maisha magumu wao ndio wanaona wamefanikiwa,kweli maajabu hayaishi duniani.
Umenikumbusha ule usemi ukitaka kumshika faru nyeti zake uwe na uhakika na mbio zako......ndukiiii
 
Abdulwahid

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,557
2,000
Na hua hawasikii kabisa hata tukilalamika vp, sijui wamekusudia nini, mfanya biashara nchi hii amekua kama mhaini
 
Nowonmai

JF-Expert Member
Jan 15, 2019
661
1,000
Asili haikubali uwepo wa ombwe.

Kama kuna bidhaa au huduma yoyote inayohitajiwa na watu na haipatikani kihalali kwa sababu yoyote, ikiwamo kodi zisizo na mpangilio, itapatikana kwa magendo.

Kodi na kifo ni vitu vya kudumu katika maisha lakini kodi zisizo na kichwa wala miguu zitaishia kuleta uhaba wa bidhaa na huduma na sana sana kutajirisha wafanya magendo na wala rushwa.
 
baraka bb

JF-Expert Member
Mar 20, 2016
2,543
2,000
Kodi watu wanapenda kulipa lakini kama watafuata ushauri wa Rais Mwinyi wa kukusanya kodi kidogo kwa watu wengi itasaidia kuliko kodi kubwa afu unakusanya kwa watu wachache na kodi mfumo wake haupo wazi ushaona wapi mtu unaanza kulipa kodi ndio ufanye biashara?
Yaan ilo swala la kulipa kodi kabla ujafungua biashara hata mm liliniachaga kinywa wazi,,,, eti ukienda kuomba TIN namba ya biashara wanakukadilia kabsa kodi ukalipe thn ndo wakupe TIN
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,051
2,000
Kuna member alisema hatofanya biashara yeyote ambayo inaingiliana na TRA kwa kipindi hichi.
ipi hiyo
FB_IMG_1610789963236.jpg
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
2,950
2,000
VAT analipa mtumiaji wa mwisho, haina uhusiano na turnover au mtaji wa mfanyabiashara. Mfanyabiashara ni wakala tu wa kuikusanyia serikali.
Hii dhana ni ngumu sana kwenye mfumo wa tz,
Si muache CCM iwaudhi wananchi ili waichukie na kuwachagua nyinyi ili mrekebishe mambo ili nchi iwe ya maziwa na asali.
Kelele za NINI?
Wewe unaota!
Kwenye sanduku la kura sahau kuiondoa kijani madarakani,chaguzi za nchi nyingi za Africa ni danganya toto,hakuna uchuguzi ulionifumbua macho kama uchaguzi uliouingiza serikali ya awamu ya tano madarakani,nimepata bahati ya wadogo zangu na majamaa wakaribu kupata nafasi za kuwa mawakala,yani kilichokuwa kinafanyika ni kituko.

Huwa sielewi ninapomsikia mkuu anapohutubia kila baada ya mstari mmoja anamtaja Mungu,ukweli ni kwamba kama pepo ipo basi mtashangaa kuwakuta majambazi peponi na wale tunaowaona wema motoni.
 
Copy

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
653
1,000
VAT analipa mtumiaji wa mwisho, haina uhusiano na turnover au mtaji wa mfanyabiashara. Mfanyabiashara ni wakala tu wa kuikusanyia serikali.
Naomba nieleweshe kidogo hapo mkuu. Maana naogopa mwaka huu nahisi nitaingizwa kwa mfumo wa VAT, japo aliyeniambia hakunifafanulia nikaelewa. Nami nimezoea mfumo wa makadirio tu.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,647
2,000
Wajibu wa TRA ni kuwasaidia wateja wake kuwapa miongozo sahihi ya kukuza biashara kwa kuwapa elimu pale wanapofanya makosa ya kiutendaji lakini bahati mbaya vijana wengi watendaji wa TRA wanawategeshea wateja wafanye makosa ili wawaadhibu.
Wanasahau kazi waliyotumwa, wanasahau baadhi ya adhabu za makusudi za kutegeshea wateja zinawahusu hata wao maana zinadhihirisha utendaji wao wa hovyo.
Ifike mahala wawajibike pale inapojulikana kwamba biashara imefungwa kwa uzembe wao
Hio elimu utapewa kwa njia ya kutandikwa fine za kukumaliza kabisa mchezoni. Una mtaji wa 15M unapigwa fine ya 35M utatoboa?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,647
2,000
Yaan ilo swala la kulipa kodi kabla ujafungua biashara hata mm liliniachaga kinywa wazi,,,, eti ukienda kuomba TIN namba ya biashara wanakukadilia kabsa kodi ukalipe thn ndo wakupe TIN
Nilikadiriwaga laki 1 nikatoka mbio 🤣🤣🤣 na wala ile laki sikupeleka niliishia kuandika barua kuwa biashara haikufanyika. Nika submit wa ofisi ya regional officer sasa sijui aliijibuje maana sikufuatilia.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,006
2,000
Wajibu wa TRA ni kuwasaidia wateja wake kuwapa miongozo sahihi ya kukuza biashara kwa kuwapa elimu pale wanapofanya makosa ya kiutendaji lakini bahati mbaya vijana wengi watendaji wa TRA wanawategeshea wateja wafanye makosa ili wawaadhibu.
Wanasahau kazi waliyotumwa, wanasahau baadhi ya adhabu za makusudi za kutegeshea wateja zinawahusu hata wao maana zinadhihirisha utendaji wao wa hovyo.
Ifike mahala wawajibike pale inapojulikana kwamba biashara imefungwa kwa uzembe wao
Nani wa kiwawajibisha?
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,119

Kwa mfumo wa kodi wanazopiga TRA unapofanya biashara unafikiri unaweza ukatoboa?
We jiulize kwanini watu wanafanya magendo kwa kupitisha bidhaa nk yote ni kukwepa makodi makubwa.....mtu anamua kucheza kamali tu
Na watu wengi wametajirika kwa style hiyo
Magendo itaendelea kuwepo na kuwepo

Ova
 
baraka bb

JF-Expert Member
Mar 20, 2016
2,543
2,000
Nilikadiriwaga laki 1 nikatoka mbio na wala ile laki sikupeleka niliishia kuandika barua kuwa biashara haikufanyika. Nika submit wa ofisi ya regional officer sasa sijui aliijibuje maana sikufuatilia.
me nilijichanganya nilienda mbeya nikafungua ki grocery kodi nikakadiliwa laki nne,, nilifanya ile biashara mwaka mmoja tu nikafunga mbaya zaid sikutoa taarifa kama nimefunga nikarudi dar

siku naenda ku update TIN namba yangu naambiwa nadaiwa laki8 hapo sijafanya biashara kama miaka miwili nyuma niko shock kinouma

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,300
2,000
Naomba nieleweshe kidogo hapo mkuu. Maana naogopa mwaka huu nahisi nitaingizwa kwa mfumo wa VAT, japo aliyeniambia hakunifafanulia nikaelewa. Nami nimezoea mfumo wa makadirio tu.
VAT inatolewa kwa mfanyabiashara ambaye mauzo yake ni m100 kwa mwaka ama m50 kwa miezi sita(mauzo si faida). Kinachotokea ukiwa wakala wa VAT hakikisha mzigo wako ukinunua unanunua kwa mtu mwenye VAT ili utakapouza na ww utoe VAT. Usikubali kupewa risiti isiyo kamili(naamini unaelewa maana ya neno risiti kamili). Ukifanya hivyo VAT haitakuumiza kabisa ww mfanyabiashara maana utakaponunua utailipa kisha utakayemuuzia atakurudishia. Tofauti ya 18% ya mauzo na manunuzi ndiyo utakayoipeleka TRA. Faida yako haitaguswa kabisa na VAT. Ukifanya tofauti utaichukia sana VAT na maisha yako yote yatakuwa ya kujificha ficha TRA wasikutane na wewe.
 
Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
804
1,000
Nkiangalia Kenya anavyofaidika na soko la mirungi hapa Tanzania kwa njia za magendo ndio najua huwa tunapoteza mapato kiasi gani. Najua hilo zao limekatazwa ndani ya nchi lkn tunawafaidisha wenzetu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom